Msaada: Period (hedhi) inanitesa

Loimata

JF-Expert Member
Dec 1, 2022
249
528
Habari zenu wakuu.

Nachukia the way ninakua ninapokua kwenye hedhi.

Ninapokua kwenye siku zangu mahusiano yangu na watu wengine yanakua hatarini.

Mwanzoni nilikua nachukulia kawaida ila sasa hivi nimejua hili ni tatizo tena kubwa na ninaomba anayeweza kunisaidia anisaidie nifanyaje mana hata najiuliza kama nikiolewa kuna atakayeweza kuishi na mimi kila mwezi siku tatu nakua wa ajabu😭.

Hili tatizo limesababisha nipoteze wafanyakazi wengi wazuri.

Hapa ninavyoandika nimetoka kufanya maamuzi mabaya sana na ninajutia ila sijui kama niliyemfanyia anaweza kunisamehe mahusiano yarudi.

Nimekuja kukumbuka nimefanya niliyofanya sababu ya period wakati niko bafuni naoga.

Cha ajabu ni kwamba,hizo siku tatu zikipita huwa najiahidi kutofanya maamuzi yeyote ya hasira nikiwa period ila nikiingia tu period zile siku tatu za mwanzo nakua na moody mbaya na mtu akiniudhi kidogo tu nahuzunika sana,naweza kulia tu au kuamua kujitenga na huyo mtu.

Najaribu sana kuji control ila mwishowe najikuta naharibu tu😭😭.

Msaada wenu please na please naomba msinihukumu mana jinsi ninavyojisikia hovyo muda huu anajua Mungu tu.
 
Pole mwaya! Hauko mwenyewe. 🫂

Kwasababu unajua tatizo lako, jaribu kua unaji-isolate kwa muda na kama mtu akikukwaza jitahidi usi-react kwa wakati huo. Kingine, ni muhimu watu wako wa karibu wakijua huwa unakua na siku mbaya during your period ili na wao wajue jinsi yaku-deal na wewe kwa wakati huo.
 
Asante dear.
Nitaongeza kujitahidi.
 
Bora wewe wengine wanapata cramps na body temperature ina -raise 😃😃😃 unakaa kizembezembe ka.kuku anaeumwa 😅😅😅😅

By the way jaribu kujizuia ainisha faida na madhara yake, then stick na hayo madhara yaani ukitaka kufanya then kumbuka utamdhuru fulani then mood ina change automatically
 
Hapa nina homa,kichwa kinauma,kichefuchefu ni mawenge tu.

Ntajitahidi
 
Back
Top Bottom