Jessica Cox, rubani mwanamke asiye na mikono

Jessica Cox, rubani mwanamke asiye na mikono

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,286
Reaction score
10,832
2020-01-13 (1).png
2020-01-13.png

Rubani huyu alizaliwa bila mikono kutokana na ‘Genetic defects’, haruhusu hali hiyo kumzuia kuishi maisha ya kukata tamaa. Yeye ndiye wa kwanza mwenye leseni ya urubani japo bila mikono

Ana mkanda mweusi katika taekwondo na hufanya shughuli zingine kama mtu mwenye mikono yote. Hupiga piano na vile vile kupiga mbizi.

Jessica ni ‘MOTIVATIONAL SPEAKER’ anayeishi kwa mifano hai. Alisema watu wengi huwa wanamuona akiwa hana mikono kama sababu ya kuzuia, lakini yuko hapa ili kuwathibitishia wote kuwa hawakosei.

Alipata leseni yake mnamo Oktoba 10, 2008 baada ya kupata mafunzo kwa miaka mitatu. Roho yake ya uthubutu siku zote imekuwa dhahiri kwake. Na mnamo mwaka 2015 aliandika kitabu, Disarm your limits, kitabu kinachoelezea maisha yake.

Alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Arizona mnamo 2005 na digrii katika saikolojia na mdogo katika mawasiliano
 
kuwa mlemavu haifanyi kutotimiza ndoto zako ila kuna mazingira mengine ya maisha ni ngumu kutimiza ndoto zako hata kama sio mlemavu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuwa mlemavu haifanyi kutotimiza ndoto zako ila kuna mazingira mengine ya maisha ni ngumu kutimiza ndoto zako hata kama sio mlemavu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nadhani ulemavu ni neno pana sana ambalo sisi binadamu tunalitumia sehemu chache sana. Kwa mfano kutokuwa na uwezo wa kuyakabili mazingira yanayokuzunguka nalo ni ulemavu haijalishi una viungo vyote au huna
 
Hapa kwetu kimkono kimoja tu kimepinda kidogo tiyari anaanza biashara ya kuomba
Hongera sana dada Ila hiyo ndege mie sitapanda
 
Back
Top Bottom