Jf Karibuni Tanzania Professionals Network

Sanctus Mtsimbe

JF-Expert Member
Jul 14, 2008
1,820
982
Naitwa Sanctus Mtsimbe na naomba niungane na wana JF wengine waliojitambulisha kwa majina yao halisi na kuomba tuweze kuungana na kufanya mambo ya kimsingi katika kuleta maendeleo ya nchi yetu.

Nimekuwa msomaji mkubwa wa JF toka mwaka 2007 na leo nimeona ni vema nami nijitokeze kuandika machache. Napenda kuishukuru na kuipongeza JF na uongozi na wanachama wake kwa kazi kubwa na nzuri manayoifanya katika kuleta changamoto mbalimbali.

Napenda kutoa mualiko rasmi kwa kuwakaribisha wana JF wenye mtazamo na mwelekeo wa kupenda maendeleo ya kweli kujiunga katika Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (Tanzania Professionals Network, TPN). TPN ni mtandao unaowaunganiasha wanataaluma wa fani mbalimbali bila kujali nafasi au vyeo vyao ikiwa na madhumuni ya kuwezeshana Wanataaluma na Wananchi kwa ujumla kiuchumi na kifedha.

Kwa kuwa michango mingi ya Wana-JF ni kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa Watanzania na Nchi kwa ujumla (Kitu ambacho TPN pia inafanya), karibuni sana tuweze kuungana na kuonana katika mikutano ya mara kwa mara ambayo ina lengo la kuboresha maisha yetu.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea tovuti ya www.tpn.co.tz (Bado tovuti inaboreshwa . . . ). Tunakaribisha pia maoni yenu yenye mwelekeo wa kujenga na kuimarisha TPN.

Na kama kuna ufafanuzi wowote unahitajika, tafadhali tuwasiliane kupitia barua pepe president@tpn.co.tz au +255-754-833-985.
 
Sanctus Mtsimbe.

Sikubaliani na wewe hata kidogo juu ya watu kutumia majina yao katika JF. Anonymity ni swala linalosaidia sana katika kufichaua maasi. Wana JF kaza buti. Huko TPN hata mimi siendi mpaka nione matunda. Siwezi kumezwa na CCM part two huku najiona ebooooooooooo. Fanyeni mambo ya maana watu watajileta wenyewe siyo kujirembea majina MSc, BSc na ushambenge mwiiiiingi!

Naitwa Sanctus Mtsimbe na naomba niungane na wana JF wengine waliojitambulisha kwa majina yao halisi na kutoa mwito wengine wafanye hivyo ili tuweze kuungana na kufanya mambo ya kimmsingi sasa yanayohitaji kufahamiana na kukutana.

Nimekuwa msomaji mkubwa wa JF toka mwaka 2007 na leo nimeona ni vema nami nijitokeze kuandika machache. Napenda kuishukuru na kuipongeza JF na uongozi na wanachama wake kwa kazi kubwa na nzuri manayoifanya katika kuleta changamoto mbalimbali.

Napenda kutoa mualiko rasmi kwa kuwakaribisha wana JF wenye mtazamo na mwelekeo wa kupenda maendeleo ya kweli kujiunga katika Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (Tanzania Professionals Network, TPN). TPN ni mtandao unaowaunganiasha wanataaluma wa fani mbalimbali bila kujali nafasi au vyeo vyao ikiwa na madhumuni ya kuwezeshana Wanataaluma na Wananchi kwa ujumla kiuchumi na kifedha.

Kwa kuwa michango mingi ya Wana-JF ni kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa Watanzania na Nchi kwa ujumla (Kitu ambacho TPN pia inafanya), karibuni sana tuweze kuungana na kuonana katika mikutano ya mara kwa mara ambayo ina lengo la kuboresha maisha yetu.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea tovuti ya www.tpn.co.tz (Bado tovuti inaboreshwa . . . )

Na kama kuna ufafanuzi wowote unahitajika, tafadhali tuwasiliane kupitia barua pepe president@tpn.co.tz au +255-754-833-985.
 
