Maajabu: Baada ya Shule kupewa jina la Mrisho Gambo, Jerry Muro naye atamani Shule iitwe jina lake

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
Heshima kwenu wakuu,

Mkuu wa Mkoa kafanya mambo mengi ya Maendeleo Arusha. Je, hicho ni kigezo tosha cha yeye kupewa Shule yenye jina lake.
IMG_20200117_121417.jpg

Katika uzinduzi wa Shule ya Sekondari Mrisho Gambo Olasiti Arusha, Waziri wa Elimu Prof. Joyce Ndalichako ameupongeza Mkoa wa Arusha kwa kuhakikisha hakuna mtoto atakaye baki nyumbani kwa kukosa nafasi kidato cha kwanza.

Nampongeza kwa Hatua hiyo kama kweli Gambo kajiona viatu vya kupewa jina la Shule vinamtosha na kama kweli kwa aliyotenda anaona anastahili.

Kwa Utashi, umoja uwajibikaji na Uongozi wa Watanzania, huu ni wakati sahihi wa kupewa shule yenye jina lake sehemu anayoongoza?

Je, ni faida ya kuwa kiongozi wa awamu ya tano ambayo kila mteule kuamua atakalo?

Je hii ni mila na desturi ya Uongozi wetu?

Ni vigezo gani vimetumika?

Je, Watendaji hawajashinikizwa kufanya hivyo?

Kwa upande wangu naichukulia kama kwenye Daladala mtoto amekalia kiti huku babu yake au Mama Mjamzito kasimama.

Hali hii imefanya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro naye kutamani apewe jina la Shule yoyote Arumeru. Dunia ina mambo.

Ni maoni yako?

Mrisho Gambo alizaliwa Mei 22, mwaka 1982 katika Hospitali ya Ocean Road ya Dar es Salaam.

Alipata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Ilala Boma na kuhitimu darasa la saba mwaka 1997 na kupata bahati ya kuchaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari kidato cha kwanza hadi cha nne, katika Shule ya Sekondari Kibaha na kuhitimu kidato cha nne mwaka 2001.

Mwaka 2002 alichaguliwa kujiunga kidato cha tano Shule ya Ufundi Tanga, maarufu kama Tanga Technical School. Alihitimu kidato cha sita mwaka 2004.

Mwaka 2005 alichaguliwa kujiunga na elimu ya juu, katika Chuo cha Uhasibu Arusha, kusomea stashahada ya juu katika Sayansi ya Kompyuta (computer science) na kuhitimu mwaka 2008.

Mwaka 2009 aliajiriwa kwa nafasi ya mchambuzi wa mifumo ya kompyuta katika Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Mwaka 2011, aliajiriwa kama msimamizi mwandamizi wa mifumo ya kompyuta wa Chuo cha Kimataifa cha Nelson Mandela.

Mwaka 2011 alijiuzulu nafasi hiyo pale Chuo cha Nelson Mandela na kurudi Jiji la Arusha. Aliweza kurudi Jiji la Arusha kwa kuwa hakuwa ameacha kazi, bali aliomba likizo bila malipo.

Mwaka 2010 alijiunga tena Chuo cha Uhasibu Arusha kusoma shahada ya uzamili (masters degree) katika masuala ya uongozi na teknolojia ya habari na kuhitimu mwaka 2011.

April 2012 aligombea ubunge wa Afrika Mashariki na kushika nafasi ya sita kati ya watu 81 waliogombea.

May 2012 aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe.

Julai 2016 aliapa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha nafasi aliyokuwa akiishikilia hadi leo alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Agosti 18, 2016 aluteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha akichukua nafasi ya Felix Kijiko Ntibenda.
 
Achievement gani na wewe!!

mkuu, umeelewa comment yangu ?
nilichomaanisha ni kwamba, tuseme wewe ni mkuu wa mkoa hapo ulipo, ukafanya shughuli za maendeleo , ukiwa kijana, hiyo haiuzuii sisi kuita shule jina lako eti kwa sababu una safari ndefu mfano kuja kuwa teja nk

hoja yangu ni kwamba, sio lazima mpaka mtu afe ndio mchango wake utajwe (mtu yeyote)
jaribu kuekewa comment yangu haipo kiushabiki kama ulivyodhani


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye CV ya Gambo hujaonesha alipofukuzwa U DC Korogwe kisa kumwambia Mwanasheria wa wilaya ana Degree ya CHUPI. Alisota mtaani hadi baadae Kikwete akamuonea huruma na kumteua DC wilaya moja kule Kigoma, jina sikumbuki. Ilikuwa ni nguvu ya Tume ya maadili ya viongozi wa umma ilishinikiza kufukuzwa U DC na ilimwiita kumhoji Dar es salaam.

Aligoma kwenda hadi tume iliposhinikiza kumpeleka kwa pingu na polisi waliojihami kwa silaa ndipo akatinga kuhojiwa kwa kumtusi Mrembo mwanasheria. Ikumbukwe JK hakupenda kufukuza watu hovyohovyo.
 
Itakapo toa zero za kutosha na kushika mkia asije kutaka kubadili jina, kwa kupewa heshima hiyo ahakikishe shule inakuwa na ufaulu bora na mahitaji ya shule yanapatikana. Sio ipewe jina akeche cheke halafu awaachie wananchi jengo na wanafunzi bila mahitaji muhimu.
 
Back
Top Bottom