Sanctus Mtsimbe
R I P
- Jul 14, 2008
- 1,820
- 1,036
- Thread starter
-
- #81
If my understanding is accurate, in trying to be everything to all graduates -labor union, financial institution, professionals club, grassroot pressure group- I have a feeling this organisation will have the effect of diluting whatever it is capable of achieving.
To illustrate, how will TPN effectively assist and organize members of different financial background, disciplines, political affiliation, within different labor markets?
IMHO, TPN will do well to review it's mission and define it's purpose, strategies and operations in fine detail, if possible with case examples to illustrate the abstract into the practical.
The bit about forsaking the comforts of anonymity is at best unwelcome, at least on my part.I am sure a multitude in here subscribe to this ghost culture.I know too much about certain clutching claws capable of catching cavalier cats callously.
Another thing, in view of your guild's distinguished membership eligibility roadblocks, you may want to project a commensurate image, especially where proofreading is at issue
IMHO, the English use "Individuals of sound mind...." or "An Individual of sound mind"
Even "Individuals who are of sound mind..." and/ or "An Individual who is of sound mind" are acceptable, albeit grammatically ugly and uneconomic, to say the least of the absence of any betrayal of Etonian lineage (I doubt it was intended) 🙂.
Hata sijui namna ya kusaidia ili kuboresha organization kama hiyo. Tatizo lililoko mbele yangu ni pale mnaposema Tanzania Professionals, halafu mnasisitiza kuwa lazima mwanachama awe na elimu ya juu. Mtu kuwa professional siyo lazima awe na digrii, kinachotakiwa ni mafunzo na ujuzi wa profession yake. Kuchoma vyuma (welding) ni profession, Uhunzi ni profession, uashi ni profession, kucheza mpira ni profession, kunengua mziki wa shoo kama wale akina dada wa Twanga pepeta ni profession, kupiga mziki kama wafanyavyo akina banana, ray C, Jay D, Q Chila, TID na wengineo pia ni profession. Je utaiitaje organization yako kuwa Tanzania Professional huku ukiondoa hizo professions nyingine.
Ninachoona hapa ni kuwa mnachukulia professionals kama ni wahandisi, wanasheria, madakatari wa tiba, wahasibu (na wataalamu wengine wa taaluma za bishara) na kadhalika.
Halafu sielewi una maana gani unaposema financial empowerement, je ni kudai walipwe mishahara mizuri au ni kuwatafutia mikopo ile wafanya bishara ziendazo na professions zao?
hata hivyo, asante sana kuwa kupigania maslahi ya professions mbalimbali lakini ni lazima muwe broader katika ku-define professions. Kubagua professions nyingine ndiko kunasababisha zisithaminiwe wakati ni za muhimu sana katika jamii.
Naomba ufafanuzi kabla sijakukurupukia.
Mr. Mtsimbe you are handling matters very presidentially in this thread. It seems to me that those who gave you the presidency did no mistake. Keep it up.
Tunaposema mtu yeyote mwenye positive attitude tuna maana yule ambaye masuala ya kimaendeleo atakuwa anayaangalia kwa mtazamo chanya badala ya mtazamo hasi.
All professionals - Mkuu hili nimelitolea sana maelezo kama umesoma baaadhi ya responses zangu . . . . LOL. Hata hivyo maana ya Professionals katika katiba ina maana wale waliosomea fani fulani, lakini pia wale wenye ujuzi katika fani yoyote bila kujali elimu yake.
Tumekubali kuwa hili linahitaji marekebisho na kuboreshwa zaidi katika Katiba ya TPN.
Sanctus, karibu sana. Nakumbuka tumewahi kuwa mawasiliano huko nyuma. Miye nawaunga mkono kabisa. Tatizo langu ambalo kidogo umeligusia hapo juu linatokana na mchanganyiko wa jina na mission yenu.
Jina linasema ni "Tanzania Professionals Network"; katika kulielewa hili mnasema katika membership kuwa ni "
Membership is open to Tanzanian Graduates from a higher Institution of learning. There also is membership for corporate organisations and honorary membership"
sasa hili lina matatizo kadhaa:
- Je wahitimu ambao siyo Watanzania na wanafanya kazi katika Tanzania wakiwa na leseni au vyeti vya kitaaluma vya Tanzania hawaruhusiwi kuwa full membership au wanapewa huo wa heshima? Kw. Madaktari, wahandisi, washauri n.k?
