Mkuu Salute. At least I can now appreciate what JK meant when he said the country has no competent poeple in contract laws. It seems that you are very conversant with these issues. I, among many here, are ignorant of all the references you have made here, which, they make a lot of sense. What i want to know from you learned brother is that in such a situation, what is the way out for Tanesco and tanzania as a country in this case?
dawa ni ubabe,kisheria hatuwezi,kama mkuu wetu wa nchi yupo tayari tuitaifishe kibabe na kuvunja mahusiano na hiyo mahakama full stop!
@MTAZAMO, nakubalina na wewe kabisa.Tukienda kwa mtindo wa kufuata sheria tutadumbukia kuzimu. Hapa solution ni kufanya 'street law' kwamba hatulipi hata cent moja, na kama ni kutaifaisha mali za TANESCO zilizoko Uingereza na sisi tufanye hivyo hivyo hapa - jino kwa jino, liwalo na liwe. Inabidi tujilipue na kuwa maskini jeuri vingenevyo tutakamuliwa damu!
IKO kisheria sana tungepata Mtaalam wa Lugha za kisheria atutafunie sisi wabeba zege maana shule zenyewe tumesoma St CCM, Chuo tumefundishwa na waadhiri walofail, wale wazuri wooote wako kwenye Siasa...
Coach Parcells, kwa kifupi,
1. Baada ya ICC kuitioza Tanesco walipe zile US$65m plus interest ambazo zinaitwa tozo za Dowans.
2. Tozo hiyo inapaswa isajiliwe na Mahakama Kuu hapa nchini ili iweze kuwa enforceble by lacal laws, yaani Tanesco wawajibike/kulazimishwa kulipa.
3. Kabla mahakama kuu haijatoa uamuzi wa kuisajili tozo hiyo, tayari kuna kesi nyingine 4 zimefunguliwa mahakama kuu kupinga kulipwa kwa tozo hiyo.
4. Hivyo uamuzi wa mahakama kuu kuisajili tozo hiyo unaweza kuchelewa mpaka Desemba 2011 au zaidi ili kuzosikiliza pingamizi hizo.
5. Ili mshitaki Dowans asizidi kupoteza haki zake, ameipandisha Tanesco kwenye mahakama ya Uingereza, akiomba mahakama hiyo kutoa uamuzi wa kukazia hukumu ya ICC, kwa kuiomba itoe kibali cha kuzishika mali za Tanesco zilizoko Uingereza au Jumuiya ya Ulaya ili mali hizo zitumike kama dhamana/security ya kuishinikiza Tanesco kulipo tozo husika.
6. Hiyo mahakama hiyo ya Uingereza imeitaka Tanesco kulipa Dola Milioni 5 zitumike kama security kusubiri uamuzi wa Mahakama kuu ya Tanzania kuisajili tozo ya Dowans.
7. Mahakama hiyo imeridia msimao wa mkataba ule ambao kwa ridhaa yao wenyewe waliamua uamuzi wa ICC ndio wa mwisho na haukutakiwa kupingwa wala kucheleweshwa.
My Take.
Wana bodi wenzangu, hii ni issue ya kisheria na sio kisiasa, nawashauri tupunguze kidogo politics kwenye masuala ya kisheria. Niliwahi kusisitiza, ule mkataba ni mkataba bomu, Tanesco walijifunga na hawana pa kutokea dawa ni kulipa tuu!.
Ila pia naungana na hoja za Tanesco kuwa wao hawalipi kwa vile aliyewaingiza kwenye mtego huo ni serikali, hivyo ni jukumu la serikali kulipa na sio Tanesco.
Nyerere angekuwa ni rais wa nchi hii, tungevunja uhusiano na ICC, tusingelipa chochote!, mitambo tungetaifisha!, hao wawekezaji wa ulaya wangefungasha virago vyao na kwenda makwao wakatengeneze dhahabu na gesi zao huko viwandani kwao. Wachina wangetuletea teknolojia ya kuichimba dhahabu yetu, gesi yetu na mafuta yetu huku faida asilimia 100%, ikibaki ni mali yetu, kuliko sasa wanavyochimba hawa maharamia kwa jina la waweklezaji, wakikomba asilimia 98% huku wakituachia asilimia 2% eti ndio royality!.
Lakini kwa vile siye yeye, waliopo wanaheshimu utawala wa sheria, wawekezaji ndio tunawanyenyekea na kuwalamba miguu, amini nawaambieni, Tozo tutalipa, tena sio Tanesco, bali serikali kwa kodi zetu!.
Wakuu huwezi kufanya ubabe kwenye hili suala. This is an international issue. Tanzania tume sign mikataba ya kimataifa na kukubali kuwa tutaheshimu hukumu ambazo zimepitishwa na mahakama za nje. Kama hatutaki then tujiondoe kwenye hiyo mikataba kwanza. Na ukisema uende kibabe, Tanzania is ina assets abroad? Thats is exactly what Dowans wants to do. Kwa vile tayari tumeshaleta ubabe nyumbani, Dowans wants to execute our assets abroad. Kama tunao ubabe basi tuhamishe assets zote na kuzirudisha nyumbani.
FJM kumbuka atakayetaifisha mali zetu ni Dowans na wala sio serikali ya Uingereza. Serikali ya Uingereza haihusiki hapa. After all sisi ndio tulichemsha wenyewe tuliposaini mkataba. Kwa nini leo tusilipe?
