Jeshi la polisi mpaka leo haliwatambui mazombi Zanzibar

GHIBUU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
4,278
2,000
NI MAZOMBI TENA YAKIENDELEZA SERA YA MAPINDUZI DAIMA

Ndugu Abdullah Ahmeid juma pichani mwenye umri wa miaka 29, mkaazi wa mchangani kisiwani Unguja. Ni mfanya biashara ndogo ndogo. Amepigwa vibaya na Mazombi na kunyang'anywa kila kitu chake. Pia kumvua nguo ikisha kumchoma moto mikononi na miguuni na kumpora laki 8. Vitu walivyomuibia ni saa ya mkononi, simu kisha na kumvua nguo zote na kumuacha uchi kama alivyo zaliwa.

Hivi sasa yuko kwa mama yake mtoni akiuguza majeraha, mama yake anaitwa Rukia Ali Faki ni mstaafu wa fire brigades.

Haya hapa ni maelezo ya mama yake ndugu Abdullah Ahmeid juma

"Serekali yenu hawataki watoto wetu wabangaize. Wamewavunjia michenzani kwaio anapita akibangaiza nguo zake anauza mitaani huko wamemkuta kaziweka chini kwahiyo wamemkamata, wakamvuruga, wakampiga, wakammaliza kila kitu wakamuibia kila kitu wakamuacha uchi kama alivozaliwa. Saa, Simu pesa taslimu laki nane na nguo zote na vitu vyote alivyokuwa navo kisha wakampiga kisha wakamtupa"

"Nnae mwenyewe tumempeleka hospitali jana kapata huduma za shindano kwahiyo ninae mwenyewe namtia tia dawa hapa. Nimeenda kumnunulia dawa ya moto kwa sababu wamemuunguza kwa maplastik kwenye miguu mote mpaka mikononi, kama mwizi alivyokuwa. Kwahiyo nimemshamnunulia dawa ndio namuuguza hapa hapa nyumbani kwangu mniombee dua M/Mungu amjaalie apoe".
Breaking news:- hio kijana mwenzetu huyoo amepigwa na mazombi huko Unguja ekesha amenyanganywa pesa kiasi cha laki 8 lkn kosa lake ni kupanga biashara chini na kutafuta riski yake na hizo ndio ajira zenyewe kwnn wampige kama hivyo halafu wamchukulie kila kitu chake wam bakishe uchi Serikali ya Unguja na Polisi wake hivi vitendo hawavioni hemu nisaidie kuwafikishia hii habari haki za Binaadamu...
FB_IMG_1497403608773.jpg
FB_IMG_1497403599547.jpg
FB_IMG_1497403617045.jpg
 

Nazjaz

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
6,587
2,000
Hiyo ni KAZI ya CCM ambayo nyie Waunguja mnajivunia na kukiona Mali yenu. Endeleeni kuvumilia uchungu wa ndoa na Jambazi, wenzenu Pemba wanajielewa.
 

GHIBUU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
4,278
2,000
Inasikitisha mpaka leo hii yanaendelea Zanzibar huku jeshi la polisi likikaa kimya, inakuwaje watu wako mitaani wasikamatwe, wa mitandaoni wamakamwa, polisi wanatumia intelligence gani?
 

Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
6,683
2,000
KUNA MOVIE MOJA YA MAZOMBI HAPA NAHISI NAWEZA KUWA MSAADA KWA POLISI
 

aleesha

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
597
1,000
Kwa muda tumekuwa tukisia vitimbi na vitisho.Kiukweli na tunataka iaminike kuwa vikundi vinavyoleta fujo vina imani ya kuwa havitopata majibu na wazanzibari watakaa wakilia-lia pembezoni.Hivi vikundi kama mazombi vinabadilika majina tuu.Miaka ya zamani vikiwa na majina kama janjaweed na sasa vikibandikwa majina ya mazombi.Nadhani ni hao hao tuu, na hatubahatishi hivi ni vikundi vya SMZ kama JKU n.k. ambavyo vina ushirikiano na vile vya ulinzi vya Tanganyika.

Kinachosikitisha hapa ni kuona wananchi wakijiinamia kama vile hawana mikono au hawajui kutia makali mapanga.Hiki ndio nataka nitoe rai kwa zama hizi za leo ukizingatia mawasiliano ya mitandao na masimu yaliojaa.Nitarudia hapo mbele jinsi ya matumizi ya mitandao na jinsi gani yanaweza kutumika kujipanga na kujihami dhidi ya uovu katika mitaa, vijiji na vitongoji tunavyoishi na familia zetu.Ni lazima tuhakikishe na kwa uwezo tuliopewa na Allah kujihami na kulinda familia zetu.Hili ni jukumu letu si la mwengine.

Ushauri wangu sio mpya miaka ya zamani imetumika sana kueka askari wa kijamii kila kitongoji kulinda wezi na majambazi.Nadhani muda sasa umeshafika wazanzibari wa kila kitongoji wakaunda vikundi vya kujihami na wote wakawa na mtandao ambao kila ataevamiwa usiku anawasiliana kwa kutoa taarifa ya dharura kwa askari jamii ambao wanazuka haraka kwenye tukio na kurekebisha mambo au kutoa suluhusho.

Nadhani hii ni njia rahisi na hahitaji leseni wala unifomu.Isifike hadi sehemu tena tunavamiwa majumbani na mazombi na wananchi wakawa wamekaa tuu na kujinamia chini.Hii inasikitisha kiufupi waliotarajiwa kulinda sheria na watu wake, wao ndio wako mstari wa mbele kuzivunja.Hapo sitarajii kusikia waliosababisha kifo kufikishwa mahakamani wala kutajwa, watabakia ‘wasiojulikana hadi kiama’.

Wasalaam,
Allah alete subra katika kipindi hiki kigumu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom