Ado Shaibu
Member
- Jul 3, 2010
- 99
- 108
JESHI LA POLISI LINAWABEBA DED WA ITIGI KWA MANUFAA YA NANI?
Chama cha ACT Wazalendo kimesikitishwa na taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida iliyonukuliwa na vyombo vya habari kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi Ndugu Pius Luhende "alikuwa nje ya kanisa wakati mauaji yakifanyika hivyo basi yeye si mtu aliyemfyatulia risasi Ndugu Isaka Petro".
Maelezo haya ya Jeshi la Polisi yanakwenda kinyume na maelezo ya Ndugu wa marehemu na waumini wote waliokuwepo ndani ya kanisa siku ya Jumamosi ya tarehe 2 Februari mwaka huu, wakati mauaji hayo yakifanyika.
Kwa mujibu wa Baba wa Marehemu na waumini wa kanisa hilo, aliyemfyatulia risasi marehemu ni Mkurugenzi wa Itigi Ndugu Luhende. Maelezo kuwa Mkurugenzi wa Itigi siye aliyefyatua risasi, polisi wameyatoa wapi?!
Ni jambo linalofadhaisha kwamba jeshi la polisi linajaribu kufanya hila ili kupindisha haki kwenye tukio hili la mauaji ya kinyama yaliyofanyika kwenye nyumba ya Mungu.
Tunachojiuliza ni kwamba Jeshi la Polisi linayafanya yote haya ili kumnufaisha nani na kwa maelekezo ya nani?
KAULI YETU:
1. Tunaendelea kulaani tukio hili la kinyama lililofanyika kwenye nyumba ya ibada. Bila shaka haya ni matunda ya vitendo vya kibabe vilivyoshamiri katika serikali ya awamu ya tano miongoni mwa watendaji wa serikali na kufumbiwa macho na serikali kuu.
2. Tunataka haki itendeke bila kuangalia nani ana cheo gani au ana mahusiano na mkubwa gani serikalini. Kila mtendaji wa serikali na askari aliyeshiriki kwenye kitendo hicho cha kinyama achukuliwe hatua za kisheria.
3. Tunawakumbusha Watendaji wa Serikali hasa Wakurugenzi, Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa kuzingatia sheria katika utekelezaji wa majukumu yao.
Ado Shaibu,
Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi,
ACT Wazalendo.
08 Februari, 2019.
Sent using Jamii Forums mobile app