Jeshi la Polisi kuweni waaminifu kwa vitu vya mahabusu mnaowaweka ndani maana vingi vinanapotelea mikononi mwenu

Babe la mji

JF-Expert Member
Dec 14, 2019
983
2,053
Mwezi uliopita ndugu yangu aliwekwa ndani kwa kosa dogo tu tena la kusingiziwa na jamaa flani mwenye hela, kisa Cha ndugu yangu kuwekwa ndani ni kumdai huyo bosi hela yake.

Kwa ufupi ndugu yangu kazulumiwa na huyo bosi Sasa kudai chake jamaa kamuweka ndani eti anadai ndugu yangu anataka kumtapeli.

Huyu ndugu yangu alikua anafanya biashara na huyo bosi Sasa hesabu ndo zikaleta shida kwa mjibu wa huyu ndugu hesabu zipo sahihi Mana Kila kitu kaandika na ilitakiwa alipwe milion Tano lakini bosi anadai ni milion tatu tu.

Sasa kipindi anakamwata na kuwekwa ndani huyu ndugu yangu alikua na smartphones mbili na hela kama laki tatu,cheni na saa.

Kwa Sababu hili tukio lilifanyika jioni alikosa dhamana tukaambiwa twende kesho yake .Hivi vitu aliviandikisha Kaunta Sasa siku ya pili asubuhi ndo tukamwekea dhamana.

Shida ikaja vitu vyake havionekani Kila akienda anaambiwa yule afande hayupo asubili aludi Leo ni kama mwezi vitu vyake havijaonekana.

Hawa Polisi wachache amabao sio waaminifu wanahalibu sifa nzuri ya jeshi letu la Polisi kwa tamaa zao.

Nawaomba mjirekebishe.
 
unategemea nini kwa polisi hawa ambao kigezo cha kujiunga na jeshi inabidi uwe umefeli?

Yani unatarajia nini cha maana kutoka kwa failures?
 
Back
Top Bottom