Jerry Muro afungiwa kujihusisha na soka kwa Mwaka mmoja!!

=========

KAMATI YA MAADILI TFF YAMPIGA PINI JERRY MURO, KUTOJISHUGHULISHA NA MASWALA YA SOKA KWA MWAKA MMOJA
jerry-muro.jpg

MKUU wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga, Jerry Muro (pichani)

amefungiwa mwaka mmoja kujihusisha na masuala ya soka pamoja na kutozwa faini ya Sh. Milioni 3, baada ya kikao cha Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kilichokaa leo kwenye Makao Makuu ya Shirikisho hilo, chini ya Mwenyekiti wake, Wakili Wilson Ogunde

Muro amefungiwa baada ya kukutwa na hatia katika mashitaka mawili kati ya matatu yaliyowasilishwa na TFF mbele ya Kamati ya hiyo, ambayo ni kudharau maamuzi ya Kamati ya Nidhamu ya TFF mwaka 2015 alipotakiwa kulipa faini ya Sh. Milioni 5 baada ya kufanya makosa, lakini amekaidi kulipa hadi leo, akahukumiwa kutengana na kutojihusisha na masuala ya soka kwa mwaka mmoja, wakati shitaka lingine ni kuchochea vurugu na kuhatarisha amani kuelekea mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho kati ya Yanga na TP Mazembe ya DRC.

Katika shitaka hilo, Jerry alidaiwa kuwashawishi mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao na kutowapa nafasi watani wao wa jadi (Simba) kuingia kwenye mchezo huo ambao timu yake ilifungwa bao 1-0 na Mazembe Juni 28, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Hata hivyo, Jerry Muro alifanikiwa kuishinda TFF katika shitaka la kupingana na maamuzi ya shirikisho hilo juu ya masuala ya utoaji wa haki za matangazo ya Televisheni.

“Kamati ilisikiliza kwa makini taarifa zake alipokuwa anazungumza na vituo vya Redio na kugundua alikuwa sahihi, hivyo hapa hana hatia,”kimesema chanzo.Hata hivyo, Jerry Muro amehukumiwa wakati mwenyewe hakuwepo kwenye kikao na inadaiwa hakutoa taarifa ya maandishi juu ya kutohudhuria kwake.

Badala yake, imeelezwa Katibu wa Yanga, Baraka Deusdedit alifika mapema leo kabla ya kikao kwa ajili ya kutoa taarifa ya mdomo kwamba Muro amekwenda kwao Kilimanjaro kusafisha makaburi ya wazee wake.

Lakini Kamati ikaamua kuendelea na kikao kwa mujibu wa kanuni na hatimaye kuchukua hatua ilizochukua. Hata hivyo, Muro ana haki ya kukata rufaa Kamati ya Rufaa ya TFF.

akimaliza hio adhabu tutamrejesha kwe nafas yake
 
Kuhamasisha mashabiki wa Yanga waje kwa wingi uwanjani na kuwanyima nafasi Simba!!? Sijaelewa hapo
 
Kwa wakati huu Jerry anaposhughulikia rufaa yake, Masao Bwire atakaimu kwa muda. Wembe ule ule
 
Tatizo lako ni: (1) kuamini kwamba mimi ni Jerry Muro kwa sababu tu nimeelezea udhafu wa hukumu dhidi yake. Nakusikitikia kwa kupoteza muda na matusi yako dhidi ya unauemdhani kuwa ndiye JM. Pole sana. (2) Unadhani mwenye haki ya kutukana wenzake ni wewe tu kama ulivyofanya hapo juu kumtukana unayemdhani ni JM. Kama wewe una haki hiyo, kwa nini naye asiwe nayo, iwapo kweli alitukana? Pole sana. (3) Kukurupuka kumtukana mtu kwa dhana tu kwamba ndiye hasa unayemchukia kwa sababu tu hupendezwi na kauli zake ni kiashirio cha vyote, ukosefu wa adabu uliokithiri na umbumbumbu uliotopea. Pole sana.
Ushauri wangu kwako ni uleule wa awali, kwamba kila mtu ana haki ya kutoa mawazo yake madhali havunji Katiba wala Sheria. Aidha, weledi ni pamoja na kuwastahamilia wanaojaribu kuwasilisha mawazo yao lakini wakateleza katika kujieleza kwao. Ndio maana ninaheshimu matusi yako kwangu. Ila ni vyema ukaelewa kwamba si kila mtu ni mstahamilivu kama mimi, unaweza ukan'gatwa na Sheria ya Makosa ya Kimtandao na ukajikuta umetumikia kifungo cha Dola, siyo cha kamba ya mgomba cha TFF unachokifurahia kwa Jerry Muro unayemdhani kuwa ni mimi.