Ndugu yangu Matejoo, unayo haki ya kuongea lolote na nadhani hiyo ni haki ya kimsingi kabisa. Kutumia jina lako halisi si lazima. Nilichosema inapofika wakati kuna mambo muhimu ambayo pengine mtahitaji kuonana na kubadilishana mawazo sidhani kama ni wazo baya kutumia majina halisi.

TPN ni mtandao mpya ambao sasa hivi unamaliza mwaka mmoja. Ni kweli kuna changamoto ya wengi kutaka kuona matunda. Na napenda kukuhakikishia kuwa matunda yanaanza kuonekana. Hakuna mwanzo mwepesi na mafanikio wakati mwingine huja kwa juhudi kubwa.

Napenda kukuhakikishia kuwa TPN haina uhusiano wowote na chama chochote cha kisisa, ndo maana kama umewahi kuhudhuria vikao utakuta kuna viongozi pia kutoka kada mbalimbali nikiwa na maana chama tawala, upinzani na hata wasio na vyama. Binafsi mimi si mwanachama wa chama chochote.

Mwisho kama kuna tatizo lolote katika kutumia qualification katika mawasiliano yenye kusudi fulani basi tusaidiane na kuelemishana na nadhani likieleweka halina tatizo. La Ushambenge Mwingi pia unaweza ukafafanua na likatolewa maelezo.
 
Sanctus Mtsimbe.

Sikubaliani na wewe hata kidogo juu ya watu kutumia majina yao katika JF. Anonymity ni swala linalosaidia sana katika kufichaua maasi. Wana JF kaza buti. Huko TPN hata mimi siendi mpaka nione matunda. Siwezi kumezwa na CCM part two huku najiona ebooooooooooo. Fanyeni mambo ya maana watu watajileta wenyewe siyo kujirembea majina MSc, BSc na ushambenge mwiiiiingi!

Mambo ya chama na utaalamu wapi na wapi?. Ndugu Sanctus amekaribisha wana JF katika mtandao huo wa wataalamu ambao wanachangia mada tofauti kwa lengo la kuendeleza Tanzania kwa kutumia utaalamu wao na wala hajagusia chama chochote cha siasa. Sioni ubaya kwa hilo hata kidogo kwani tunahitaji kuunganisha nguvu ili kubadilisha hali katika Tanzania yetu.
 
Zimwi likujualo halikuli likakwisha, lakini kwa JF CCM wakijua jina lako halisi umejiingiza kifungoni kimawazo. We unafikiri wakijua kuwa wewe ni Ofisa IKULU na upo JF si ndio watajua kuwa mvujisha siri. Hivi hivi anonimity ndio watajirekebisha maana humjui nani adui yako na hivyo itakufanya uwe katika mstari ulionyooka kila wakati. Mnaojitambulisha ni vizuri kwani role yenu humu ni kusoma Ila wapo wenye role ya kijasusi humu. Yaani wafukua habari ili kuisaidia nchi hawa waendelee kuwa ANONIMOUS
 
Hofstede nakubaliana na wewe. Ni kweli kama kuna mtu ana mambo nyeti au anataka kutoa mchango wa ku-Criticise hatapenda hajulikane, na nadhani hilo ni la msingi sana ili kuhakikisha mhusika anatoa mchango wake bila kuwa na wasiwasi.

Pengine mimi nimeona nijitambulishe kwa ajili ya role yangu katika kutoa taaarifa hizi. Wengi wengependa kujua kwa uhakika anayeleta habari hizi ni nani na kwa nini. Na kwa hili nitakuwa muwazi katika kujibu au kuelezea critics zozote na mambo mengine kama alivyoanza ndugu yangu Matejoo hapo juu kwa maandishi makubwa sana.

Hata hivyo sidhani kama tukionana katika Networking Meeting utatumia jina lako hilo. Na hata ukijitambulisha katika hiyo meeting kwa jina lako sitaweza kujua kama wewe Hostede katika JF.
 
Watanzania ni lazima tujifunze tabia ya "kupeana shavu". Tusiangalie tu jinsi sisi tutakavyonufaishwa na jumuiya bali pia tuangalie jinsi sisi tunavyozinufaisha jumuiya hizo.
Mtsimbe karibu sana JF. Asante kwa kuamua kuandika "live kwa jina lako".
"Nitatoa shavu" kwa TPN kila nitakapoweza na later this year nitachukua uanachama.Take my word Mtsimbe and other TPN crew.
 
