Jeshi la Polisi sio tatizo, ni viongozi

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,879
Binafsi sidhani kama kulichunguza Jeshi la Polisi kutaleta ufumbuzi wa matatizo yanayolalamikiwa na wananchi.

Tatizo la Jeshi la Polisi ni viongozi wake. Viongozi wa Jeshi la Polisi hawana weledi, uadilifu ktk utendaji kazi wao viongozi wa jeshi la polisi wapo kimaslahi na kisiasa, ukienda upande wa usalama barabarani ni rushwa tu

Ukienda upelelezi ndio hakuna kitu ni kubambikiana kesi bila kufuata sheria

Jeshi la polisi mpaka leo hii halina majibu kwa matukio makubwa kama haya

1. Kupigwa Risasi 16 kwa LISSU
2. Kutekwa kwa Mfanyabiashara MO
3. Kupigwa Risasi na kuuawa kwa AKWILINA
4. Kupotea kwa BEN SAANANE
5. Kupotea kwa AZORY

Juzi wakati wa kesi ya ugaidi ni aibu tu kwa jeshi la polisi kesi ya kutungwa ushahidi wa kutungwa hata taratibu za kazi polisi wake hawazijui kesi inafunguliwa kabla ya mtuhumiwa kukamatwa.

Kesi ya ugaidi ya mbowe imelivua nguo jeshi la polisi

Endapo jeshi la polisi na viongozi wake wangekuwa waadilifu na wanatenda kazi kwa kuzingatia pgo yao haya malalamiko ya wananchi yasingekuwepo

Wakati umefika wa kulifumua na kuliunda upya jeshi la polisi kuwatoa viongozi wote na kuanza upya
 
Ukiwa unatowa hoja nzito usiingize mambo ya chadema hoja yako inaonekana haina mantiki maana chadema ni kundi la matusi
 
Vijana mnaojiandaa kugombea ubunge 2025, hata ikitokea mkapata teuzi, kwanza kama tutafanikiwa kupata katiba mpya au hata mageuzi yakifanyika katika katiba iliyopo hali ya siasa nchini kwetu itabadilika.

Katika mamlaka yenu tendeni haki, haki na wena ni keki isiyooza. Kiburi na majivuni havina mwisho mwema.
 
Binafsi sidhani kama kulichunguza JESHI la POLISI kutaleta Ufumbuzi wa Matatizo yanayolalamikiwa na Wananchi.
Tatizo la Jeshi la POLISI ni VIONGOZI WAKE.Viongozi wa JESHI la POLISI Hawana Weledi,Uadilifu ktk Utendaji Kazi
Umeji.contradict. Kiufupi umesema tatizo sio Jeshi la Polisi, ila ni Viongozi wa Jeshi la Polisi (ambao nao wamo katika Jeshi la Polisi)
 
Eti tatiZo sio jeshi la polisi ila ni viongozi halafu bado huoni kuwa jeshi la polisi ni tatizo.

Ukapimwe sio bure.
 
Mkuu tueleze kinaga ubaga kwenye suala zima la kufumuliwa ,lifumuliwe kiaje yani maana naona umekuwa wimbo"jeshi la polisi lifumuliwe".
 
Umeji.contradict. Kiufupi umesema tatizo sio Jeshi la Polisi, ila ni Viongozi wa Jeshi la Polisi (ambao nao wamo katika Jeshi la Polisi)
Kukubali kwamba tatizo ni jeshi zima ni kama kuamua kichoma shamba zima la mahindi kwa sababu kuna nyoka kaingia humo,hasara ni 100×.
Jeshi la polisi ni taswira halisi ya namna nchi yetu ilipo kwa sasa,na siku watawala watakapoamua jeshi hilo libadilike,basi ukombozi kwa wananchi umefika.
 
Polis wa Tanzania ni tatzo kubwa sana na hii pia inachangiwa na idala ya polisi kuchukuwa vijana wengi ambao ni kama wamekata tamaa, shida kubwa iliyopo polisi ni kubebena sana ndo maaana hata jana polisi aliempiga risasi mtu nje ya mgodi wa North mara amehamishwa hiyo hiyo jana, tunaposema polisi wanavunja sheria na hawaaminiki watu muwe mnaelewa ikiundwa tume huru na ya haki na wananchi wakaamua kusema ukweli juu ya polisi hii nchi itazizima kbsa
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom