Jeshi la Polisi lazima tukio la ujambazi, wahalifu watimua na kuacha bunduki ikiwa na bendera ya CHADEMA

Habari za kiwendawazimu. Hawa jamaa ukichunguza sana bunduki ambazo huwa zinaoneshwa ni zile zile, na lazima ziwe kuukuu!! Ina maana majambazi wote kiwanda chao ni kimoja au zile zile ukifika muda wa maoneshwa hutolewa?
 
Wamenikumbusha Igunga CCM walipochoma nyumba, kesho yake polisi wakaokota kikaratasi ambacho hakikuguswa hata na moshi kimeandikwa CHADEMA yaani ni mambo ya kitoto kabisa.
 
Huwa wanasema eti nchi ikitawaliwa na upinzani itatokea vita.
Kwahiyo wanataka kuwaaminisha wananchi kuwa hiko chama hakifai kutawala na kinajihusisha na vitendo vya kiharifu. Siasa zisizo na tija hizo!
 
Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga, limefanikiwa kuzima tukio la ujambazi katika kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia cha Jielong Holdings (Tanzania)

Aidha Majambazo hayo yametimua na kutelekeza Bunduki aina ya AK-47 yenye namba 18116428 iliyokuwa imefungwa kwenye skafu yenye rangi ya nembo ya CHADEMA pamoja na Pikipiki aina ya SANLG

Kamanda wa Polisi wa Shinyanga ACP Simon Haule akionesha pikipiki aina ya SANLG iliyotelekezwa na Majambazi hao

Kaimu Meneja Mkuu wa kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia cha Jielong Holdings (Tanzania),Bw Liu Buhua akilishukuru jeshi la polisi mkoani Shinyanga kwa kuzuia uhalifu uliotaka kufanywa na majambazi
hôngera sana serikari awamu ya tano imethibiti uhalifu ipasavyo!!
nb;tunaomba muda uongezwe kama rwanda mkulu. tunakupend
 
Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga, limefanikiwa kuzima tukio la ujambazi katika kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia cha Jielong Holdings (Tanzania)

Aidha Majambazo hayo yametimua na kutelekeza Bunduki aina ya AK-47 yenye namba 18116428 iliyokuwa imefungwa kwenye skafu yenye rangi ya nembo ya CHADEMA pamoja na Pikipiki aina ya SANLG

Kamanda wa Polisi wa Shinyanga ACP Simon Haule akionesha pikipiki aina ya SANLG iliyotelekezwa na Majambazi hao

Kaimu Meneja Mkuu wa kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia cha Jielong Holdings (Tanzania),Bw Liu Buhua akilishukuru jeshi la polisi mkoani Shinyanga kwa kuzuia uhalifu uliotaka kufanywa na majambazi
Hii sinema ya kihindi ipelekeni Lumumba. Hivi mnawachukuliaje wa Tz, mnadhani ni mazezeta kama nyie wa " ndiyo mzee? "
 
Sasa wamekimbia vp hao majambazi wafia chama??? Au polisi walivyoiona Bendera ya CHADEMA walishikwa na butwaa wakazani ni FREEDOM FIGHTERS? Au,,, au,,, au,,, mbona ss tuko hv lakini?? Nakuja!!!!
 
Hivi kweli katika hali ya kawaida kwa sasa na mazingira ya kisiasa, mwizi anaweza kujificha katika utambilisho wa upinzani achilia mbali CHADEMA? Ni kipofu tu 'ataona' haya na kuyaamini.
 
Back
Top Bottom