Sijaona ubaya wa rais wa TPN kualika watu kujiunga na TPN, kwanini baadhi yetu tuna mawazo hasi kwa kila jambo linalotolewa bila hata kufikiri? Hivi ni lini watz tutajifunza kuwa negative thoughts kills, and will never take you anywhere! Huu ni wito wa hiari kabisa kama unaona kuna jambo halifai kuna njia za kistaarabu za kuuliza na wa kumuuliza amejitokeza na sio kumattach kila mtu, "After all not everything is for everybody", kama huu si uwanja wako kuna pengine pa kukufaa. Mambo mengine yanadhihirisha wazi upeo tulionao katika maisha, kumbuka " Being positive or negative are habits of thoughts,that have a strong influence in life"
 
Mzalendo mwenzangu Zemarcopolo nashukuru sana kwa kututia moyo.

Kitu ambacho ni ningependa kuweka wazi ni kuwa TPN haiko pale kwa manufaa ya watu wachache au kikundi fulani cha watu. Kwa wale walio wanachama wanaweza wakahakikisha hili. Tumeona kutoka ndani ya TPN watu wakianzisha makampuni, Wengine wakipata kazi, wengine wakipata mikopo maalumu nk.

Najua Wanataaluma wengi wamekata tamaa kwa jinsi mambo yanavyokwenda kimaendeleo. Nia yetu wote ni kuangalia ni namna gani Wanataaluma tunaweza kuungana na kutumia fursa zilizopo kujiletea maendeleo makubwa bila kujitumbukiza katika siasa kama TPN na hatimaye kuleta maendeleo ya nchi.

Nadhani hapa JF kuna mkulu moja anaitwa Mwanakijiji ambaye aliwahi kuandika makala nzuri sana katika gazeti iliyokuwa na changamoto pia kwa TPN na nilifurahi na kunufaika baadaye nilpowasiliana naye na kupata mawazo yake. Hakuna ambaye anaweza mwenyewe, ni kwa kupitia jitihada za pamoja tukiwa na lengo moja tunaweza kuleta mafanikio ya kweli.

Asante sana Zemarcopolo and am taking your words
 
Asante sana Tonga. Hakika kama ulivyosema "Mambo mengine yanadhihirisha wazi upeo tulionao katika maisha, kumbuka " Being positive or negative are habits of thoughts,that have a strong influence in life". Ulichosema hakiitaji ufafanuzi. Thanks.

Ndugu yangu Tgeofrey uliyeandika "Usijusumbue Muheshimiwa Nilishakufuza Kwa Michuzi Akili Yako Inazidi Kutokuwa Na Akili Hembu Muone Dr Frank Mmc Pschiatric Atakusaidia Hata Mimi Alinisaidia"

Kama kwa kumbukumbu yangu nitakuwa sawa huenda wewe ni Tumaini au Odinga Radical. Nadhani ndugu yangu ukitumia lugha ya kistaarabu nitakuelewa pia. Si nazima umtukane mtu. Hata hivyo kama ulishamwona Pysichiatric na akakusaidia kama ulivyosema, basi tunamshukuru Mwanataaluma huyo Daktari. TPN kuna wanachama ambao ni madaktari pia.

Niliwaeleza kuwa Blog ya michuzi kwa TPN si ya majibizano ni kwa taarifa tu. Nikawaalika kama mna critics zozote mnipigie simu mimi au viongozi wa TPN au hata kuandika ili tuwafafanulie hamkufanya hivyo. Hoja yenu ni kuwa hamkupenda msimamo wa TPN kuwa "Sullivan Summit haikuleta Impact kama ilivyokusudiwa na kutangazwa". Tukatoa mwito kuwa wana TPN, wanataaluma na wadau wengine tukutane ili kupata feedback ya mikutano ya China-Africa Business Meeting na Sullivan Summit kutoka kwa watu waliohudhuria mikutano hiyo na hatimaye tuangalie uwekano wa ku-explore idea ya kufanya Summit ya Tanzanians in Diaspora hapa Tanzania mwakani. Nadhani nyie wawili hamkuafiki wazo hilo na hivyo kama kawaida yenu mkaanza kashfa na matusi vitu ambavyo hakika havisaidii. Niliwahi kuona Thread ya Sullivan Summit hapa JF na wachangiaji wengi hawaoni kama Sullivan Summit ilileta impact kama ilivyotangazwa.

