Jicho la Tatu (The Third Eye)

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
75,055
156,674
JICHO LA TATU!

312218268_10219297406465377_1646917980003385092_n.jpg

Binadamu ameumbwa na milango mitano ya fahamu, macho, ngozi, masikio, pua na ulimi(mdomo?)Hivi vinamuwezesha kutambua yanayoendelea katika ulimwengu wa mwili!!

Ili kutambua yanayoendelea katika ulimwengu wa roho mtu anatakiwa kupata uvuvio wa jicho la tatu,hili ndilo litakuwezesha kupata hisia zaidi ya zile zilizo za kawaida katika mwili!

Jicho la tatu hufanya kazi kupitia ndoto, jicho la tatu linaweza kukupa taarifa mchana kweupe juu ya Jambo litalojiri muda si mrefu, jicho la tatu ni ufunguo wako kuelekea dunia isiyoonekana, nje ya mwili!

Umewahi kuona mtu ameahirisha safari na alikata tiketi basi fulani lakini dakika za mwisho anaahirisha safari ile na ukimuuliza sababu Hata yeye hajui? Na masaa machache baadae utasikia basi lile lile limepata ajali na Watu wamekufa?

Wengine husukumwa na jicho la tatu kutambua yanayojiri baadae wakayaepuka bila wao kujua, wengine wameweza kujiunganisha na jicho la tatu hata wakawa na uhakika na yale yatarajiwayo!

Jicho la tatu linakuunganisha na anga lako(cosmos), linakuunganisha na satellite ambazo Mungu ameziweka zikuongoze duniani!

Ukitambua kuwa mambo mengi yanayotokea katika ulimwengu wa mwili yameratibiwa ama kukamilishwa katika ulimwengu wa roho, basi bila Shaka utaanza kujifunza kutambua na kutumia milango huu wa sita wa fahamu uitwao JICHO LA TATU, Mimi mwenyewe bado ni mwanafunzi!

Ufahamu wa jicho la tatu haujafungwa katika Dini fulani ama imani, umefungwa katika ujuvi na matendo, mfano dini ya kibudha maarufu katika mashariki ya Mbali(China, India, Japan, Mongolia nk) hawa wamejifunza kuutumia mlango huu kwa kufanya MEDITATION!

MEDITATION ya Wakristo na waislam ni kusali na kufunga, sala na fungo hufungua kope za jicho la tatu, ni darasa pana! Mimi pia ni mwanafunzi!!!

NSAJI MWASEGE
 
Back
Top Bottom