Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,836
- 12,016
JESHI LA POLISI KIGOMA LAZUIA MKUTANO WA ZITTO KABWE.
Jeshi la Polisi Wilaya ya Kigoma limezuia mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini Ndugu Zitto Kabwe uliopangwa kufanyika leo katika viwanja vya Mwanga Center, Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Kwenye barua yao kwa Ofisi ya Mbunge huyo, Jeshi la Polisi Wilaya ya Kigoma linadai kuwa limezuia mkutano huo "..kwa sababu za kiusalama kutokana na taarifa za kiintelijensia zilizopo".
Sababu iliyotajwa bila shaka haina mashiko na inalenga kumzuia Ndugu Zitto Kabwe kutekeleza shughuli zake halali za kutumikia wananchi wa Jimbo lake.
Ado Shaibu, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano na Umma, ACT Wazalendo.
17 Januari 2020.
Zaidi soma: Bashiru aanza ziara Kigoma, Zitto Kabwe azuiwa kufanya mkutano