Ukweli nikuwa katika mkutano wa TPN wengi walikutana na wakapewa feedback ya mikutano hiyo na contacts za kibiashara. Na pia wazo la kuwa na Diaspora Summit lilijadiliwa na kuafikiwa. Tulionana pia na Ministry of Foreign Affairs kwa ajili ya ushauri na wazo hilo pia lilionekana ni zuri na tukapeana majukumu.

Sasa brother shida iko wapi? Hebu sasa tuongee hapa jamvini mwite na jamaa yako hoja zenu zote mzilete hapa na wadau wazipime. Ila matusi si uungwana.
 
Zimwi likujualo halikuli likakwisha, lakini kwa JF CCM wakijua jina lako halisi umejiingiza kifungoni kimawazo. We unafikiri wakijua kuwa wewe ni Ofisa IKULU na upo JF si ndio watajua kuwa mvujisha siri. Hivi hivi anonimity ndio watajirekebisha maana humjui nani adui yako na hivyo itakufanya uwe katika mstari ulionyooka kila wakati. Mnaojitambulisha ni vizuri kwani role yenu humu ni kusoma Ila wapo wenye role ya kijasusi humu. Yaani wafukua habari ili kuisaidia nchi hawa waendelee kuwa ANONIMOUS

Ahsante sana umeandika vizuri kabisa na huo ndiyo ukweli wa mambo.
 
Bubu Ataka Kusema . . . . LOL. Nimependa sana usemi wako wa "I will die poor rather than stealing from Tanzanians through fake contracts and dubious ownership of Tanzanians' Natural Resources"

Natamani kama ingewezekana maneno hayo ya busara ndiyo yangekuwa sheria ya moyoni ya viongozi wote katika utumishi wa umma na hata maakampuni binafsi.
 
Thanks ndugu Mtsimbe, I have an idea ni kwa nini wanaJF tusiingie humo kwenye tovuti ya TPN tusome na kuelewa halafu ndio tuanze kuijadili hiyo network. I guess kutakuwa na mengi comments,criticism (constructive or otherwise), mashaka, new ideas, malengo etc.

Na hata hiyo hoja aliyoitoa mchangiaji kuhusisha network hii na CCM inaweza kujadiliwa pia kwa mapana zaidi (Mtsimbe usiirahisishe let the pple brainstorm). Because if this is the case I doubt kama kutakuwa na commitment.
 
Ndugu yangu Nyambala, nakubaliana na wewe kwa asilimia 100%. Tungependa sana TPN ijengwe katika misingi imara kwa kutumia approach uliyoisema.

Maana halisi ya mimi kuwa muwazi na kutoa jina langu halisi ni kuwa tayari kupokea mawazo ya namna yote ya kujenga na hata ya kubomoa (+ve and -ve). Naamini kuwa yote yatasaidia kujiimarisha.

Binafsi ningependa kuona TPN iwe taasisi inayowaunganisha Wanataaluma wote kwa vitendo ili nasi tupate mahali pa kutoa mchango wetu kwa vitendo. Ningependa kuona pia mawazo mapya na wote wenye vipaji vya uongozi wanaingia ndani ya TPN na kuboresha zaidi. Kama nilivyosema TPN si ya wachache wala wale walio katika uongozi hawana nia ya kuhodhi madaraka. Tungpenda tujenge Mfumo ambao utadumu hata vizazi vijaavyo.

Kwa hiyo kaaribuni sana kutembelea tovuti na haata kama kuna information zaidi zinahitajika unaweza kunijulisha mimi au wengine katika TPN. Kuna walioniandikia jana kuomba information zaidi na niliwatumia.

