JF imekunufaisha vipi mwaka huu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JF imekunufaisha vipi mwaka huu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jaluo_Nyeupe, Dec 27, 2010.

 1. Jaluo_Nyeupe

  Jaluo_Nyeupe JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2010
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 2,269
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Habari wana JF,

  Tukiwa tunaelekea mwishoni mwa mwaka nimeona sio vibaya tukifanya tathmini kuhusu majukwaa mbalimbali ya JF yalivyokunufaisha au kukutia hasara.

  Kabla sijajiunga na hata baada ya kujiunga na JF nimenufaika kwa mambo mengi, hasa wakati wa kampeni nilikuwa nikipata habari mpya na za kila sehemu kabla hata hazijatoka kwenye magazeti. Kwenye majukwaa mengine nimenufaika kwa kupata software, kununua kununua vitu mbali mbali, kuwawezesha ndugu zangu kupata kazi, kupunguza stress za kimaisha kwenye jokes na kujua mambo mbali mbali yahusuyo afya. Pia kwenye jukwaa la MMU nimeweza kupata ushauri mbali mbali kwa mambo yahusuyo maisha ya kimapenzi na soon nategemea kunufaika zaidi kama nitapata mchumba JF.

  Hasara nilizopata ni chache kama kuchelewa kulala na kupunguza muda wa kufanya kazi, pia kimodem changu kilikuwa kinani-cost sana nikiwa nje ya ofisi.

  Je wewe umenufaika au kupata hasara gani kwa ajili ya JF?

  Kama umenufaika usisahau kuichangia JF mwaka ujao kama Mungu akitujaalia.
   
Loading...