Jerry Muro afungiwa kujihusisha na soka kwa Mwaka mmoja!!

Wonderful

JF-Expert Member
Apr 8, 2015
7,347
5,984
=========

KAMATI YA MAADILI TFF YAMPIGA PINI JERRY MURO, KUTOJISHUGHULISHA NA MASWALA YA SOKA KWA MWAKA MMOJA
jerry-muro.jpg

MKUU wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga, Jerry Muro (pichani)

amefungiwa mwaka mmoja kujihusisha na masuala ya soka pamoja na kutozwa faini ya Sh. Milioni 3, baada ya kikao cha Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kilichokaa leo kwenye Makao Makuu ya Shirikisho hilo, chini ya Mwenyekiti wake, Wakili Wilson Ogunde

Muro amefungiwa baada ya kukutwa na hatia katika mashitaka mawili kati ya matatu yaliyowasilishwa na TFF mbele ya Kamati ya hiyo, ambayo ni kudharau maamuzi ya Kamati ya Nidhamu ya TFF mwaka 2015 alipotakiwa kulipa faini ya Sh. Milioni 5 baada ya kufanya makosa, lakini amekaidi kulipa hadi leo, akahukumiwa kutengana na kutojihusisha na masuala ya soka kwa mwaka mmoja, wakati shitaka lingine ni kuchochea vurugu na kuhatarisha amani kuelekea mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho kati ya Yanga na TP Mazembe ya DRC.

Katika shitaka hilo, Jerry alidaiwa kuwashawishi mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao na kutowapa nafasi watani wao wa jadi (Simba) kuingia kwenye mchezo huo ambao timu yake ilifungwa bao 1-0 na Mazembe Juni 28, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Hata hivyo, Jerry Muro alifanikiwa kuishinda TFF katika shitaka la kupingana na maamuzi ya shirikisho hilo juu ya masuala ya utoaji wa haki za matangazo ya Televisheni.

“Kamati ilisikiliza kwa makini taarifa zake alipokuwa anazungumza na vituo vya Redio na kugundua alikuwa sahihi, hivyo hapa hana hatia,”kimesema chanzo.Hata hivyo, Jerry Muro amehukumiwa wakati mwenyewe hakuwepo kwenye kikao na inadaiwa hakutoa taarifa ya maandishi juu ya kutohudhuria kwake.

Badala yake, imeelezwa Katibu wa Yanga, Baraka Deusdedit alifika mapema leo kabla ya kikao kwa ajili ya kutoa taarifa ya mdomo kwamba Muro amekwenda kwao Kilimanjaro kusafisha makaburi ya wazee wake.

Lakini Kamati ikaamua kuendelea na kikao kwa mujibu wa kanuni na hatimaye kuchukua hatua ilizochukua. Hata hivyo, Muro ana haki ya kukata rufaa Kamati ya Rufaa ya TFF.
 
kwani ile kamati si iliitupa ile barua ya tff.

ngoja nisubiri hadi mwisho.
 
