Jeshi la Wananchi JWTZ liendelee kuimarishwa

Kila mtu anaona dunia imekuwa sio Sehemu salama tena na hata Tanzania haipo salama tena.Nashauri jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ liimarishwe zaidi kwa kupewa silaha za kisasa zaidi kama vifaa vya ulinzi wa anga (Air defence systems za kisasa), mamia ya ndege vita za kisasa makombora ya masafa marefu Nk.

Sidhani kama tunauwezo wa kuzuia makombora mengi kama Israel. Tuwatumie marafiki zetu kama Russia, China Nk kuchukua utaalamu, jeshi lisiwe jeshi la ovyo.
China na Russia wajanja wajanja tu...tubaki na marekani
 
China na Russia wajanja wajanja tu...tubaki na marekani
Wamarekani matapeli tu wanatuuzia vifaa feki.china na urusi huwa ni marafiki wa kweli watatupatia maarifa.tena urusi sio wachoyo kabisa wanaweza kupa hata maarifa ya kutengeneza mabomu ya nuclear.
 
We badala utafute pesa unakumbatia umasikini afu eti pengo la walionacho na masikini
Ndg. HIMARS nakuheshimu sana ila kuna baadhi ya maeneo unapwaya sana , yakupasa uulize maswal kwa nini nimeandika hivyo ili nikujubu na si vingenevyo ...
 
Kila mtu anaona dunia imekuwa sio Sehemu salama tena na hata Tanzania haipo salama tena.Nashauri jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ liimarishwe zaidi kwa kupewa silaha za kisasa zaidi kama vifaa vya ulinzi wa anga (Air defence systems za kisasa), mamia ya ndege vita za kisasa makombora ya masafa marefu Nk.

Sidhani kama tunauwezo wa kuzuia makombora mengi kama Israel. Tuwatumie marafiki zetu kama Russia, China Nk kuchukua utaalamu, jeshi lisiwe jeshi la ovyo.
Kwa hofu ya nini.Mbona Israel ana kila kitu na watoto wamepaa juu ya kuta kwa pikipiki bila kuonekana. Muhimu jeshi letu lisifanye dhulma kwa mtu yoyote.
 
Mkuu nchi masikini kama hii tupigane vita kweli. Jw wenyewe wapo bize kukusanya nguo
 
Unaweza kuta jeshini pale kuna 'windows 11 /10' kwenye PC zao... technology hatuna lakini tuna vijana wamesoma IT kibao mtaani
 
Kwa hofu ya nini.Mbona Israel ana kila kitu na watoto wamepaa juu ya kuta kwa pikipiki bila kuonekana. Muhimu jeshi letu lisifanye dhulma kwa mtu yoyote.
Magaidi yanaweza kuanzisha tu vita kuvuruga tu kama wale wa kibiti.bila vifaa vya kisasa tutawapoteza watu wengi.
 
Mkuu unajua bajeti ya air defence system....?
Hapa Africa nani anayo?
Tunapoteza pesa kwenye mambo mengi yasiyo na msingi, nadhani tungepunguza matumizi ya ovyo tungemudu hizo vitu maana hata malipo yake huwa ni kidogokidogo kadiri ya mtavyokubaliana.
Projects za kipigaji kama maboresho ya uwanja wa taifa, ununuzi wa ndege n.k zimechukua kiasi kubwa cha pesa ambazo zingeweza kufanya kitu kingine cha msingi.
 
Mkuu nchi masikini kama hii tupigane vita kweli. Jw wenyewe wapo bize kukusanya nguo
Ndiyo wewe unaona umasikini kwenye nchi hiii wengine wanaona utajiri.wanaweza tu kusababisha vita ili wachukue rasilimali.jwtz wabadilike.
 
Kuna nchi huwa tunagombana nao kisa mipaka wanaweza kujipanga na wao.hakuna nchi ambayo ipo salama.
Nchi gani?!!

Kwa yule mama aliyelitaka Ziwa letu lote?!!!

Huyo alilalamika kuwa NDANI mwake amezungukwa na "sympathizers" wetu

Na yule "slim" mtoto wetu
 
Back
Top Bottom