Jeshi la police jijini Dar limewakamata vijana 149 Panya road/ Mbwamwitu

Direct impact ya wezi wa tembo kwako ni nini? na Panyaroad wanapopita direct impact kwa mwananchi ni instant.

unazani bila ya hao wezi wa tembo panya road wangekuwepo? kwanza waliokamatwa ni nusu yao jumla wapo 300 think big!
 
Jeshi la polisi kanda maalum ya DSM, limewakamata vijana 155 wanaosadikiwa kuunda kundi la uhalifu lijulikanalo kwa jina la “PANYA ROAD” na kupiga marufuku ngoma za 'VIGODORO” kwa madai kuwa vijana hao hujificha katika ngoma hizo.

Je, unapendekeza "PANYA ROAD"
wapewe adhabu gani ili makundi kama haya yasijitokeze tena?

mbona hawajakamatwa wote jumla wapo 300
 
Serikali yenu sikivu, iko mbioni kuandaa mpango mkakati kuhakikisha vijana wote wanapata ajira, itaboresha maisha ya wazee kwa kuwapa huduma muhimu kama matibabu bure, inampango wa kupanua wigo wa mafunzo ya ufundi ili kila kijana akimaliza shule aweze kujiajiri uchumi wa Tanzania umepanda na kufanya pato la taifa liwe kubwa kwa wastani wa dola 200 kwa mwezi kwa kila mwananchi kidumu Chukua Chako Mapemaaaa!!!!!!
 
Kwa hili Kova na team yako tunakupongeza na tunaomba kundi hilo ibaki historia kama lile la komandoo yoso, hakika kilichokuwa kinafuata ni wanajamii kuanza kuwashughulikia maana wanajulikana wao na wazazi wao.
 
Hao vijana wahukumiwe na wafungwe na wapelekwe gereza la Idete kule kilombero wakalime Mpunga kwa misimu miwili wakirudi watakuwa na adabu
 
hizi ni taarifa nzuri kutoka jeshi la polisi popote tuwaonapo hawa wanaojita watoto wa mbwa tutoe ushirikiano kwa polisi hii itapunguza ualifu ambao unasababisha sisi raia tuishi kwa hofu pamoja na mali zetu tusiishie kuponda kutoa kejeli wakati hv majuzi hapa ndugu zetu jamaa mama zetu wajeruhiwa na kikundi hiki kikatili
 
Wawachome sindano tu za killing me softly, hawana umuhimu wowote wa kutupunguzia oxygen duniani machizi hawa, maisha yenyewe yanabana alafu tunazidi kurudishana nyuma, kama wanapenda wizi si watumie boxer na bunduki wakawaibie waliokwishaiba za epa huko sio wanapiga kabari wauza vitumbua.
 
Wanaosema kova aanze na mafisadi hawakuwai kuwaona hawa watoto wakifanya fujo, mtu unatoka job usiku unaamua kulala guest kwako hapapitiki hawa wahuni wametanda na visu, viwembe,mapanga na nyundo
 
  • Thanks
Reactions: naa
adhabu itolewe kwanza ka mafisadi wa CCM wanaoitafuna nchi,.

Hao watoto hawana makosa maana mfumo mbovu wa CCM hasa katika elimu ndiyo unapelekea mambo kama hayo!!

Hao watoto msiwafanye lolote badala yake muwatafutie mambo ya kufanya ili waweze kujitegemea na kuzisaidia familia zao na hata taifa,...

Kuwapeleka Jela ni uonevu achilia mbali maovu waliyoyafanya,.. Narudia tena kusema uozo wa CCM ndiyo umepelekea haya!!!

Elimu yako haijakukomboa
 
Safi sana jeshi la polisi kwa hatua nzuri, ila tunaomba pia musiwafanye mtaji wa kupatia kitu kidogo kwa kuwakamua viji rushwa na kuwaachia, manake ndiyo hukumu nzuri kwenu, ili wananchi watulie huku nyie mkifaidika na wahalifu hao, na baadaye kupelekea wananchi kufanya mob justice kitu ambacho si kizuri, vijizi vyenyewe vya miaka kati ya ishirini na kumi, naomba mutende haki na haki ionekane ikitendeka.
 
adhabu itolewe kwanza ka mafisadi wa CCM wanaoitafuna nchi,.

Hao watoto hawana makosa maana mfumo mbovu wa CCM hasa katika elimu ndiyo unapelekea mambo kama hayo!!

Hao watoto msiwafanye lolote badala yake muwatafutie mambo ya kufanya ili waweze kujitegemea na kuzisaidia familia zao na hata taifa,...

Kuwapeleka Jela ni uonevu achilia mbali maovu waliyoyafanya,.. Narudia tena kusema uozo wa CCM ndiyo umepelekea haya!!!

usiwe mpuuzi wewe sio kila kitu siasa hata chadema ikingia madarakani matatizo haya yatakuepo japo hapo kwenye kuingia madarakani sina uhakika
basi hata mkeo akifumaniwa uilaumu serikali usiwe mjinga chadema sio mungu na hata wakiingia madarakani hutonufaika na chochote kama sio juhudi zao
 
watoto wajinga hawa waliwai kunizuia juzi kati narudi home na mpenzi wangu eti wameweka barrier bila mtu kutoa buku hupiti ikabidi niwape maana ilikua saa 5 usiku
 
Jeshi la Polisi limesema vigodoro,Kangamoko zimepigwa marufuku na polisi kwa kile kilichoelezwa kuwa sehemu ya uhalifu.
 
Back
Top Bottom