Jeshi la Polisi linamsaka aliyemfanyia Mtoto Kitendo cha Ukatili na Udhalilishaji kwa Kumning’iniza kwenye mti

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,554
IMG_8540.jpeg

Jeshi la Polisi limeona video hii fupi (clip) ikimwonesha Mtoto aliyefanyiwa vitendo vya ukatili na udhalilishaji na limeanza kuifanyia kazi kuanzia ilipoanza kusambaa ili aliyefanya kitendo hicho cha kinyama kisichokubalika aweze kukamatwa na hatua zingine za kisheria ziweze kufuata.

Mtoto huyu lazima atakuwa na Mama, Babu, Bibi, Shangazi, Mjomba, Majirani na Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Tunatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za nani alifanya kitendo hicho au kilifanyikia wapi asisite kutoa taarifa Polisi au kwa Kiongozi yeyote yule ili kufanikisha kukamatwa kwake.

Imetolewa na:
David A. Misime - SACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu Ndogo ya Polisi
Dar es Salaam, Tanzania

Pia soma: Serikali imchukulie hatua kali za Kisheria huyu aliyemtesa Mtoto kwa staili hii
 
View attachment 2754985

Huu si unyama bali ni ushetani na uuaji
 
Huwa tunawalaumu watu kurekodi badala ya kusaidia. Ila hapa kama jamaa asingerekodi huyu mtoto sijui angeteseka mpaka lini, Na angekuja kuwa na utu wa aina gani ukubwani.
 
Hio ni sample ya namna Yesu alivyotwaliwa kwenda kwa Baba kupitia wa akina pilato wa kiyahudi
 
Akikamatwa atiwe NONDO inchi 4 kwenye tupu yake ya nyuma.
Tumechoka wangese kwenye jamii zetu.
 
Back
Top Bottom