Jeshi la police jijini Dar limewakamata vijana 149 Panya road/ Mbwamwitu

Wanaosema kova aanze na mafisadi hawakuwai kuwaona hawa watoto wakifanya fujo, mtu unatoka job usiku unaamua kulala guest kwako hapapitiki hawa wahuni wametanda na visu, viwembe,mapanga na nyundo
Mkuu, Mimi sijawaona na kutokana niliyoyasikia; sihitaji kukutana nao ili nifahamu udhalimu wao. It is simple common sense kukubali ukweli kuwa hapa polisi wametimiza wajibu wao kwa wananchi wao. Na kwa hili, wanastahili pongezi.
 
wapelekwe kwenye magereza maalum ya kilimo kama songwe mkoani mbeya
 
jana ucku mida ya kama saa sita ucku kuna defender ilikuja mtaani na mama mmoja inasemekana ndie anaewafuga mapanya road kaja na askari kuja kuwapeleka nyumba hadi nyumba wanazoishi watoto panya roa hadi kufikia jana kuna wazaz sita wamekamatwa wawataje watoto hao walipo kimbilia askari wametoa tamko kuwa panyaroad watakamatwa wananch msiwe na matatizo
 
  • Thanks
Reactions: naa
adhabu itolewe kwanza ka mafisadi wa CCM wanaoitafuna nchi,.

Hao watoto hawana makosa maana mfumo mbovu wa CCM hasa katika elimu ndiyo unapelekea mambo kama hayo!!

Hao watoto msiwafanye lolote badala yake muwatafutie mambo ya kufanya ili waweze kujitegemea na kuzisaidia familia zao na hata taifa,...

Kuwapeleka Jela ni uonevu achilia mbali maovu waliyoyafanya,.. Narudia tena kusema uozo wa CCM ndiyo umepelekea haya!!!
Naona wewe unataka kugombea udiwani ndo maana unaharisha jukwaani.
 
Tulipochangia ile thread yenye hiki kisa cha panya road, nafikiri wengi tulisema hawa wahuni watashughulikiwa mapema tu. Huwezi kuwa na organized crime ya wavuta bangi, mateja nk wanakimbiza watu barabarani halafu polisi ishindwe kuwashughulikia mapema. Thanks polisi kwa hilo......

Wamechelewa sana hata hivyo.
Hao vijana 149 hawakuwa formed siku moja na hawakufanya tukio moja, vijana walitakiwa wawe wameshekamatwa tatu tukio la kwanza wakiwa hawajawalisha sumu wenzao na kuongeza idadi hiyo kuwa mara dufu!
 
Hawa vijana wapelekwe kwanza SITAKI SHARI UKONGA wakapatiwe mafunzo ya ukakamavu...

Then wakiiva wapelekwe GEZAULOLE, au KIBUGUMO KWA BW BIRATO na wengine KIMBIJI KWENYE MAKAO MAPYA. Tatizo linakuwa limeisha tunaendelea na ujenzi wa taifa
 
Kwa kweli naingia mashaka sana na chadema! watu wamekatwa mapanga na kuporwa na hao panya road na polisi wamewajibika ipasavyo mnawatetea? nyie ni wezi.
 
Katika siku za hivi karibuni kumeibuka na matukio ya uharifu yanayosadikiwa kuwa yanafanywa na vikundi vinavyojiita panya road,mbwa mwitu nk,hivi ni vikundi vya vijana ambao hawana kazi na wana mahitaji,leo hii wanafanya uharifu randomly lakini hatari ninayoiona ni kua wasipodhibitiwa mapema makundi haya yataimarika yatapata uongozi,yatapata hata sponsors,with no time yatakua km Mungiki-Kenya,Boko haram-Nigeria,who knows may LRA-Uganda.Majukumu ya kuhakikisha kua makundi haya yanatokomezwa ni pamoja na mimi na wewe,kwa kushirikiana na jeshi la polisi,tukileta mchezo hapo baada ya uchaguzi wa 2015 makundi yatakua hatari zaidi,ni muda muafaka sasa vikosi vya inteligensia viingie mtaani.
 
waliwaahidi maisha bora, kwani kungekua na equalization of life haya yangetokea?
 
Usiogope mkuu! Kundi lolote hatari haliwezi kudhibitiwa na polisi, pia ni nadra kuanzishwa katikati ya mji. Hawa ni vijana wanaomkumbusha mkulu ahadi yake ya ajira siju 5M alizojinadi nazo.
 
Hakuna sera endelevu kwa vijana, haya ndio matokeo yake, wengi wamekata tamaa na ahadi hewa wanazopewa na wanasiasa uchwara na sera zisizotekelezeka wapeni hizo bilioni 200 uone ka watasumbua raia mtaani.
 
Jaman ebu tutumie akili kidogo hawa vijana wanawadhuru walala hoi wenzao ndo maana tunawalaani asilimia zote.lakin mafisadi hawaji kupora simu yako wala bodaboda yako.siwatetei mafisadi!
 
Nimepata taarifa muda huu, hawa vijana wanaojiita panyaroad au mbwamwitu mida hii wanatesa mitaa ya Kinyerezi utadhani nchi hii haina vyombo vya dola, Kova maneno ya bure tu, serikali kweli inaweza kuzidiwa na vijana kama hawa kiasi watambe kiasi hiki tena mchana kweupee.

Anyway tuyaache ya serikali, naomba niwakaribishe kitunda hawa vijana tuwaoneshe kazi, si serikali imewashindwa.
 
Back
Top Bottom