Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Baada ya Rais kutembelea miradi miwili ya ujenzi wa Barabara za Juu maeneo ya Tazara na Ubungo, Rais aliagiza kuwa Makao Makuu ya Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) lililopo eneo la Ubungo sambamba na jengo la Wizara ya Maji yawekwe alama X tayari kwa kubomolewa kupisha ujenzi wa mradi huo.
Sipingani na Rais yuko sawa katika amri ya kubomoa, ila hoja yangu hakuna uwezekano kufanya kama picha zinavyoonyesha hapa? Maana nijuavyo ni kwamba unajenga Fly Over kuepusha msongamano wa magari wakati huo huo shughuli zingine kama za Ofisi au Kibiashara zikiendelea maeneo hayo. Au hata Ulaya nako wanabomoa majengo wakitaka kujenga Fly Over, Au Ubungo Interchange?
Nawasilisha
==========
Mdau Mwingine
Jengo la Tanesco pale Ubungo limejengwa kwa fedha nyingi kwa mabilioni na ni fedha za wananchi masikini wa Taifa hili.
Ni kweli mradi wa Fly over ni wa muhimu na ni maendeleo kwa nchi lakini unapoleta maendeleo hupaswi kukurupuka na kuharibu vile vya thamani ulivyokuwa navyo awali.
Huo utakuwa ulimbukeni na kukurupuka. Nani kasema Fly over lazima inyooke? Kuliko kuvunja jengo la bilioni kadhaa, zingetumika milioni kadhaa kupata mshauri elekezi kutengeneza mchoro wa kukwepesha barabara kwa juu kwa hiyo section isiyozidi hata mita mia moja.
Kuliko kuvunja jengo kama majigambo wakati ni hasara. Mbona wenzetu wanaweza kufanya hivyo? Wataalamu wa kufanya hivyo wapo, tusipende wataalamu rahisi wa kubomoa. Oneni mbona hawa wameweza?