Kwa hiyo karibuni na tusioneane haya. Hoja ijibiwe kwa hoja. Naamini palipo na hoja au ukweli, basi ukweli utajulikana au utabikia haijalishi kama ukweli au hoja hiyo itatoka kwa yeyote mwenye mwelekeo chanya au hasi.
 
Sanctus,

Shukrani kwa kuitumia JF kufikisha ujumbe. Kwangu hii inamaanisha unatambua kuwa JF inaweza kutumiwa pia kwa shughuli hiyohiyo ya kuwaunganisha wataalam wetu (nadhani nikiwemo mimi) kwakuwa JF si siasa tu pia tunaweza kuitumia kwa malengo tofauti tofauti.

Aidha, nakushukuru kwa ujasiri wa kufikisha hoja kwa hekima kubwa!
 
MTZ Mwenzetu umeeleweka,huo ni mwaliko ambao kila mtu ana hiari yake kwa utashi wake kuamua.
Kama hupendi, basi achana nao kuliko kutoa lugha isiyochujwa.Binafsi niliwahi kuwaona wakijieleza TBC1 Kipindi cha asubuhi cha Jambo Afica huyo MSIMBE na akina dada wawili,mmoja kiswahili kilikuwa kinampa shida kweli,anapendelea ngeli
 
Nitakuja... Ngoja nione huko TPN kuna nini... Ila suala la kutumia majina halisi Mtsimbe sijajua una lengo gani haswa? Unawatakia Wapambanaji mema ama?

Kutumia hizi Alias doesn't mean watu ni waoga, hapana. Ni katika kuhakikisha yale ambayo tunashindwa kufanya tukilinda maslahi yetu na wale tegemezi kwetu yanakuwa wazi!!! Hata kama tunapambana na Wadhalimu kama Wazalendo, we gotta take care of our own! JF mwendo ule ule...

Nikitoka TPN ntawa na mengi!!!
 
Mtsimbe uko sawa rai yako ni endelevu na naiunga mkono.
Jamani kujumuika ni mwanzo, kuendelea kukaa pamoja ni hatua na kufanya kazi pamoja kama WANA TPN ni mafanikio.
Wamataaluma tumeanza kujumuika na sasa tuendelee kukaa pamoja ili tufanye kazi na hatimaye tufanikiwe.
BIG UP TPN founders, good idea.

Ndugu yangu Matejoo, unayo haki ya kuongea lolote na nadhani hiyo ni haki ya kimsingi kabisa. Kutumia jina lako halisi si lazima. Nilichosema inapofika wakati kuna mambo muhimu ambayo pengine mtahitaji kuonana na kubadilishana mawazo sidhani kama ni wazo baya kutumia majina halisi.

TPN ni mtandao mpya ambao sasa hivi unamaliza mwaka mmoja. Ni kweli kuna changamoto ya wengi kutaka kuona matunda. Na napenda kukuhakikishia kuwa matunda yanaanza kuonekana. Hakuna mwanzo mwepesi na mafanikio wakati mwingine huja kwa juhudi kubwa.

Napenda kukuhakikishia kuwa TPN haina uhusiano wowote na chama chochote cha kisisa, ndo maana kama umewahi kuhudhuria vikao utakuta kuna viongozi pia kutoka kada mbalimbali nikiwa na maana chama tawala, upinzani na hata wasio na vyama. Binafsi mimi si mwanachama wa chama chochote.

Mwisho kama kuna tatizo lolote katika kutumia qualification katika mawasiliano yenye kusudi fulani basi tusaidiane na kuelemishana na nadhani likieleweka halina tatizo. La Ushambenge Mwingi pia unaweza ukafafanua na likatolewa maelezo.
 
Membership is open to Tanzanian Graduates from a higher Institution of learning. There also is membership for corporate organisations and honorary membership.

Kabla sijaendelea mbele Mtsimbe ningependa unifafanulie hiyo sentensi hapo. Maana ulipowakaribisha wana JF hukusema hivo. Hivi unadhani ya kwamba Wana JF wote ni Graduates? Ama tutafall under Honorary maana hata kwa corporate hatuingii.

Nangoja ufafanuzi!
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom