Jicho la nne ono la njia ya kuzimu

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,843
Binadamu ana macho mawili ya kawaida.... Yanayoona vitu vya kawaida kabisa visivyohitaji darubini ama hadubini kuona... Ndio macho tunayotumia kila siku kwenye maisha yetu kuona tunavyotaka kuviona na tusivyotaka kuviona pia.... Ni kupitia macho haya ndio tunaweza, kuangalia, kutazama na hatimaye kuona... Kwakuwa tunaweza kuangalia au kutazama lakini tusione....!!!! Macho haya wote tunayo tunayaita macho ya kawaida.. Hata wenye ulemavu wa uono wanayo

Halafu tunakuja kukutana na kitu kinaitwa jicho la tatu... Hili huwa moja tu.... Linatambulika kama jicho la kiroho... Lionalo zaidi ya kuona.. Lionalo zaidi ya darubini na hadubini... Ni jicho lenye uwezo wa kuona yajayo... Uwezo ambao macho ya kawaida hayana.... Jicho la tatu ni maalum kwa watu maalum.. Si kila mmoja wetu anauwezo wa kulimiliki hili jicho

Macho hayo matatu yote yako kwenye upande unaoelezeka zaidi... Lakini kama tujuavyo dunia Ina uwili... Yani kila kitu kina kinyume chake.... Ama uwili wake.... Kwenye hili la macho uwili wake sio jicho la kushoto ama kulia, ama lile jicho la rohoni... Kuna jicho lingine tofauti kabisa jicho lisilo na mboni, jicho butu lenye kipenyo.... Jicho la ajabu hili....!!!!

Hivi ulishawahi kusikia watu wanaume wakisimuliana kuwa.....
Wamekula jicho?
Ama wakisimuliana utamu wa jicho?
Au wakilisifia jicho?
Naamini hizi si habari ngeni kwako.... Jicho ndio habari ya mujini.... Lakini je unafahamu tafsiri ya jicho hili? Hili ndio jicho la nne la mwanadamu ukiacha yale mawili ya kawaida na lile moja la rohoni....
Jicho hili la nne ndio ono la mlango wa kuzimu... Hufunguka tu pale linapochungulia mlango wa kuzimu... Rejea hii mada....

https://www.jamiiforums.com/index.php?threads/1251985/

Cha kushangaza mno ni kwamba dunia ya sasa ushabiki wote ni kwenye jicho la uono wa kuzimu.... Je unabii utajirudia? Maana miji ya Sodoma na Gomora iliangamizwa kwa sababu ya watu kupenda mno jicho la uono wa kuzimu.....

Jicho la nne.... Tunaziishi enzi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom