Huyu Kijana alikuwa Jasiri sana,Kabla ya 2010.Enzi hizo anatembea na Camera za kidukuzi pamoja na pingu.
Nguvu ya Dume la Ng'imbe (Bull) Ziko dhahiri popote pale utaona vurugu,machachari na umahiri wa kupiga kwake Bull wakati bado Halija HASIWA.
Mara tu likigongowa zile kede zake baaasi hata mulio hubadilika na kuwa sio wa yule Dume tuliomzoea huegeuka na kuanza kutoa mulio kaa wa Ndama au Ngo'mbe Jike.Mara moja hata Jina lake hubadilika na kuanza kuitwa MAKISAI.
JERRY MURO! JERRY MURO! JERRY MURO!
Uko Wapi? Hio kashfa ya kupokea Rushwa ilikuwa ya kweli?
Au wana siasa waliwahi kuku-Mute ili usiwaletee Madhara kwenye kampeni za 2010.
Ulikuwa POSTIVE/CHANYA (+) ghafla umegeuzwa na umekubaliana na hio hali ya KUHASIWA.Kuwa NEGATIVE/HASI (-).
Hivyo vipindi vyako vya PPRA vinakufaa kwa Ajili ya tumbo lako tu.Umeacha wito wako halisi ambao ni WAKUJIHATARISHA KWA MASLAHI YA UMMA WA WATANZANIA.
Umeacha,ukasahau tena umeifukia chini Talanta yako,2015 RUDI KWENYE NAFASI YAKO.
TAIFA LINAKUHITAJI.
NAWASILISHA JAMII IJUE.
Sasa hivi ni afisa habari wa yanga
Nilikutana nae siku moja pale Mlimani City akiwa anapaki ki-corona chake. Tukaongea kwa kifupi sana lakini kikubwa ni nia yake ya kugombea ubunge huko kwao kwa tiketi ya moja ya vyama vya ukawa.
Jerry Muro alikata tamaa mapema mno. Wakristu husema "majaribu ndo mtaji wa Imani".
Majaribu ya Jerry ndo ulikuwa mtaji wake wa kusonga mbele na kuwa na jina kubwa katika nchi na nje ya nchi. Lakini yeye kaamua kupokea mtaji na kuutia kwenye kibuyu mvunguni.
Hebu aone kazi nzuri za investigative journalist Mohammed Ali wa NTV ya kenya. ( JICHO PEVU: Makri ya Injili: http://youtu.be/mSi5UHlDOCA) .
We need him to get inspired and kick off again. Aache uoga.
Hebu Tuache Dharau Kwani Alichokupa Wewe Yeye Kamnyima Na Kuna Tunu Pengine Muro Anayo Na Wewe Pamoja Na Utajiri Wako Huo Wa Vipesa Vya Ngama Huna! ktk Maisha Yangu HUWA NACHUKIA MNO na SANA WATU WENYE DHARAU KAMA Wewe. Na Si Ajabu Ukawa Huna CHOCHOTE Kuanzia Akili Na Mali. Nimechukizwa Na Sentensi Yako Kuwa Nimemkuta Na Ki Korona Chake..........Umeniboa Na Umenikera Mkuu Na Hongera Zako Wewe Uliyebarikiwa Kuwa Na Magari Makuu Kuu.