Mkuu Pasco: Napingana na wewe kwa nguvu zote kuhusu hapo nilipo-highlight na red. Serikali hii katu haina utawala wa sheria na mifano ambayo ipo ni mingi sana, nawe unafahamu fika. Hili suala la Dowans kwa kuwa linahusu ulipwaji wa pesa na kuna watu fulani humu nchini ni beneficiary, basi ndiyo kunaletwa hii ya kusema kwa kuwa utawala huu unafuata sheria, basi ni sharti tozo hiyo ikalipwa.
Kwa mambo mengine hatusikii kuletwa hiki kitu "utawala wa sheria". Serikali hii imekuwa ikikaidi hukumu za mahakama zake zenyewe hapa nchini zilizowekwa kikatiba na wala haijali, na wala akina Pasco hatujawasikia wakisema. Mfano ni kesi ya Valambia. Lakini kwa hukumu za mahakama za nje hata kama ni za binafsi kama vile hiyo ICC (isichanganywe hapa na ile ICC ya The Hague) basi serikali inakuwa na uchu mkubwa sana wa kulipa, na kuandaa wapambe chungu nzima kuipigia debe kwamba lazima utawala wa sheria ufuatwe.
Suala la pili ni serikali kutowachukulia hatua wale waliotufikisha hapo kwani wanajulikana -- akina Karamagi & co. Dola 65m ni nyingi sana kwa serikali kuingizwa mkenge na watu wachache. Jee, Pasco, kwa nini usiipigie debe suala hili kwamba serikali hii yenye kufuata 'utawala wa sheria' ni lazima iwafikishe mahakamani wachache hawa kwa kuliingzia taifa hasara?
Nawasilisha.
kubwa hapa ni kuwa mahakama ya uk haijasema tulipe ila inataka tuweke rehani dola milioni 5 na uamuzi wao una utata na waweza kutenguliwa na UK court of appeal au House of the Lords..........................................so it is not yet over until it is truly over.........
Not necessarily, especially given the kind of legal language aka legalese applied here. The statements provided appear to be open to interpretation. That being said, you'll need to clarify as to the particular context(s) these statements allude to (according to you), and your own understanding of their legal meanings and/or consequences.
FJM kumbuka atakayetaifisha mali zetu ni Dowans na wala sio serikali ya Uingereza. Serikali ya Uingereza haihusiki hapa. After all sisi ndio tulichemsha wenyewe tuliposaini mkataba. Kwa nini leo tusilipe?
.
Mkuu EMT, kwenye red; Hivi nani anamiliki Dowans? Ni Al-Adawi? au Symbion? Kama sikosei mwaka huu huu kuliwahi tolea amri na mahakama yetu kuwa Dowans wafanye maamuzi i.e kuuza mitambo (correct me if I am wrong) bila idhini ya mahakama. Hii ina nguvu yoyote?
Kwa ujumla Richmond/Dowans ni jinamizi ambalo kwangu naamini litapeleka CCM kaburini. Can you imagine sasa hivi baada ya wauza mafuta kuishikisha adabu serikali iseme italipa Dowans? Tayari Richmond ilisababisha Baraza la mawaziri kuvunjwa, sasa Dowans itasambaratisha chama. Na huyo aliachana na siasa uchwara ili kushughulikia biashara nadhani aliasahau/aliamua makusudi kutosema kuwa biashara yake kwa sasa ni 'kupanga' mijeledi tayari kwa minyukano ndani ya ccm. Watachapana kuliko.
Ushauri kwa ccm maana hakuna lisilowekezana kwa hawa wakubwa, wapitishe sheria kwa sasa inayosema kuwa mwanasheria yoyote mtanzania akishiriki kwenye kuandaa mikabata 'inayohujumu' uchumi wa nchi basi atakuwa anatenda kosa. Hii inaweza kusaidia potential scandals huko mbeleni.
Mkuu Pasco: Napingana na wewe kwa nguvu zote kuhusu hapo nilipo-highlight na red. Serikali hii katu haina utawala wa sheria na mifano ambayo ipo ni mingi sana, nawe unafahamu fika. ....
Una maana uamuzi wa kulipa dola milioni tano kama sercurity ya kuhairisha kesi? If so, then Tanesco wanaweza kukata rufaa kwenye mahakama za Uingerezeza. Lakini mahakama za UK haziwezi kutengua uamuzi uliotolewa na ICC Tribunal. Pia for update, there is no longer the House of Lords. Siku hizi inaitwa Supreme Court. House of Lords imebakia kuwa sehemu ya bunge tuu.
Wakuu, ngoma bado mbichi?
See the latest 'music'
CCM na serikali yake wasipoondoka madarakani nchi haitaendelea .. i swear
Dowans wana haki kwenye hii issue,wether we like it or not.Serikali hata iwe ys Shetani huwezi kuwapa watu mkataba wameutimiza halafu uwaambie basi ondokeni, siwalipi!
Hata Nyerere aliwahi kufanya hivyo kwa Tiny Rowlands, alikiona cha mtema kuni. Alisema hatazami nyuma atageuka jiwe. Tiny akamwambia hujui sheria wewe. Baada ya muda, mbona Nyerere alirudisha mali zao zote na kuwalipa hasara zote juu. Aliufyata. Mcheze na Watanzania tu, msicheze na mijitu inayojuwa biashara za kimataifa. Kiranga komo! siku ingine itakuwa ni fundisho la kukurupuka kujidai kudhulumu eti kwa kuwa ni Mwaarabu. Huyo Mwaarabu sasa, anafanya mavitu yake, na kila tunapozidi kuipinga hukumu ya ICC ndivy mifedha yake inavyozidi kuongezeka, bureeeee "bilash" kisemeo cha waarabu.