Mimi ni yanga damu ila huyu jamaa anatafutaga sifa ya kugombea udiwani
Kitanzi ama pingu hizi nahisi ni za kamba ya mgomba kwa sababu:
(1) Kosa la kwanza alilotiwa nalo hatiani ni kukaidi kulipa faini ya Shilingi milioni tano aliyopigwa mwanzoni. Kuna tata mbili kwenye hukumu hii. Kwanza ni kauli iliyotolewa majuzi na Manji kwamba hela hiyo imeshalipwa. Licha ya ufahamu mdogo anaotuhumiwa kuwa nao, Manji asingethubutu kusema hadharani jambo lililo rahisi kuthibitisha kama la mtu kulipa ama kutokulipa. Kimbuka ameweza kuthibitisha yaliyo magumu kuliko hayo. Ukisoma baina ya mistari, utaona utata uliopo kuhusu malipo haya ni kupokelewa ama kutopokelewa na TFF, lakini sio kutowasilishwa. Utata wa pili wa hukumu hii ni ile kanuni ya msingi ihusuyo madeni, kwamba mtu hafungwi kwa deni. Laiti tungepata kuisikia TFF ikikimbusha na kusistiza mapema kwamba mtuhumiwa hajalipa deni hilo na akapewa muda wa kuwa amelilipa, ni kioja kuliibua shtaka hilo na hatimaye kulitumia kumtia mshtakiwa hatiani.
(2) Kosa la pili alilohukumiwa ni la kushawishi wapenzi wa Yanga kufanya fujo kwa kauli yake kwamba kwenye mechi dhidi ya Mazembe Wanasimba wasiruhusiwe kukaa 'Jukwaa la Simba' kwa sababu mechi imelipiwa na Yanga. Hapa pia kuna tata kadhaa za kisheria, iwapo Kamati iliyotoa hukumu hiyo ilitakiwa kutoa hukumu kisheria. Kwanza ni kwamba bila ya kupata kauli ya mhusika kufafanua alichomaanisha, maoni ya Kamati kwamba kauli hiyo ni kuchochea fujo inabaki kuwa ni tafsiri yao tu. Sababu kwamba alidharau wito (Kama kweli lilofanyika) haina mashiko kwenye hoja hii kwa sababu msingi wa shtaka hili ni kujua nini mshtakiwa alimaanisha kwa kauli anayodaiwa kuitoa. Kumbuka kwamba hata TFF haijawqchukulia hatua wanaodaiwa kupanga matokeo ya fainali Ligi Daraja la Kwanza wala ile ya wanaosemekana kupanga njama za kumziwia Manji asigombee Uenyekiti wa Yanga, zilizonaswa kwenye mawasiliano ya simu. Ni kwa sababu ya msingi kwamba bila ya kuthibitishwa kwamba kilichosemwa ndicho kilichokusudiwa, kuna hatari ya kutafsiri kauli ya mtu nje ya muktadha (out of context). Akiwa Naibu Waziri Mkuu, Mrema aliwahi kuwahimiza Wazanzibari kwenye mkutano wake mmoja wa hadhara kwamba 'wauze hata miili yao' katika kutetea Muungano na Mapinduzi. Je, Mchaga huyu alikuwa ahukumiwe kwa kushajiisha uzalendo wa hadhira yake kupitia umalaya? Huenda namna hiyo pia ndivyo Kamati hii ya TFF inavyomhukumu Mchaga Muro kwa kutafsiri kauli yake neno kwa neno! Lakini utata wa pili wa kisheria kwenye hukumu hii ya kuchochea fujo ni tafsiri ya 'Jukwaa la Simba'. Ni kwenye sheria, kanuni, tamko au andiko gani rasmi kisheria ilipoazimiwa kwamba jukwaa hilo ni lazima likaliwe na Wanasimba tu au lile 'la Kijani' ni lazima likaliwe na Wanayanga tu? Hivi kutoruhusu mtu kufanya jambo ni lazima iwe kwa fujo pekee, hasa kwenye muktadha wa kuhamasisha jamii? Hivi Chama A cha siasa kinapowataka wanachama wake wasiruhusu wapinzani wao kuirudisha nchi nyuma, wanahamasisha fujo? Kwani haiwezekani Muro alikusudia kwamba wanachama wake wasiwaruhusu Wanasimba kukaa 'Jukwaa la Simba' kwa wao Yanga kutangulia kulijaza kabla Simba hawajafika, hasa kwa sababu hakuna sheria, kanuni wala tamko lolote rasmi kisheria linalolazimisha Wapenzi wa Simba tu kukaa jukwaa hilo?
Udhaifu huu mkubwa kwenye hukumu ya Kamati hii ndio unaonifanya nimwone Muro amefungiwa kwa kamba ya mgomba. Kamati yoyote making ya rufaa ya TFF haitaichukua sekunde sitini kutengua hukumu hii iliyoitishwa na Mahakama ya Kangaroo (Kangaroo Court) ya TFF. Labda na Kamati hiyo ya rufaa nayo iwe ya Kangaroo pia! Ila mpaka kufikia kwenye Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo, kangaroo wote watakuwa wametoweka!
Najua nimewakwaza wale wote ambao kwa sababu zao binafsi wanamchukia Muro kutokana na matamshi yake yanayoonekana kuwaudhi. Ili kujipunguzia machungu, naomba wazichukulie kauli za aina hii kuwa ni za kawaida na za kutegemewa hata kama hatimaye hukumu ya Muro itasimama na hata Kama Yanga itakatazwa kuwa na msemaji mwemgine. Kwa utamaduni wa soka la Kitanzania sambamba na utani wa jadi unaokaribia kuwa uhasama wakati wa usajili na wa mechi baina yao, atatokea Muro mwengine tu kama atavyotokea Manara mwengine baada ya huyu ndani ya Simba. Kadhalika akina Kifaru, Bwire na wengineo. Wakwazika hawa wa kauli za Muro, Manara, Kifaru, Bwire na wasemaji wa timu nyengine wakumbuke kwamba hata kama kauli hizo zitawaudhi, wasemaji hao wana haki nazo Kikatiba, kisheria na kikanuni madhali hawatavunja sheria za nchi - bila ya kujali iwapo TFF itapendezewa nazo ama la! TFF na Kamati zake haina uwezo kikatiba kumziwia mtu yeyote kutoa mawazo yake hadharani wala chombo chochote cha habari kueneza kauli za mawazo hayo.
 
Huyu Muro tumepiga kelele muda mrefu, ashauriwe, asaidiwe, watu mkawa mnabeza. Leo mtu analeta hotuba ndefu na kutoa sababu za kulazimisha eti kaonewa!!! Ukiona mtu anashabikia kauli na vitendo vya Muro ujue ama hajui vizuri kazi ya Afisa habari wa timu au amezidiwa na dozi ya unazi.
 
!
!
ID hii nina wasiwasi nayo hii. Huenda ni ya bwana JM
 
Ki ukweli hata uwe una mchukia vipi Muro TFF hawa kuwa na sababu yoyote ya msingi ya kumfungia

Kuhamasisha vurugu ni kosa kubwa, mzaha mzaha unaweza kupelekea vifo vya mashabiki. Yatupasa wote tukemee hali hii. Michezo ni furaha, lkn ni eneo very delicate sana. Watu kuumizana ni kitu kidogo kabisa kma viongozi watachochea vurugu hata kwa ku-imply.
 
Back
Top Bottom