Jennifer arejea nyumbnai kwao jana.

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
266
mwanafunzi aliyetoroka kwao kutokana na kupata ziro katika matokeo yake ya kidato cha nne arejea nyumbnai kwao jana.
Jennifer alitoweka kwao Januari 30 mwaka huu kwa hofu ya kupewa adhabu na wazazi wake kutokana na kupata ziro katika mitihani yake ya kumaliza elimu ya Sekondari.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii kilidai kuwa, Jennifer alirejea kwao hapo majira ya saa 3 usiku, akiwa na hofu kubwa kutokana na kile alichokifanya.

Ilidaiwa kuwa Jennifer aliongozana na mwanamke mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja alioyedaiwa kuwa alikuwa amemuhifadhi nyumbani kwake na alikuja hapo kumuombea msamaha kwa wazazi wake

Hata hivyo ilidaiwa kuwa Jennifer alijieleza kuwa alikuwa nyumbani kwa mama huyo kwa lengo la kumuhifadhi kwa kuwa alikuwa akiwahofia wazazi wake.

Imedaiwa kuwa mwanamke huyo alikiri kuwa Jennifer alikuwa nyumbani kwake alimuomba akae kwa muda nyumbani kwake kwa hofu ya wazazi wake.Wazazi wapokee bila ya kumuliza maswali ya kumtisha ili asikimbie tena.ANGALIZO Msimcheke kupata ziro bali iangaliwe kupata ziro nani alaumiwe mwanafunzi au ccm?maana matokeo yalikua mabaya sana mwaka jana.
 
Tumewaandaa watoto wetu kwa challenge kama hizi za kimaisha? Kwake hii ndio ilikuwa njia pekee. hajaandaliwa nyumbani wala shuleni
 
kwani yy ndiye wa kwanza kupata zero? wazazi wawe waelewa wakati mwingine!! nakumbuka hata mie sikufanya vizuri mitihani yangu, lkn niliporudia nilifanya vizuri sana!! hivyo kufeli si kwamba huna akili, bali ni bahati mbaya
 
alifichwa na bwana huyo hana lolote...................utamu umeisha kaaamua kurudi home.welcome back
 
bora karudi salama,wamsaidie tu manake hata yeye kufeli hakumfurahishi.
 
akapimwe, asije akawa amerudi na mjukuu tumboni, ataongeza machungu ya wazazi. Hatuwezi kumlaumu kwa kufeli hatujui maandalizi yalikuwaje.
 
sio mjukuu tu hata ngoma!!!kwa hesabu zangu za chapchap mwakani baraza la mitihani litapata fedha sana kwa kua vijana wengi watarudia pepa kama private candidate so watalipia!
akapimwe, asije akawa amerudi na mjukuu tumboni, ataongeza machungu ya wazazi. Hatuwezi kumlaumu kwa kufeli hatujui maandalizi yalikuwaje.
 
kamepewa mambo kamechoka kanona bora kurudi kwa mamaaaaaaaa, home sweet homeeee
 
mwanetu karibu nyumbani,tena nakuomba ujisikie amani kabisa.
Tutakuchinjia kondoo na ndama aliyenona sana.
Cheers
 
mwanafunzi aliyetoroka kwao kutokana na kupata ziro katika matokeo yake ya kidato cha nne arejea nyumbnai kwao jana.
Jennifer alitoweka kwao Januari 30 mwaka huu kwa hofu ya kupewa adhabu na wazazi wake kutokana na kupata ziro katika mitihani yake ya kumaliza elimu ya Sekondari.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii kilidai kuwa, Jennifer alirejea kwao hapo majira ya saa 3 usiku, akiwa na hofu kubwa kutokana na kile alichokifanya.

Ilidaiwa kuwa Jennifer aliongozana na mwanamke mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja alioyedaiwa kuwa alikuwa amemuhifadhi nyumbani kwake na alikuja hapo kumuombea msamaha kwa wazazi wake

Hata hivyo ilidaiwa kuwa Jennifer alijieleza kuwa alikuwa nyumbani kwa mama huyo kwa lengo la kumuhifadhi kwa kuwa alikuwa akiwahofia wazazi wake.

Imedaiwa kuwa mwanamke huyo alikiri kuwa Jennifer alikuwa nyumbani kwake alimuomba akae kwa muda nyumbani kwake kwa hofu ya wazazi wake.Wazazi wapokee bila ya kumuliza maswali ya kumtisha ili asikimbie tena.ANGALIZO Msimcheke kupata ziro bali iangaliwe kupata ziro nani alaumiwe mwanafunzi au ccm?maana matokeo yalikua mabaya sana mwaka jana.
wamwache tu maaana hili limekuwa janga la taifa!!! lakini uchunguzi ufanyike isije ikawa alikuwa kwenye madanguro akifanyishwa biashara ya kuuza mwili...maoni yangu tu...
 
Matokeo yalikuwa ni mabaya nchi nzima, labda kama wazazi wake sio waelewa. Huyo huenda aliwekwa ndani na mwanaume!
 
hahaaaaaaaaaaaa!!so mitihani inachangia watoto wetu kuwekwa kinyumba
Matokeo yalikuwa ni mabaya nchi nzima, labda kama wazazi wake sio waelewa. Huyo huenda aliwekwa ndani na mwanaume!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom