Jeshi la polisi kumkamata Dr. Slaa

Jeshi la polisi kumkamata Dr. Slaa

Sababu ya yote hii hata mwanangu wa miaka 10 atabaini. Ni uchungu mkubwa wanaopata CCM kuona mashina yao yanapukutikia CDM -- kutokana na mikutano ya Dr. Slaa. Kimbunga hiki hakiwezi kurudi nyuma ng;0 hata CCM wakitumia njia hii.

Mimi naona Dr Slaa akamatwe kwani kuongezewa kesi moja na iwapo anazo nyingine kunaipunguzia CDM nini? Wamkamate tu kwani hatua hiyo itaongeza kasi ya CCM kukimbiwa.

Haya makosa hufanywa na viongozi wengi hasa wa nchi za Kiafrika, kwamba wakiwalimbikizia kesi viongozi wa wapinzani, basi wananchi watawachukia na kuzidi kuwakumbatia watawala. Kinyume chake ndiyo hutokea.
 
Baada ya singo inayoimbwa na cdm ya mawaziri 8 kujiuzulu na ikifanya vizuri sokoni,waacha wasababishe another single ambayo itadumu kwa wadosi kwa miaka 2..wamkamate then?
 
kazi ya polisi ni kulinda usalama wa raia na mali zao. sasa hapo nani wa kukamatwa? aliyejuruhi raia au aliyewakumbusha majukumu yao? ama kweli nimeamini polisi hawana elimu...hata sentensi ya maneno saba wanashindwa kuielewa?
"kulinda usalama wa raia na mali zao"
 
Hana lolote, matamko yake ni ya uchochezi tu, na ashukuru serikali kuwa sikivu na kuruhusu vilaza kutukana kadiri wanavyoweza, tofauti na hapo alitakiwa saa hizi awe ndani.
.
"WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
 
Sina uhakika kama tishio la kaimu kamanda wa polisi mkoa wa mwanza kumkamata Dr. Slaa, litakuwa limezingatia weledi wa kipolisi.
Kwamba ametamka maneno ya uchochezi geita na mwanza lakini hawakumkamata siku ile ile hadi wanasubiri kupiga siasa kwa kuuza nyago mbele ya kamera. Hapa mtu hupati shida kutambua kwamba wanafanya hivyo kwa maelekezo ya magamba.
Kama kweli wanamtafuta hata akiwa mkoa gani anakamatwa tu kisha anakodishiwa ndege ama helikopta na kupelekwa mwanza kujibu tuhuma zake!
 
Chenye akili kivyako ni kumwacha aendelee na uchochezi wa uvunjifu wa amani?

ni vema ukajivua gamba coz kila niki log in na kuona id yako na scrol fasta mana nimezowea pumba toka kwako mkuu.
 
Hawa wamekosa kazi za kufanya, wameshindwa kuwakamata mafisadi wa rada, richimondi, meremeta, tbs, dowansi, epa, nk,......ukiwakuta OSTERBAY DAR ambako majizi/majambazi /matajiri wakubwa wanaoiba mali ya uma kwenye miradi mikubwa ya nchi wanakoishi wanasema wanadumisha ulinzi au wako kwenye doria, ukiwakuta MANZESE DAR wanasema wako kwenye msako wa vibaka........
 
Watanzania hatutaki vita bali tunataka amani so kwa vitendo vya slaa vya uvunjifu wa amani hatuwezi kuvumilia hata kidogo na ninawapongeza polisi kwa uwajibikaji wao kwani ni lazima tuitunze amani kwa gharama yeyote.
 
Hana lolote, matamko yake ni ya uchochezi tu, na ashukuru serikali kuwa sikivu na kuruhusu vilaza kutukana kadiri wanavyoweza, tofauti na hapo alitakiwa saa hizi awe ndani.
.
"WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".

acha uchoko we pimbi nani kakuambia nchi inajengwa na wasomi tu.nchi inajengwa na wakulima,wafanyabiashara,wajasiriamali,wasomi pamoja na siasa safi.so kila m2 akisimama katika nafasi yake mwenyewe na kukawepo na ukweli pamoja na matumizi sahihi ya rasilimali za nchi hakika nchi yetu lazima itapiga hatua.so dr slaa kaza mwendo ili kuleta mabadiliko ya kweli nchini sisi tupo pamoja na watakaojudge na kupima kazi yako ni sisi wana
 
sijaelewa hapo.....
anayetakiwa kukamatwa ni nani? aliyewakata wabunge mapanga au ni polisi wasiokua na haki!!!?
 
Jamani, Dr Slaa amewaomba washughulikie matatizo yaliyojitokeza, kama wao (Polisi na Chama chao) wanaona madai hayo hayana msingi, si wayapuuze ?kwani Dr atawapiga? Mbona wanaburuzwa mpaka mimi mwanakiji naona waaaaaazi ! kumbe wakimkamata Dr inasaidia nini ? majambazi watakuwa wamepatikana ? hawaoni kwamba wanawapa "vichwa" hao majambazi wajione kama wanakingwa na nguvu ya dola, wasitajwe, wasishughulikiwe wala mtu yeyote kuomba washughulikiwe kwa haraka ?. Inatupa nguvu kuendelea kuamini kuwa walishiriki matukio maovu na wanajua kilichotokea. They have the whole story !
 
Hana lolote, matamko yake ni ya uchochezi tu, na ashukuru serikali kuwa sikivu na kuruhusu vilaza kutukana kadiri wanavyoweza, tofauti na hapo alitakiwa saa hizi awe ndani.
.
"WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".

Asante kwa kuongea kinyume!
Maana mchochezi na mnafiki mkubwa ni KIkwete na matamko yake yasiyo ya kizalendo............wasikivu ni Chadema.
 
wakishasifiwaga polisi huwa wanapagawa wanataka wakamate kila mtu ikibidi ata wajikamate wenyewe ili wazidi kupata misifa.
 
Wajaribu tu, na huo utakuwa mwisho wao, na serikali yao.
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"] [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Wednesday, 25 April 2012 20:22 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 0diggsdigg

dk%20slaa%2021.jpg
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibroad Slaa

Sheilla Sezzy, Mwanza
JESHI la Polisi mkoani Mwanza limesema kuwa litamchukulia hatua za kisheria Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibroad Slaa ikiwemo kumkamata kutokana na kauli zake za uchochezi alizozitoa katika mkutano wake wa hadhara mwishoni mwa wiki iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Philipo Kalangi alisema kauli zilizotolewa na Dk Slaa ni za uchochezi ambazo zinaweza kuharibu amani ya nchi.

Mwishoni wa wiki iliyopita katika mkutano wake wa hadhara kwenye Viwanja vya Sahara, Dk Slaa alitoa wiki moja kwa Jeshi la Polisi mkoani hapa kuwakamata wale wote waliohusika na vurugu katika uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Kirumba uliofanyika mwanzoni mwa mwezi huu.

Ilidaiwa kuwa vurugu hizo ambazo zinahusishwa na wafuasi wa CCM, zilisababisha kujeruhiwa vibaya kwa wabunge wa Chadema, Samson Kiwia wa Ilemela na Salvatory Mchemli wa Ukerewe.

Katika mkutano wake, Dk Slaa alisema kama Jeshi la Polisi halitawakamata watuhumiwa na kuwachukulia hatua za kisheria ndani ya siku saba, basi yeye mwenyewe atachukua jukumu la kuwahamasisha wananchi wa Mwanza kuwakamata vijana hao.

Kamanda Kalangi alisema Jeshi la Polisi linafanya kazi kwa mujibu wa sheria za nchi na kusema kuwa kauli za Dk Slaa haziwezi kulilazimisha jeshi lake kufanya kazi kwa matakwa yake.

“Ofisi yangu inafanya kazi yake bila kushurutishwa, mpaka hivi sasa watu 18 wamekwisha kamatwa na kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo ila kuna baadhi ya watu ambao wapo nje kwa dhamana kutokana na kutokuwepo na maelezo ya kujitosheleza,” alisema Kalangi.

Alisema hawezi kuwashikilia watu ambao hawana maelezo yoyote na kinachotakiwa ni wananchi kujitokeza na kuandikisha maelezo ambayo yatawaweka hatiani watuhumiwa.

Katika hatua nyingine: Aliyekuwa mgombea wa udiwani kwa tiketi ya CCM, Jackson Masamaki amesema kwamba ametoa maelezo yake Polisi kuhusiana na tukio hilo la wabunge kukatwa mapanga.

Alisema hakuhusika kabisa na tukio hilo na hawezi kushiriki unyama huo, akitoa mfano wa Mbunge Machemli kwamba ni ndugu yake.
Baba, watoto wadaiwa kuua mama
Jeshi la Polisi mkoani hapa linawashikilia baba na watoto wake wawili wa kiume kwa madai ya kumuua mama yao.

Kamanda Kalangi alidai kuwa mnamo Aprili 24, mwaka huu saa 5:00 usiku katika Kijiji cha Kisesa B, mama huyo, Scolastica Mjangera (58) alikutwa nyumbani kwake akiwa ameuawa baada ya kupigwa na kitu kizito kichwani.

Alisema katika tukio hilo, mume wa marehemu aliyetambuliwa kwa jina la Mgeka Ngapi (75) pamoja na watoto wake wawili John Mgeka (25) na Ndaki Mgeka (18) wanashikiliwa.

Kamanda Kalangi alisema taarifa za awali zinaeleza kuwa kabla ya kifo hicho kulikuwa na mgogoro wa kugawana fedha zilizotokana na kuuzwa kwa shamba la marehemu.

Alisema marehemu aliuza shamba lake kwa Sh5 milioni ambalo linadaiwa kuwa ni la urithi kutoka kwa wazazi wake. Kamanda huyo alidai kwamba baada ya kupokea fedha hizo, aliwagawia kila mmoja kiasi cha Sh200,000 ambazo walizikataa.

Alisema kuwa baada ya kutokea kwa mzozo katika nyumba hiyo, marehemu alitoa taarifa katika ofisi za Serikali ya Kijiji na kabla kuamuliwa kwa ugomvi huo, marehemu akakutwa ameuawa.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Bora wamkamate huyu mpare mwenye asili ya kichaga kwani anataka kuleta machafuko.
KUSHABIKIA CHADEMA NI SAWA NA KUMTUSI MWL NYERERE.
 
Polisi wana test peoples power eeeenh! Waache wajidanganye tuu
 
Back
Top Bottom