Jeshi la police jijini Dar limewakamata vijana 149 Panya road/ Mbwamwitu

MstahikiMeya

JF-Expert Member
Jan 8, 2014
1,654
0
Jeshi la polisi kanda maalum ya DSM, limewakamata vijana 155 wanaosadikiwa kuunda kundi la uhalifu lijulikanalo kwa jina la "PANYA ROAD" na kupiga marufuku ngoma za 'VIGODORO" kwa madai kuwa vijana hao hujificha katika ngoma hizo.

Je, unapendekeza "PANYA ROAD"
wapewe adhabu gani ili makundi kama haya yasijitokeze tena?

==========

Akinukuliwa na radio wapo jijini Dar es salaam, kamanda Kova amesema wamefanikiwa kuwakamata vijana 149, wanaojihusisha na matukio ya kiharifu jijini Dar es salaam, vijana hawa wanatoka katika makundi mbalimbali yakiwemo Mbwamwitu na lile la Panyaroad.
 
fiter

JF-Expert Member
Dec 3, 2013
1,148
0
Jeshi la polisi kanda maalum ya DSM, limewakamata vijana 155 wanaosadikiwa kuunda kundi la uhalifu lijulikanalo kwa jina la “PANYA ROAD” na kupiga marufuku ngoma za 'VIGODORO” kwa madai kuwa vijana hao hujificha katika ngoma hizo.

Je, unapendekeza "PANYA ROAD"
wapewe adhabu gani ili makundi kama haya yasijitokeze tena?

kutatokea makundi mengine tu si mliwaahdi maisha bora?
 
chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
18,736
2,000
adhabu itolewe kwanza ka mafisadi wa CCM wanaoitafuna nchi,.

Hao watoto hawana makosa maana mfumo mbovu wa CCM hasa katika elimu ndiyo unapelekea mambo kama hayo!!

Hao watoto msiwafanye lolote badala yake muwatafutie mambo ya kufanya ili waweze kujitegemea na kuzisaidia familia zao na hata taifa,...

Kuwapeleka Jela ni uonevu achilia mbali maovu waliyoyafanya,.. Narudia tena kusema uozo wa CCM ndiyo umepelekea haya!!!
 
bysange

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
4,432
2,000
nawapongeza polisi kwa hilo ila bado tatizo ni kubwa sababu kuna wengine watajitokeza chanzo cha tatizo ndio kitafutwe na kupatiwa ufumbuzi.
 
Marire

JF-Expert Member
May 1, 2012
12,045
2,000
adhabu itolewe kwanza ka mafisadi wa CCM wanaoitafuna nchi,.

Hao watoto hawana makosa maana mfumo mbovu wa CCM katika elimu ndiyo unapelekea mambo kama hayo!!

Hao watoto msiwafanye lolote,...

naunga hoja mkono ila hiyo ya mwisho toa
 
twijuke

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
548
500
Akinukuliwa na radio wapo jijini Dar es salaam, kamanda Kova amesema wamefanikiwa kuwakamata vijana 149, wanaojihusisha na matukio ya kiharifu jijini Dar es salaam, vijana hawa wanatoka katika makundi mbalimbali yakiwemo Mbwamwitu na lile la Panyaroad.
 
Kwetunikwetu

JF-Expert Member
Dec 23, 2007
1,540
1,225
Akinukuliwa na radio wapo jijini Dar es salaam, kamanda Kova amesema wamefanikiwa kuwakamata vijana 149, wanaojihusisha na matukio ya kiharifu jijini Dar es salaam, vijana hawa wanatoka katika makundi mbalimbali yakiwemo Mbwamwitu na lile la Panyaroad.

Tulipochangia ile thread yenye hiki kisa cha panya road, nafikiri wengi tulisema hawa wahuni watashughulikiwa mapema tu. Huwezi kuwa na organized crime ya wavuta bangi, mateja nk wanakimbiza watu barabarani halafu polisi ishindwe kuwashughulikia mapema. Thanks polisi kwa hilo......
 
RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
40,646
2,000
wa.pu.zi wakubwa hawana lolote kujisifia watupe feedback ya wizi wa meno ya tembo na rasirimali zetu zingne

nyinyi watu mna matatizo sana. juzi tu hapa hawa vijana wameleta fujo mkaanza kusema polisi wako wapi!!! leo wanatangaza kukamata hao vijana mnaanza kuleta habari nyingine eti waanze na mafisadi na wewe sasa unataka feedback ya meno ya tembo!!! hivi hamna jema??? kila kitu kulaumu tu mmezidi. ndio mnafanya JF ionekane sehemu ya porojo na majungu tu.
 
Leomimi

JF-Expert Member
May 20, 2013
2,548
1,750
Mibongo kama papa likiwa baharini litakula watu likitolewa nchi kavu litanuka
nyinyi watu mna matatizo sana. juzi tu hapa hawa vijana wameleta fujo mkaanza kusema polisi wako wapi!!! leo wanatangaza kukamata hao vijana mnaanza kuleta habari nyingine eti waanze na mafisadi na wewe sasa unataka feedback ya meno ya tembo!!! hivi hamna jema??? kila kitu kulaumu tu mmezidi. ndio mnafanya JF ionekane sehemu ya porojo na majungu tu.
 
SoNotorious

JF-Expert Member
Sep 11, 2011
2,422
1,195
Kama hatutajenga utamaduni wa kuappreciate mambo madogo, hata kama mabillion ya uswizi yakiletwa tutasema mbona chenji ya rada hatujaiona. Nashukuru jeshi la police dsm kwa kazi nzuri.

Kazi ya meno ya tembo ma rasilimali haiko chini ya kova, ni taifa zima.

Hatuwezi kuwapongeza kwa kutegua bomu walilotega wenyewe, think twice biaach.
 
Mlaleo

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
11,270
2,000
zomba nasikia naye alikuwemo nadhani hatutamuona kwa muda mrefu kuanzia sasa
 
Last edited by a moderator:

Sista

JF-Expert Member
Sep 29, 2013
3,210
2,000
Hawa vijana wapewe adhabu kali sana imeniuma kusikia pamoja na kufanya uharifu wamewabaka wana kike wadogo na watu wazima
 
JPN

Senior Member
Jul 28, 2013
119
225
Nawaliofirisi mali za umma watakamatwa au ndio mapapa na vidagaa hapa inadhihirisha.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom