JESHI letu at 45... Hongereni! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JESHI letu at 45... Hongereni!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Aug 29, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam wakiangalia moja ya vifaru vya kurushia makombora vya JWTZ katika maonesho ya maadhimisho ya miaka 45 ya Jeshi hilo kwenye viwanja vya Kikosi cha Anga Dar es Salaam juzi. (Picha na Mroki Mroki).
   
 2. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #2
  Aug 30, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  [​IMG]


  Unajua siku hizi hatuna yale mambo yaliyokuwa yakitufanya tuwe patriotic na kama yako ni ya kuhesabu...mfano WATAWALA wameamua kuuza na kuibinafsisha almost kila URITHI tulioachiwa kama vile TBC,BANDARI,HESHIMA,RTD na mengineyo...lakini pamoja na ufisadi unaeoendelea wa hawa watawala na tofauti zetu za kiitikadi na namna ya kudeal na hao watuhumiwa nimeone ingekuwa bora ningechukua nafasi hii kwa niaba ya ma "ARM CHAIR GENERALS" wenzangu kuwapongeza hawa walinzi wetu kwa kutimiza miaka 45 bila ya kuwa na misukosuko mikubwa ambayo imekumba nchi zinginezo

  Lakini zaidi ya hayo japo nilipinga wanajeshi wetu kupelekwa kule Comoro bila clear mandate au bila kujadiliwa na bunge lakini nadhani it was a gross mistake for TPDF na WIZARA YA ULINZI kutofanya open HOME COMING PARADE...imagine wanajeshi wetu kutembea from MNAZI MMOJA kupitia Bibi titi Mohammed rd kulekea Alihassan Mwinyi mpaka HQ zao pale UPANGA...

  Lakini wapi sijui Hussein Mwinyi hataki tuone viatu wanvyovalishwa wanajeshi wetu au sijui vipi

  Lakini hayo hapa si mahala pake lakini ningependa kuwashukuru kwa kutuweka katika nafasi ya sisi kukaa na kuwa ma ARM CHAIR CRITICS usiku na mchana ili hali TPDF wakiwa kazini kutulinda 24/7

  [​IMG]

  [​IMG]
  [​IMG]
  Tazama wenzetu wanavyowathamini vijana wao..WATAWALA walaaa hatuna hata mawazo ya kuwaonyesha kuwa tunatambua wala kuwathamini lakini mkae mkijua kuwa some of us are strongly behind you kwa hali na mali
   
 3. J

  JokaKuu Platinum Member

  #3
  Aug 30, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,103
  Trophy Points: 280
  GM,

  ..mimi ningependa sana makamanda wa Operation mbalimbali za JWTZ waandike vitabu.

  ..karibu makamanda wote walioongoza majeshi ya Marekani ktk vita vya Iraq wameandika vitabu.
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Aug 30, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Tuwashuku kwa kupiga watu mitaani na kushiriki ujambazi?????hilo jeshi lipunguzwe if u ask me.na bajeti yake ikatwe nusu,hakuna uwezekano wa vita karibuni na hata vita ikija tutahitaji new tech weapons na sio idadi ya wanajeshi,labda wanastahili pongezi kwa kukaa mbali na siasa,
   
 5. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #5
  Aug 30, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  hivi wakuu tuna silaha kali kama nyuklia au? hii habari ya migingo migingo tungesettle scores once and for all......ungekuwa ni sisi

  anyways siombei vita lakini naulizia tu uwezo wa kizana wa jeshi letu just in case...wana bajeti ya kutosha? mafunzo wanapata wapi, kina nani wanaenda nk.? tuna kikosi cha makomando kama wenzetu (special forces?)
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  hakuna lolote uwezo wetu unategemea zaidi ari na kujitolea na silaha za miaka ya sabini.......wanajeshi wengi wana vitambi these days...............
   
 7. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #7
  Aug 30, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  Rais Kikwete athibitisha Tanzania iko salama

  Na Zaina Malongo

  RAIS Jakaya Kikwete amewataka wananchi wasiwe na waziwasi kuhusu usalama wan chi kwa sababu jeshi lina zana na silaha za kisasa ambazo zitaliwezesha kukabiliana na adui.

  Aliyasema hayo jana alipotembelea maonyesho ya kumbukumbu ya miaka 45 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yanayofanyika katika eneo la uwanja wa ndege wa jeshi, Ukonga, jijini Dar es Salaam.

  Rais Kikwete alisema kuwa nchi ipo salama na ina vifaa vya kisasa na kulipongeza jeshi kwa kuandaa maonyesho hayo ili kuwaelimisha wananchi juu ya matumizi yake.

  “Nimefurahi kuona vifaa hivi vinafanya kazi hapa. Inanaonyesha ni jinsi gani maonyesho yaliyovyoandaliwa na nina amini wananchi wamejifunza mengi dhini ya maonyesho haya na kuona kuwa jeshi letu linavyfanya kazi,” alisema.

  Rais Kikwete alielezwa kwamba jeshi linamiliki ndege zenye uwezo wa kuruka zaidi ya umbali wa kilomita 2,000, 1,800 na 800 kwa saa.

  Hata hivyo, Rais Kikwete alisema kwamba katika mkakati endelevu wa miaka 15 ijayo, jeshi litaongeza zaidi zana za kisasa ambazo zinaendana na teknolojia ya sasa.

  Msemaji wa jeshi, Mbota Mwikambo alisema tangu maonyesho yaanze Agosti 26, wananchi zaidi ya 800 wameyatembelea na kujifunza mambo mbalimbali.

  Maonyesho hayo, alisema yanaandamana na huduma za bure za afya kwa wananchi.

  Wagonjwa wa dharura 403 walipata huduma mbalimbali za tiba, wengine kupima virusi vya ukimwi na miongoni kujitolea damu kwa ajili ya kutunisha benki ya damu nchini.


  Source:
  Mwananchi
   
 8. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #8
  Aug 30, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Ongereni sana wanajeshi wa Tz kwa kutimiza miaka 45 na pia ongereni kwa kuwa wavumilivu kwa kipindi chote hiki cha umri wa mtu mzima.

  JWTZ ni miongoni mwa Majeshi machache sana Afrika yalio bora kiutendaji kwenye medani ya kivita. Ushujaa, wenu uvumilivu na ujasiri katika kuilinda nchi na baadhi ya nchi za Afrika mmeifanya Tanzania kueheshimika sana nje ya mipaka yake.
   
 9. Buricheka

  Buricheka Member

  #9
  Aug 30, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndio, tuwashukuru sana kwa hayo, na pia tuwalaani vikali kwa kitendo vyao vya kidhalimu kupiga na kuteketeza mali za raia, kupiga polisi wa usalama barabara kwa vile hawataki kupanga foleni.

  Hawa si wanapanda mabasi bure, au nini cha zaidi wanataka? Nchi nzima hali ya usafiri ni hiyo hiyo, mbaya, wao hawalipishwi nauli, ungependa tuwafanyie nini cha zaidi?
   
 10. T

  T_Tonga Member

  #10
  Aug 30, 2009
  Joined: Jul 24, 2007
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hili si jeshi la wananchi ni jeshi la mafisadi na majambazi pia ni jeshi la kurepu wanawake pemba ni jeshi la kizamani ambalo halina muelekeo wowote
   
 11. M

  Magezi JF-Expert Member

  #11
  Aug 30, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Sikubaliani na wewe hata kidogo
   
 12. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #12
  Aug 30, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  I agree with you, Joka. Despite recently shortfalls here and there, JWTZ has made our nation proud for such a long time. Kama watu walikuwa wakiiangalia Tanzania enzi hizo, moja ya sehemu waliyokuwa wakiipa heshima ni nidhamu na kazi ambayo JWZT ilikuwa ikiifanya. Haikuwa ndio chuo cha marais wa TZ kama Nigeria, haikusaidia watawala wabovu kama Zaire na kwingine...walijitoa kwa dhati kusaidia watu wengi waliokuwa na matatizo mbalimbali. Ipo haja sasa ya kusoma nini walifanya kina Silas Mayunga, Mwita Marwa, Muhidin Kimaryo,David Musuguri, Abdallah Twalipo na wengine wengi...Natamani ningewasoma kama vile ninavyowasoma kina George Patton, Douglas MacArthur, Erwin Rommel, Montgomerry etc
  Watawala waanze kuona haya kujaribu kulichafua jeshi letu kwenye biashara zao haramu kama Meremeta. Historia ya jeshi letu inakila sababu ya kulindwa na kuheshimiwa.
   
 13. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #13
  Aug 31, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Imebidi nitoke katika self imposed censorship ili niwapongeze JWTZ(Jeiwaa) katika kutimiza miaka 45 ya kuanzishwa kwake.Si vijana wengi wa sasa walio na kumbukumbu halisi ya jeshi letu lilikotoka zaidi ya miaka 45 iliyopita.
  Namshukuru Mungu kuwa mwaka 1964 niliona mikiki ya maasi ya KAR na kushuhudia uanzishwaji wa JW.
  Zamani na mpaka miaka ya karibuni ilikuwa dhambi kuonyesha silaha zetu hadharani.Leo hii self confidence imeongezeka sana mpaka kuonyesha ulimwengu zana za vijana wetu.Sera ya Ulinzi na usalama imetubeba kwa miaka mingi na natumaini maonyesho haya yatarudisha hamasa ya vijana wa miaka 16-20 kujiunga na jeshi kwa ulinzi wa taifa
   
 14. Sonara

  Sonara JF-Expert Member

  #14
  Aug 31, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 730
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tenda watu wataona majisifu weka kando .
   
Loading...