Sanctus Mtsimbe
R I P
- Jul 14, 2008
- 1,820
- 1,031
Naitwa Sanctus Mtsimbe na naomba niungane na wana JF wengine waliojitambulisha kwa majina yao halisi na kutoa mwito wengine wafanye hivyo ili tuweze kuungana na kufanya mambo ya kimmsingi sasa yanayohitaji kufahamiana na kukutana.
Nimekuwa msomaji mkubwa wa JF toka mwaka 2007 na leo nimeona ni vema nami nijitokeze kuandika machache. Napenda kuishukuru na kuipongeza JF na uongozi na wanachama wake kwa kazi kubwa na nzuri manayoifanya katika kuleta changamoto mbalimbali.
Napenda kutoa mualiko rasmi kwa kuwakaribisha wana JF wenye mtazamo na mwelekeo wa kupenda maendeleo ya kweli kujiunga katika Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (Tanzania Professionals Network, TPN). TPN ni mtandao unaowaunganiasha wanataaluma wa fani mbalimbali bila kujali nafasi au vyeo vyao ikiwa na madhumuni ya kuwezeshana Wanataaluma na Wananchi kwa ujumla kiuchumi na kifedha.
Kwa kuwa michango mingi ya Wana-JF ni kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa Watanzania na Nchi kwa ujumla (Kitu ambacho TPN pia inafanya), karibuni sana tuweze kuungana na kuonana katika mikutano ya mara kwa mara ambayo ina lengo la kuboresha maisha yetu.
Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea tovuti ya www.tpn.co.tz (Bado tovuti inaboreshwa . . . )
Na kama kuna ufafanuzi wowote unahitajika, tafadhali tuwasiliane kupitia barua pepe president@tpn.co.tz au +255-754-833-985.
Sanctus Mtsimbe.
Sikubaliani na wewe hata kidogo juu ya watu kutumia majina yao katika JF. Anonymity ni swala linalosaidia sana katika kufichaua maasi. Wana JF kaza buti. Huko TPN hata mimi siendi mpaka nione matunda. Siwezi kumezwa na CCM part two huku najiona ebooooooooooo. Fanyeni mambo ya maana watu watajileta wenyewe siyo kujirembea majina MSc, BSc na ushambenge mwiiiiingi!
Zimwi likujualo halikuli likakwisha, lakini kwa JF CCM wakijua jina lako halisi umejiingiza kifungoni kimawazo. We unafikiri wakijua kuwa wewe ni Ofisa IKULU na upo JF si ndio watajua kuwa mvujisha siri. Hivi hivi anonimity ndio watajirekebisha maana humjui nani adui yako na hivyo itakufanya uwe katika mstari ulionyooka kila wakati. Mnaojitambulisha ni vizuri kwani role yenu humu ni kusoma Ila wapo wenye role ya kijasusi humu. Yaani wafukua habari ili kuisaidia nchi hawa waendelee kuwa ANONIMOUS
Sanctus,Ndugu yangu Nyambala, nakubaliana na wewe kwa asilimia 100%. Tungependa sana TPN ijengwe katika misingi imara kwa kutumia approach uliyoisema.
Maana halisi ya mimi kuwa muwazi na kutoa jina langu halisi ni kuwa tayari kupokea mawazo ya namna yote ya kujenga na hata ya kubomoa (+ve and -ve). Naamini kuwa yote yatasaidia kujiimarisha.
Binafsi ningependa kuona TPN iwe taasisi inayowaunganisha Wanataaluma wote kwa vitendo ili nasi tupate mahali pa kutoa mchango wetu kwa vitendo. Ningependa kuona pia mawazo mapya na wote wenye vipaji vya uongozi wanaingia ndani ya TPN na kuboresha zaidi. Kama nilivyosema TPN si ya wachache wala wale walio katika uongozi hawana nia ya kuhodhi madaraka. Tungpenda tujenge Mfumo ambao utadumu hata vizazi vijaavyo.
Kwa hiyo kaaribuni sana kutembelea tovuti na haata kama kuna information zaidi zinahitajika unaweza kunijulisha mimi au wengine katika TPN. Kuna walioniandikia jana kuomba information zaidi na niliwatumia.
Kwa hiyo karibuni na tusioneane haya. Hoja ijibiwe kwa hoja. Naamini palipo na hoja au ukweli, basi ukweli utajulikana au utabikia haijalishi kama ukweli au hoja hiyo itatoka kwa yeyote mwenye mwelekeo chanya au hasi.
Ohooo! Makubwa haya.......mmoja kiswahili kilikuwa kinampa shida kweli,anapendelea ngeli
Ndugu yangu Matejoo, unayo haki ya kuongea lolote na nadhani hiyo ni haki ya kimsingi kabisa. Kutumia jina lako halisi si lazima. Nilichosema inapofika wakati kuna mambo muhimu ambayo pengine mtahitaji kuonana na kubadilishana mawazo sidhani kama ni wazo baya kutumia majina halisi.
TPN ni mtandao mpya ambao sasa hivi unamaliza mwaka mmoja. Ni kweli kuna changamoto ya wengi kutaka kuona matunda. Na napenda kukuhakikishia kuwa matunda yanaanza kuonekana. Hakuna mwanzo mwepesi na mafanikio wakati mwingine huja kwa juhudi kubwa.
Napenda kukuhakikishia kuwa TPN haina uhusiano wowote na chama chochote cha kisisa, ndo maana kama umewahi kuhudhuria vikao utakuta kuna viongozi pia kutoka kada mbalimbali nikiwa na maana chama tawala, upinzani na hata wasio na vyama. Binafsi mimi si mwanachama wa chama chochote.
Mwisho kama kuna tatizo lolote katika kutumia qualification katika mawasiliano yenye kusudi fulani basi tusaidiane na kuelemishana na nadhani likieleweka halina tatizo. La Ushambenge Mwingi pia unaweza ukafafanua na likatolewa maelezo.
Membership is open to Tanzanian Graduates from a higher Institution of learning. There also is membership for corporate organisations and honorary membership.