- Je wale waliohitimu katika vyuo ambavyo si Higher Learning (kwa maana havitoi shahada labda vyeti tu) kama waliosomea fani za Ukatibu Muhtasi, Ukarani wa Mahakama n.k hawastahili kujiunga na mtandao huu kwa sababu hawakujiunga na Higher Learning Institutions?
- Jina linasema ni "Professionals" lakini kama ambavyo niliwahi kulisema hili awali ni kuwa professionals siyo sawa na intellectuals au wanataaluma. Kama lengo ni kuwa mtandao wa wasomi basi siyo kila mtu aliyehitimu higher learning anaweza kuwa kweli kwenye kundi la wasomi. Msomi, ni mtu aliyebobea katika elimu ya fani yake, unless kuna haja ya kudefine mtaaluma ni mtu mwenye sifa gani. Siamini kuwa kila anayetoka na shahada ya kwanza anaweza kujiita msomi. Usomi wa mtu siamini kama unaweza kupimwa kwa kuangalia alivyograduate isipokuwa kwa kuonesha mtiririko wa kazi, uzoefu na mchango wake wa kitaaluma katika fani yake.
- Lakini inaposemwa kuwa ni "professionals" kwa mtu mwingine inaonekana ni pana zaidi kuliko definition ya "graduate". Je fundi seremala ambaye amejifunza useramala alipokuwa sekondari na baada ya kazi na uzoefu wa muda mrefu amekuwa ni gwiji katika fani yake anaweza kuwa memba? Jibu langu kwa haraka ni hapana, kwa sababu hajagraduate. Lakini tukiuliza is he a professional? the answer is in the affirmative. Sasa kama ni professional na mtandao ni kwa ma professional kwanini yeye haingii?
- Kwa kutilia mkazo elimu ya kizungu (western education) na jinsi ambavyo tunatambua mtu kasoma (kwa kuonesha cheti) mtandao unatenga jamii kubwa ya professionals wa tanzania ambao hawakuhitimu katika vyuo vyenye mfumo wa kizungu lakini wamejifunza kupitia kile kinachoiwa "the school of hard knocks". Ipo haja ya kuangalia jinsi gani hawa nao wanaweza kushirikishwa.
- Kwa vile mnasema mission ya TNP ni "To stimulate and promote effective use of the POWER OF THE BRAIN among Tanzanians in addressing and solving their various Social, Cultural, Economical; Developmental and Psychological Problems" inaonekana kuwa Brains ambazo kwenu zina uwezo wa kuaddress and solve hayo mliyoyataja ni zile zilizograduate tu. Je hakuna watu wengine wenye bongo ambazo ziko sharp na mchango wao unaweza kuhitajika katika mjadala huu lakini hawakupitia katika vyuo vya mfumo wa kimagharibi ili kuthibitishwa kuwa wamesoma?
Ninachoona kwa upande wangu ni kuwa, kama hii ni taasisi ya wasomi wa vyuo vikuu, basi itajwe hivyo na kuwa "Tanzania Intellectual Society" or a "Network of Tanzanian Intellectuals" or "The Association of Tanzanian Academicians" or similar titles. Mkifanya hivyo basi wengine tujua tunaingia katika taasisi gani au kama tutaona hatustahili kuingia kwa taasisi hiyo. Lakini kama lengo ni professionals wa Tanzania, ipo haja ya kuredefine na kupanua wigo wa maana yenu na wito wenu.
Sanctus,
Kuna bwana mmoja namfahamu mbongo katengeneza hizi sites hii hapa na ingine hii hapa niandikie email au PM nitakupa contacts zake email yangu taskmgt@gmail.com.
Naomba tena ufafanuzi.
Nisichotaka kuruka kukisema kabla sijapata ufananuzi mzuri ni kwamba wewe Raisi wa chama cha watu wenye digrii na mashirika ya biashara unashindwa kueleza hata qualification za uanachama. Utawezaje kufanya makubwa zaidi?
Kwamba unataka kuonekana kwamba ni cha wote wakati sivyo.
Sitaki kuruka kusema kwamba wewe sio mkweli kabla hujafafanua.
