JF imenifanya niporwe simu!

Hata kama uko una gari yako ndo ushuke ili ukimbize mwizi wa simu ya laki, heeee,
Na ukirudi ukakuta hata gari haipo itakuwaje.

Pole mwaya.
 
Mi jumamosi ilopita yamenikuta mbona.

Tena nlikua napost kitu JF, milango ya saa 2 usiku.

Nipo kwenye taxi nyuma, na kioo nimeshusha. Yani akili yote imehama imehamia dunia ya JF.

Mitaa ya Jang'ombe zenji, dereva ka slow down kwa sababu ya mkanganyano wa magari. Nashtukiza kwapuuuu.

Nlivovinjari mtt wa kike, tulivutiana simu na kibaka mpk simu ilitoa mlio wa kudata.

Gemu lilienda kimya kimya, mana nguvu zote nlizihamishia mikononi basi hata kuongea sikuweza.

Nashkuru nlishinda, mana by the time dereva anakaza mwendo kibaka katoka mbio.

Ndani ya gari tulikua watu wa4 hamna alojua mpk nliporudisha pumzi na kuwahadithia.

Yani ilikua kama kituko flan ivi.
 
...simu, nami sikujivunga! nilifungua mlango na kumkimbiza huku nikipiga kelele za mwiziii! mwiziii! mwiziii! nilimkimbiza peke yangu bila kupata kampani yoyote. Na muda huo huo gari zikawa zimeruhusiwa nikajikuta nimeweka foleni nyingine huku....

ungepiga kelele kuwa wewe ni member wa jf na ulikuwa unawahi lumumba ungepata msaada fasta.
hata hivyo ugua pole ndugu
 
Hahahahahah jinsi ulivyopost tu ...
 
humu ndo kilichonchekesha mkuu...!
 
Ujue ulikua unaenda Machi Machi Guest House......hahahaaaaa pole Mpwa I can feel the pain

Na pale 'imported good' ilikuwa inasubiri maelekezo ya simu, on the top ndipo inachukuliwa, lazima umlaani kibaka.
 

Bila shaka huyo watakua washamla sana kwa gear hizo za first impression!...
 
Bora ungekua unamkimbiza huku unaita jf jf jffff labda wangetokea wadau wahumu kando kando ya hapo kukupa tafu au saa ingine huyo mwizi ni mdau wa hili jamvi angesitisha mbio na kukurudishia simu umalizie kusoma.

Ila pole sana ndugu.
 
Pole sana mdau.
Sijui tupitishe kampeni tukuchangie jamani. Nahofia kukumiss hapa
Hahahaha! ahsante sana King'asti, hata hivyo hutanimis coz nitakuwa natumia simu ya wifi yako, asubuh au jioni baada kutoka kazini!
 
Last edited by a moderator:
Simu ndio ishaporwa hapo kabla sredi hajaimalizia heheh...strange uunh!!!

Hapana watu8, hii ni simu ya mai waifu ina herufi chache sana, hata hivyo nawashukuru mods kwa kuiunganisha na kuwa na mtiririko mzuri.
 
Last edited by a moderator:
Kuna uzi ukiusoma hata kibaka hatumii nguvu kukupora
 
Na hii unayotumia lazima iondoke..

Hahahahahah, hii ni ya mai waif labda anipore yeye kwani ninapokuwa jamvini huwa nakata mawasiliano nae kabisa hata anapoongea huisi nimemdharau! Nahis atanipora muda wowote!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…