....ondoa mashairi yako hapa,huu ushauri wako ungempa huyo muro unaemtetea ningekuona wa maana zaidi.Inshort, muro ni mhuni anastahili adhabu full stop!,mlimuendekeza sasa yamemkuta unanza kuleta analysis hapa!,kamtetee mahakamani,hop unapendezwa sn na ule mdomo wake! (hilo jina sijaanza kwa herufi kubwa kwa sababu maalum!)
 
Nashukuru umeelewa kwamba mimi siyo Muro. Hongera. Usijionee haya kwa utumbo wako wa awali kuwavaa watu kwa dhana. Lichukulie kuwa ni funzo kwako, kama utakuwa na akili ya kujifunza. Najua umesema 'full stop' kwa maana ya kuwa huhitaji tena mjadala nami. Nami kwako nasema sitaendeleza mjadala nawe kwa hili. Full stop.
 
Well said mkuu..
Mpka nmejiulza io kamat ilyotoa hukumu ni wanafunzi wa primary au watu wazma
Exactly. Wanashindwa hata kuelewa kwamba Muro ni mwajiriwa wa Yanga na kwa hivyo waitake Yanga iliyo mwanachama wao TFF ndiyo imfungie msemaji wake. Hata hilo hawalijui basi? Kusoma hawajui, basi hata picha hawaoni?
 
Ingawa mimi ni shabiki na mwanachama wa Msimbazi, ila kuna sehemu hawa wakubwa wameteleza, hasa hili la kukosa kujitetea mbele ya kamati baada ya kutopata wito wa kuitwa. Wakubwa wameteleza!

Kutokuhudhuria mbele ya kamati kwa visingizio vya kitoto hakuwezi kukufanya uepuke adhabu. Alishapata wito, alipaswa kwenda kujitetea
 
Exactly. Wanashindwa hata kuelewa kwamba Muro ni mwajiriwa wa Yanga na kwa hivyo waitake Yanga iliyo mwanachama wao TFF ndiyo imfungie msemaji wake. Hata hilo hawalijui basi? Kusoma hawajui, basi hata picha hawaoni?

Hivi sheria au hizi kanuni unazipata wapi? Kosa linaweza kuwa la mtu mmoja mmoja au taasisi, au vyote. Hebu pitia tena details za shauri la Muro halafu ndio ulete analysis zako. Adhabu anapewa menda kosa na sio familia yake au taasisi anayofanyia kazi
 
Ingawa mimi ni shabiki na mwanachama wa Msimbazi, ila kuna sehemu hawa wakubwa wameteleza, hasa hili la kukosa kujitetea mbele ya kamati baada ya kutopata wito wa kuitwa. Wakubwa wameteleza!

Hili la Muro kutopata wito wa kamati una uhakika nalo au ni dhanio lako tu? Huoni kama Katbu wa Yanga alihudhuria kikao kutoa udhuru wa mdomo kuhusu Muro kwenda Moshi kwa mambo yake binafsi? Someni vzr details za shauri kabla hamjatafuta pa kuchomokea
 
Sio mimi niliyechomeka, ni Jerry Muro!
 
Hivi sheria au hizi kanuni unazipata wapi? Kosa linaweza kuwa la mtu mmoja mmoja au taasisi, au vyote. Hebu pitia tena details za shauri la Muro halafu ndio ulete analysis zako. Adhabu anapewa menda kosa na sio familia yake au taasisi anayofanyia kazi
Adhabu na kosa unalozungumzia wewe ni la makosa ya jinai ambayo msikilizaji na anayehukumu ni Mahakama pekee. Hili la Muro ni swala la nidhamu (disciplinary matter) baina ya mkubwa na aliye chini yake (boss and his subordinate). Unapochelewa kwenda kazini, mwajiri anaweza kukukata mshahara bila ya kupitia mahkamani kwa sababu ni swala lililo ndani ya mkataba wa ajira yako. Yanga ikiruka ukuta kuingia uwanjani itaadhibiwa na TFF bila ya kupitia mahkamani kwa sababu nidhamu ya kuingia uwanjani ni sehemu ya makubaliano baina ya Yanga na TFF ndani ya kanuni za kuendesha Ligi. Niambie Muro ana uhusiano gani wa moja kwa moja na TFF au kuna makubaliano gani ya moja kwa moja baina ya Muro na TFF bila ya kupitia Yanga iliyomwajiri ambayo ndiyo ina makubaliano yenye mashiko na TFF? Umeona wapi baba mkwe akatoa talaka kwa mke wa mwanawe?
 
Back
Top Bottom