Mimi nafikiri hatuna tena sababu ya kuwa na muwakilishi (mbunge) mmoja. Nafikiri wawe wa muda na kwa ajili ya sababu maalumu na kila wakati wawe wanachaguliwa hiyo shughuli ya kiuwakilishi ikiisha na uwakilishi wao unaisha. Hatuwezi kuwa na wawakilishi ambao ni jack of all trades. Ikiwa ni mambo ya bajeti aende akatuwakilishe muhasibu, ikiwa ni mambo ya sheria aende akatuwakilishe mwanasheria, ikiwa ni mambo ya kawaida waende hao wenye elimu ya darasa la saba. Nafikiri tuache kukariri, wachaguliwe kwa sababu fulani na sababu hiyo ikiisha uwakilishi wao uishe hapo hapo. Mathalani hakuna vikao vya bunge hao wabunge wanawawakilisha wananchi kwenye kitu gani? labda huko mnadani kwenda kula nyama