Jeshi la Mali kusimamia Serikali ya mpito ya miezi 18

Shadida Salum

Journalist at JamiiForums
Sep 11, 2020
69
104
Serikali ya kijeshi ya mali imelazimishwa na mkataba wa kisiasa kuanzisha serikali ya mpito ya miezi 18 ambayo inaweza kupelekea kuteuliwa kwa mwanajeshi kama Rais wa mpito , licha ya mapingamizi kutoka kwenye muungano uliofanya maandamano ya kuipinga serikali kabla ya mapinduzi ya kijeshi.

Kuidhinishwa kwa ramani ya barabara, ilimaanisha kuweka ramani ya muelekeo wa nchi hiyo tangu mapinduzi ya tarehe 18 mwezi wa nane 2020, ambayo yalimuondoa madarakani Rais Ibrahim Boubacar Keita.

Makubaliano hayo yaliafikiwa Jumamosi ya Septemba 12 ,2020 baada ya mapatano ya siku 3 kati ya serikali ya kijeshi, viongozi wa kisiasa na jumuia za kiraia.

Mkataba unasema kuwa Rais anaweza kuwa raia au mwanajeshi na ataiongoza serikali ya mpito kwa kipindi cha miezi 18 kabla ya kuitishwa kwa uchaguzi, alisema Moussa Camara msemaji wa mapatano hayo.

“Rais wa mpito atachaguliwa na wachaguaji waliowekwa na serikali ya kijeshi,” aliongeza Camara.

Rasimu ya awali ya mkataba huo ilisema serikali ya mpito ingedumu kwa kipindi cha miaka 2 na Rais wa mpito angechaguliwa moja kwa moja na viongozi wa kijeshi, Kamati ya Taifa ya Uokozi wa Watu (CNSP).

“Tunajitoa mbele yenu kuongeza jitihada za makusudi katika utekelezaji wa haya masuluhisho kwa shauku ya watu wa Mali,” Rais wa CNSP Assimi Goita alisema Jumamosi ya Septemba 12,2020.

Ripota wa Aljazeera Ahmed Idris aliye Abuja, Nigeria amesema kuwa vikwazo vinahitaji kuondolewa nchini Mali kwakua inakumbana na matatizo ya kiuchumi na kijamii.

“Na watu watakua wakiangalia vipi serikali mpya ya mpito itashughulikia swala la ulinzi ambalo limekua tishio si kwa makundi yenye silaha ya Kaskazini, lakini pia na machafuko ya kikabila kati ya wafugaji na wakulima, “ alisema Ahmed.

Raia 6 akiwemo mwanamke mjamzito, waliuawa Kusini mwa nchi hiyo wakati gari ya kusafirishia wagonjwa waliyokuwamo kukumbana na mabomu ya kutegwa ardhini, waziri wa afya alisema.

Idris aliongeza kuwa makubaliano ya Jumamosi yalikua dhaifu na mwitiko wa watu wa Mali ni wa umuhimu.

Mali military backs 18-month transition government as talks close
 
Mali Iko MSAMBWENI....

Matukio Ya Jeshi Kupindua Si Mapya.....

Kule Viongozi Wa DINI Wana USHAWISHI MKUBWA mno,kiasi kwamba hata Jeshi Na Wengineo WANAWATII..

Ikumbukwe Pia UTAWALA Wa KIDEMOKRASIA ni Suala gumu bado(si tu Mali Bali Afrika Nzima).

Wako Waafrika Wanaooupinga UTAWALA WA DEMOKRASIA kwa kuainisha VISINGIZIO LUKUKI,kuwa hauendani na SISI...😁😁😁

Ajabu kubwa ni kuwa,kwa jinsi TEKNOLOJIA inavyokuwa,mfano MITANDAO ya kijamii....Basi ni UJUHA wa kunidanganya pakubwa kuwa AFRIKA ITAFUTE MFUMO MWINGINE BORA kiutawala...

Walio na MAWAZO hayo muflisi,watabaki kuwa nyuma ya wakati......na wakati utakuwa ni KATILI kwao....

Kule kaskazini Mwa Mali,Tuareg na wenzao Wameamua kuutafuta UTAMBULISHO WAO kwa njia yoyote wanayoona "inafaa"...

Kiukweli Mali Ina Safari Ndefu Mno,na ninaifananisha japo si kwa Sana na mgogoro wa Morocco na Sahrawi.....

Time will tell
 
Kwahiyo tuareg wanataka kujitenga?
 
Back
Top Bottom