Travis Kitengo
JF-Expert Member
- Sep 19, 2023
- 489
- 1,200
Jana nimetumia ukurasa huu kulipongeza Jeshi la Polisi wilayani bunda kwa operation iliyofanyika majuzi ambayo ilifanikisha kukamatwa kwa wahalifu watatu waliokuwa wakikabiliwa na tuhuma nyingi za uhalifu.
Hao ni sehemu ndogo tu ya wahalifu ambapo kwa makisio ya haraka 90% ya vijana wanaoishi maeneo mengi ya kata ya bunda mjini wanajipatia mkate wao kwa kupitia uhalifu.Hizi takwimu nina uhakika nazo kabisa.Sasa hii ni hatari sana na kundi hili lisipodhibitiwa mapema na mamlaka husika za kiusalama litaleta athari kubwa sana kijamii na kiuchumi.
Baada ya hao wahalifu kukamatwa nini limetokea?
Baada ya watuhumiwa hao kukamatwa vijana wengi wameanza kutafuta maficho kwa muda ili upepo huu upite kwanza.Baadhi wamekimbilia Kinyambwiga,Tarime nk.
Mtuhumiwa mwingine wa matukio ya kiuhalifu maarufu kwa jina la Kulwa Gidion kapeleka Mali zake ikiwemo Tv kuhifadhi kwa Mzee mmoja ajulikanae kwa jina maarufu la Juma magodoro ambaye hushughulika na shughuli za ushonaji mito ya kulalia,usokotaji nyuzi za pamba ambazo hutumika kwa kuzibia nyufa kwenye mitumbwi.Licha ya Mzee huyu kujishughulisha kitendo chake cha kupenda kununua vitu vya bei chee na hasa vilivyopatikana kwa njia zisizo sahihi kunazorotesha sana juhudi za vyombo vya ulinzi na usalama katika kupambana na uhalifu sababu vitendo hivi huwahakikishia soko vibaka na wahalifu kwa Mali wanazopora.
Swali tu kwa Polisi
Yule bwana anayepelekewa simu baada ya wananchi kuibiwa ili azitafutie soko na kuziflash hafahamiki?Nauliza tu kwa mapenzi mema.Je hafahamiki?Hili ni doa sana kwenu!
Pia yule Jamaa mweusi tii anayevaa kibharagashia ana Timu kubwa sana ya wahalifu wao wanamwita master.Pamoja na kwamba kazaliwa 1979 Bado hajaamua kubadilika na kufanya kazi halali.Ule mgahawa feki ni kiini macho tu mbele ya raia ila huyu Jamaa ndie master plan wa njia mbali mbali mbali za kitapeli.Mbaya zaidi wamekuwa wakiona mtoto kaagizwa kupeleka kutuma hata pesa kwa wakala watamuwahi na kumrubuni mpaka atawaachia.
Licha ya pesa wakikutana hata na mtoto kapewa mzigo wa thamani aufikishe mahala watamtapeli kisha bila kuchelewa hurudi na kubadili nguo haraka sana.Fikeni muulize hili kama nasema uongo.
Niwatolee mfano kwa huyu wa kibharaghashia
Kuna dada mmoja mjaluo ni mfanyabiashara wa magodoro na vipodozi aliwahi kumuagiza mwanae apeleke pesa nyumbani takribani sh.laki Tano,Mzee wa kibharagashia alipousima michezo alimuwahi yule mtoto na kubeba mzigo wote huku akiwa kamhadaa kwa njia zao zile zile.
Bahati nzuri Kuna watu walishuhudia mchezo mzima na ilikuwa rahisi Jamaa kudakwa na kufikishwa kwenye vyombo vya Sheria.Polisi watu kama hawa mnawaangalia tu kama hamuwaoni wakati wanafahamika.Sasa semeni no ili mlinde status ya kazi zenu,Semeni imetosha ili mlinde viapo vyenu!
Alamsiki