JF DOCTORS' nahitaji msaada wenu.

tbl

Senior Member
Mar 29, 2011
116
41
Hellow doctors please naomba msaada wenu.mara tu ninapoanza menstruation period huwa nakuwa na hasira za ajabu ajabu sana,tukipishana kauli kidogo tu na mtu yeyote ntamuwakia hatari.hali hii kwa mara ya kwanza aliigundua rafiki yangu huwa najitahidi sana kuepuka lakini nnachoshtukia nimeshakwazana na mtu najutia tu.msaada wenu tafadhali nna matatizo gani mie.
 
Ni hali ya kawaida kwa mwanamke kuwa na hasira sana kipindi anapokaribia kuinia mwezini, cha msingi ni kuwa aware na mzunguko wako na kujifunza jinsi ya kucontrol hasira zako "Anger management" ukijua hilo wala hutapata shida, pole sna
 
Hata mimi napokaribia huwa very angry utazan m2 mwenye mimba changa, pia huwa natoa onyo kwa wa2 wangu wakaribu nawambia kabisa BEWARE
Hii inasababishwa na mabadiliko ya hormone ivo kuleta k2 knwn as MOOD SWING ambayo wengne huwa wanafeel very sad and lonely, wengne very angry kama mimi, mwingne ana loose confidence e.t.c e.t.c
 
Pole sana mkuu tbl

PMS- Shida Wakati wa Hedhi
Wanawake wengi huwa na mabadiliko ya kimwili na hisia kabla, baada na wakati wa hedhi. Haijulikani vizuri ni nini kinachosababisha PMS. Dalili huja wiki moja au mbili kabla ya hedhi. Watu wengi hutoa mzaha kuhusu PMS na hawaichukulii kwa uzito. Ukweli ni kuwa hali hii huweko. Waweza kuwa hamu kubwa ya chakula fulani, kuumwa na matiti, kuvimba mwili na mabadiliko katika hisia.


Ishara zake ni zipi?

Kubadilika kwa hisia
Kukasirika upesi
Kulia bila sababu
Kuwa na wasiwasi
Tamaa ya chakula
Maumivu tumboni au mgongoni
Kufura au kuumwa na matiti
Kuvimba mwili


Utatibu vipi PMS?

Kati ya wanawake 5 mmoja ana PMS. Mabadiliko ya hormone huleta dalili za PMS. Kuna mambo unaweza kufanya ilikukufanya uwe na raha.

Kula vyakula bora vya kujenga mwili
Pumzika, fanya mazoezi ya uvutaji pumzi ndani na nje
Meza dawa za kutuliza maumivu kama Panadol
Tumia chupa yenye moto kujikanda sehemu ya tumbo inayouma
Mueleze daktari wako maumivu yakizidi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom