Muhimu hakimiliki za watoa mawazo zilindwe..!!Wana JF
Nimekua nikipitia jukwaa hili la businesss and economy na kukutana na mawazo mazuri sana ya biashara kutoka kwa members wengi
Naomba nitoe wazo la kuanzishwa kwa mashindano ya mawazo mazuri ya biashara kwa members wa JF
Mashindano haya yanaweza kuratibiwa kwa ushirikiano na UDEC (University of Dar es salaam Entrepreneurship Center)
Mashindano haya ya mawazo ya biashara yatakuwa ni challenge kwa wote wenye mawazo mazuri na chachu ya kuwawezesha ili mawazo hayo yaweze kutekelezeka na kufanikiwa
Mashindano haya basi yanaweza kuwa katika madaraja mbali mbali kutokana na kiasi cha mtaji wa kuanzisha biashara, yaani kunaweza kuwa na daraja la kwanza ambalo ni biashara mpaka Tsh. 25m, daraja la pili mpaka Tsh. 15m na daraja la tatu mpaka Tsh. 5m, pia kunaweza kuwa na washindi maalum (special category) kama vile kilimo na ufugaji, mazingira na utalii
Mashindano haya yanaweza kupata udhamini kutoka makampuni na wafadhili kama airtel, TPSF, TBL, SIDO, UNIDO, TCCIA, TIB, NMB na wengine wengi
Mashindano haya pia yatatoa fursa za kutoa elimu ya ujasiriamali kwa washiriki, mentorship, networking, market opportunities, financial assistance opportunities na kuwawezesha washiriki kuwa marafiki wa mabenki na taaasisi za kifedha kwa kuwafanya kuwa wanakopesheka
the competition is suggested to be 80% online
nawakilisha
Muhimu hakimiliki za watoa mawazo zilindwe..!!
Mkuu Bongo sheria za hakimiliki ziko katika vitabu tu.Ningumu kuzi Police kama ugumu wa TBL kuuza Juice.Muhimu hakimiliki za watoa mawazo zilindwe..!!
Usipime kaka.... ujanja KUPATA si KUWAHI....!!!ha ha ha haaa
mkuu unaogopa wata paste idea yako fasta
Bongo unauza idea unapondwa..ukimpa kisogo mtu anaifanyia kazi na huna pa kupigania ubunifu wako... hakia unaipata AHERA..UK na Marekani kumewahi kuwa na TV show za watu ku-pitch business ideas zao to potential investors. Idea ikiwa nzuri basi unajipatia partner, mwekezaji au mzunuzi wa shares. You may be onto something here...
I ain't no fool, idea is all that matters...people like fallen Jobs kept apples to the sky bse of his unique ideas! Beside we don't have patent/copyright laws in place in tz!
My JF Family, niliwahi kuhudhuria International Trade Fair 2008.niliona kampuni inayouza mitambo ya kutengeza Cement.kuna mtambo unaanzia Dola Elfu 40.ipo inayozidi hapo.Founder wa hii kampuni ni Mtu wa INDIA.yeye alianza na mtambo wa kutengeneza 200KG/Day. akawa anauzia majirani zake,baada ya miaka kadhaa akafungua kiwanda cha kutengeneza viwanda vya cement.siku hiyo nilikutana na Mjukuu wake huyo mzee.
Sikuhishia hapo nikafanya tafiti online nikagundua China wanakuletea mtambo na mafundi wawili onsite for 1yr.na bei za wachina kama tujuavyo ni za kujipimia tu.
Wazo langu:JE Saccos ikishasimama wima,tufikirie jinsi ya kuweza ktk uzalishaji wa Cement.hiki kiwanda kitakuwa cha wazawa 100%.viwanda vya cement vilivyopo sasa karibuni vyote ni vya wageni.
Cement inatumika na kila mtanzania na itazidi kutumika kwa miaka mingi ijayo.Tafakari Chukua HAtua 🙂