Jeshi la Polisi lazima tukio la ujambazi, wahalifu watimua na kuacha bunduki ikiwa na bendera ya CHADEMA

Ujinga huu sijui utaisha lini. Kwanza tuwaulize mlipeleka wapi visu vya cuf.
Ndiyo maana hao polisi wamebaki ni wa kuzuia chadema tu. Jambazi mwenye ak 47 mtamuweza wapi nyie milenda.
 
Wakuu mnakumbuka kontena la visu vyenye rangi ya bendera ya CUF vya Omari Mahita?!!! Mnakumbuka juzi kati Omari Mahita alieleza juu ya ushauri wake kwa IGP wa sasa juu ya namna ya kuwashughulikia wapinzani.
Haya ndiyo matunda ya ushauri wa Mahita, Bendera ya Chadema kwenye AK47 ya Majambazi!!!!!!
 
Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga, limefanikiwa kuzima tukio la ujambazi katika kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia cha Jielong Holdings (Tanzania)

Aidha Majambazo hayo yametimua na kutelekeza Bunduki aina ya AK-47 yenye namba 18116428 iliyokuwa imefungwa kwenye skafu yenye rangi ya nembo ya CHADEMA pamoja na Pikipiki aina ya SANLG

Kamanda wa Polisi wa Shinyanga ACP Simon Haule akionesha pikipiki aina ya SANLG iliyotelekezwa na Majambazi hao

Kaimu Meneja Mkuu wa kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia cha Jielong Holdings (Tanzania),Bw Liu Buhua akilishukuru jeshi la polisi mkoani Shinyanga kwa kuzuia uhalifu uliotaka kufanywa na majambazi
Kwa ujinga kama huu Trump alikuwa sahihi kabisa
 
Teteeeee....haya ni sawa na Meli zilizokamatwa na madawa ya kulevya zikipeperusha bendera ya Tanzania. Malipo hapa hapa duniani-tumeona nguvu mliyotumia kukanusha
 
Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga, limefanikiwa kuzima tukio la ujambazi katika kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia cha Jielong Holdings (Tanzania)

Aidha Majambazo hayo yametimua na kutelekeza Bunduki aina ya AK-47 yenye namba 18116428 iliyokuwa imefungwa kwenye skafu yenye rangi ya nembo ya CHADEMA pamoja na Pikipiki aina ya SANLG

Kamanda wa Polisi wa Shinyanga ACP Simon Haule akionesha pikipiki aina ya SANLG iliyotelekezwa na Majambazi hao

Kaimu Meneja Mkuu wa kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia cha Jielong Holdings (Tanzania),Bw Liu Buhua akilishukuru jeshi la polisi mkoani Shinyanga kwa kuzuia uhalifu uliotaka kufanywa na majambazi
IMG-20180118-WA0033.jpg
 
Nakuapia kwa mama yako kwamba kamwe hutakaa umsikie mmiliki wa pikipiki wa mwendeshaji wake. Hizo ndizo akili za akina Heri. Uliwahi kusikia kontena la visu la Mahita na CUF lilipigwa mnada na dalali gani?!!!!
Mambo mengine hayawekwi hadharani kwa kwa sababu za kiusalama, lakini hatua zinachukuliwa kama kawaida. Hilo tukio kama wanahabari watalifuatilia watapata majibu tu, sema wanahabari wengi hawamalizi habari..
 
Hivyo zilikuwa ni sababu za kiusalama kutangaza hadharani vile visu siku chache kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2000, na mara baada ya uchaguzi kupita ikawa si salama kutangaza hatua walizochukuliwa waleta visu, siyo?!!!
 
Nitaendelea kuusoma huu uzi kwa taratibu sana, mpaka hapo muda utakapo muda utakapo ruhusu niandike ya kwangu.
 
Si mbaya saana kwani tumetambua kuwa ukiwa na bendera ya CDM polisi hawakuui wala kukufyatulia risasi. Next time nendeni na kadi kabisa mchana muonekane huenda wakawasindikiza
 
Ukisikia siasa za majitaka ndio hizi. Yaani Chadema wanaenda kufanya uhalifu wakiwa wamebeba bendera yao. Na isitoshe wanafanikiwa kutoroka bila hata mmoja wao kukamatwa au hata kujeruhiwa! Tuwasubiri maana watakuwa wanasakwa. Muda si mrefu tutawasikia wakifikishwa mbele ya sheria.
 
Inasikitisha kuona Jeshi la Polisi likitumika kufanya siasa za kipuuzi namna hii. Mwaka 2005 walifanya ujinga huo huo walipofai eti wamekamata shehena ya visu vyenye rangi kama bendera ya CUF. Kumbe ilikuwa ni kukichafua tu hicho chama siku moja kabla ya uchaguzi
 
Huu ni uongo wa POLISI WETU.
mara nyingi HAWA POLISI ndio wanaopanga matukio mengi ya ujambazi.
Bendera ni kitambaa kama khanga nk....mmiliki halisi wa silaha hapa nchini ni majeshi yetu.
Kwa hiyo Kaimu RPC shinyanga jaribu kutumia busara unapopanga kudanganya jamii ya watu wenye taaluma tofauti na wenye uelewa kukuzidi wewe .
ELIMU YA OPEN UNIVERSITY.
Exactly
 
Kama ni kweli Chadema waliopata kura milioni 6 za urais 2015 wafanye vituko vya namna hii?
Nawashauri police mhalifu ni mhalifu tu si busara kumuunganisha na Chama au dini yake,shughulikeni na mhalifu tu.
 
Back
Top Bottom