Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,763
- 50,213
Miaka ya themanini katikati (1984 - 1986) Gari lililokuwa linaonekana la kisasa na la thamani lilikuwa ni gari aina ya Pajero. Mitaani wakaamua kuiita shilingi mia tano "Jero" kwa kufupisha neno Pajero. Ndiyo kwenye miaka hiyo hiyo waliokuwa wanatumia kiswahili kwa kukigeuza walianza kuwaita watu wazima wanaume wanaofuatilia mambo ya watu wengine kuwa ni "wakuda" kwa kuligeuza neno "wadaku".
Wakati fulani Dar es salaam kulikuwa na tatizo kubwa sana la usafiri. Wakati huo pale Manzese Darajani Pakiitwa "Manzese Msufini". Miaka hiyo usafiri rasmi ulikuwa ni mabasi ya UDA. Ilikuwa unaweza kusimama Manzese Msufini kwa masaa zaidi ya matatu bila ya kupata basi la kukupeleka Kariakoo. Nauli ya UDA ilikuwa shilingi moja kwa watu wazima senti Hamsini kwa watoto.
Magari binafsi yalipoanza kutoa huduma ya usafiri huo kwa jiji la Dar es salaam, yakawa yanatoza nauli ya shilingi tano kwa safari. Wakati huo Dollar moja ya Kimarekani ilikuwa ni sawa na shilingi tano ya Kitanzania. Ndipo jina Daladala lilipoanza kutumika na kuota mizizi kwenye matumizi ya Lugha yetu ya Kiswahili.
Na wewe kama unayo mengine tuongezee ili tufahamu kuanza kwake kutumika katika Lugha yetu!!