Unasema chama chenu cha wenye digrii na mashirika ya biashara ni cha wote kwa sababu kuna lile kundi la tatu, la honorary membership. Hiyo honorary membership unapewa kwa heshima au yeyote anapata? Kama yeyote anapata basi clause ya qualification za uanachama kwa nini ina neno "uhitimu"? Ni katiba yenu au wewe Raisi ndio hau make sense?
Raisi naomba utumie nafasi nyingine tena kufafanua ni nani anakubaliwa kundini mwenu.
Au, ahidi kwamba maneno matamu yako mlisahau kuyaweka kwenye katiba na mtayaweka. Isipokuwa kama neno la Rais ndio Katiba.
Assuming wewe ni Rais.
Maana umesema tuwasiliane kupitia barua pepe president@tpn.co.tz
Kwa mtaji wa hiyo email address, unaweza ukawa Katibu au karani mpokea barua wa Rais.
Naomba jitambulishe wewe nani kwenye chama cha waliohitimu na Mashirika ya Biashara.
Tena.
Maelezo bado yananipa maswali mengi kuliko majibu.... tupo pamoja bado Sanctus.
Bado napiga hatua na I sincerely hope that there will be light at the end of the tunnel.
Hongereni sana kwa hili. Lifanikiwe.
Je na mafisadi ambao wameshathibitika kwa asilimia 80 wanaruhusiwa kujiunga TPN? je kuna sheria zozote za kuhakikisha mnawafilter out members wanaojihusisha na ufisadi? Inaonyesha kuwa wengi wa mafisadi ni graduate an corporate elites.
Mama umefika... umenipa burudani kwa hiyo input yako. Ni ukweli mtupu.
Jambo jengine kwa Mzalendo mwenzangu Mtsimbe, hapa tumekuwa tukienda hoja kwa hoja na wewe kuanzia asubuhi na mapema, na so far umeiwakilisha vema TPN. Unahitaji pongezi.
Lakini je huwezi kuwa na member mwengine wa TPN ambae ni mwanaharakati wa JF ili nae/nao waweze kuchangia katika hili ili sisi tuweze pata mwanga zaidi? jaribu kuwaalika katika mjadala huu, ama kama utaniruhusu naweza watumia mail members wote kupitia ile mailing list yenu kisha waje hapa katika mjadala tupate mambo kwa wingi na undani zaidi.
Mie binafsi nimeridhika kwa maswali na duku duku zangu na pia kama anavyosema Mzozo wa Mizozo unahitaji pongezi kwa kutumia siku yako ya leo na mda mwingi kujibu maswali na duku duku mbali mbali. Keep it up Bro! kama wenzako wa TPN wanaweza basi wakupe tafu kidogo, hapa watu tunalala na kukesha hapa!! LOL usiogope lakini!
Nakushukuru sana Sir Mtsimbe, kama kuna waliokuunga mkono huko JF nadhani ni watu wazima na wanajua walifanyalo. La msingi ni kuwa malengo ya hizi community mbili ama community hii na TPN Org yanaweza kufanana lakini njia za kufikia malengo ziko tofauti sana, sasa member wa JF akienda TPN unamtaka abadili namna ya kujishughulisha kama hatapenda kujulikana maana ukiwa TPN huwezi kupiga kelele, vinginevyo utashtukiwa...? Ukiwa TPF huwezi kutoa siri unazozijua, utashtukiwa...? Huwezi kusema lipi linawezekana maana utaulizwa ushahidi ambao utafanya watu wagundue wewe unajua mengi...? na kama ulishayasema mahala pengine..., ndio umenaswa hivyo...! Those JF concretes shall remain Rigid in order for JF to remain strong and loud.
Katiba haiendani na maelezo yako. Nimeyasoma yalivyojipinga. Ndio maana nikaomba ufafanuzi.
Ahsante.
Swali langu la mwisho, kama jibu lako halitazua maswali mengine. Kama utajibu:
Je, matatizo ya Katiba yako umeyajua hapa leo, au hata kabla ya kuja kuinadi hapa bila ku disclose toka mwanzo kwamba the seminal document yenu ina mushkeli katika kutueleza nyinyi ni kina nani na mnakubali kumkaribisha nani katika chama chenu cha Wenye Digrii na Mashirika ya Biashara kama ilivyo sasa mpaka hapo mtakapofanya amendment.
Ahsante tena.
Sanctus..
Umefanya kitu kimoja ambacho ni very rare hapa.. you didn't snap! labda kuja kwa jina lako mwenyewe na katika capacity yako kept you in check! Asante kwa uungwana wako maana wakati mwingine JF inaweza kumpush mtu hadi akaamua kuomba togwa azimulie.
Nadhani jambo moja ni dhahiri kwamba TPN inahitaji mabadiliko ambayo ni ya lazima ili iende na lengo lake lakini pia ili iweze kuakisi kwa haki matamanio ya wanachama wake wa sasa na wale wa baadaye. Muda uliotumia hapa natumaini umekupa mwanga wa yale ambayo bila ya shaka tayari unayajua au mengine mapya. Nakuomba tu ukiweza print hii kitu na uisambaze kwa uongozi wenu.
Lakini kubwa zaidi ni haja ya nyinyi kukutana hata kama katika extra ordinary meeting (kama imo kwenye Katiba) ili kufanya mabadiliko yanayohitajika ili kuifungua TPN kwa wanachama wengi zaidi na wapya. Endapo hili litaweza/linapangwa kufanyika mapema ni bora zaidi kwa sababu kuna watu ambao bila ya shaka wamekuwa wakisubiri mabadiliko hayo ili na wao waweze kujiunga nanyi.
Asante sana.
Naomba tena niweke quote ya membership kutoka katika katiba:
3.1 MEMBERSHIP.
Membership of the Organization shall be open to:
3.1.1 Individuals who is of sound mind and attained the age of majority who are interested in furthering the work of the Organization and who will be appointed and approved by the Executive Committee and who have paid for the registration fees and annual subscription laid down from time to time by the Executive Committee. Must be Tanzanian Graduates from Higher Learning Institutions within or outside the country with a POSITIVE ATTITUDE, and;
3.1.2 Any corporate or unincorporated association or body which is interested in furthering the Organization's work and that has been approved by the Executive Committee and has paid for the registration fees and annual subscription (any such body is being called in this constitution "member organization").
3.1.3 Honorary Membership given to other individuals, groups or Corporate which supports the Vision, Mission and Objectives of Tanzania Professionals Network.
Kwa ufupi mwanachama anaweza kuwa:
1. Graduate of Higher Learning Institutions
2. Corporate Association or body
3. Uncorporate Association or Body
4. Other Individuals who do not fit in the three above but have interest of joining TPN.
Kwa lugha rahisi na kwa ujumla ni kuwa yeyote anaweza kuwa mwanachama ili mradi awe graduate wa elimu ya juu, au kampuni ambayo inaafiki malengo ya TPN au mtu yeyote hata kama si graduate ambaye anaafiki malengo ya TPN.
Sanctus,Mzalendo Mwanakijiji natambua sana with due respect kuwa JF si mahala pa mchezo, mimi napaita Tanuru na Moto . . . LOL. Madhumuni ya kuja hapa pamoja na kutoa mualiko, nilitaka tupitie katika Tanuru hili ili tuweze kujisafisha na pia kijiboresha kwa kupata michango yenu ya mawazo na mitazamo yote.
Kwa hakika tutakuwa na AGM mwezi wa nane na hili la kuboresha katiba litakuwa ni moja wapo.
Hawa wakulu humu JF wakishamaliza kutoa maoni yao nitayakusanya yote na kudistribute kwa TPN Members ili yafanyiwe kazi pamoja na wao pia kutoa maoni yao. TPN inathamini sana michango yote yenye mwelekeo wa kujenga na kuboresha.
GM asante sana bro. Kuna mambo mengine yanahitaji sacrifice na hata kutake risk. JF si mchezo, ni tanuru, we si unaona hoja za wakulu, unaweza ukaingia mitii hivi hivi.
Wenzangu wa TPN wako na kila mtu akiwa na majukumu yake. Of course wote tunaweza kutofautiana katika utendaji na commitment lakini lengo letu ni moja na nina uhakika kila mtu ana umuhimu wake na mchango wake. Ila ningefurahi sana kama members na viongozi wote wangekuwa active sana. TPN ingekuwa mbali sana.
Hoja hii ni ngumu, ngoja nife nayo tu mimi mwenyewe hata kuniua niueni lakini siachii . . . haaa haaa LOL