Jengo la ofisi yetu linatikisika

Hassan Mtengo

New Member
Aug 10, 2011
2
0
jamani tusaidieni ipo siku tutafunikwa,
hili jengo la habour view tower nina wasiwasi na viwango vyake.
upande wa ofisi yetu kulikuwa ni 'parking' hawa wenye jengo wakafanya
marekebisho sasa ni ofisi. tena ni ofisi kubwa tu ya shipping inayopokea
wateja wengi kwa siku. kinachotupa wasi wasi ni mtikisiko usioisha kana
kwamba kuna tetemeko la ardhi. chonde chonde wadau tusaidieni tukiwa hai
msingoje tufunikwe halafu mje kufukua vifusi
 
Tafadhali arifuni mamlaka zinazohusika kabla maafa hayajatokea.
Anzia Wizara inayohusika,Wizara ya Ujenzi
Kuna Bodi ya Wahandisi,ERB
Taasisi za maafa,
Hili ni muhimu kabla hatujapata mkubwa.
 
Gomeni, ondokeni ofisini !
Hakuna hatua zozote mtachukuliwa
 
Haiwezekani!!
Labda tuanzie hapa;
Hilo jengo lilijengwa mwaka gani?
Na je linaukubwa gani (urefu wake kwenda juu) ni gorofa ngapi mkuu?
Vipi hiyo hali inatokea kila siku au ni mara moja moja?
Vipi ofisi za jirani, nao wanaipata hiyo adha au ni ofisi yenu mkuu?

**Pengine hiyo sehemu iliyokuwa parking, baada ya kuikarabati basi hawakufanya kwa kiwango kwa kubania bajeti si unajua kibongo kibongo.
 
jamani tusaidieni ipo siku tutafunikwa,
hili jengo la habour view tower nina wasiwasi na viwango vyake.
upande wa ofisi yetu kulikuwa ni 'parking' hawa wenye jengo wakafanya
marekebisho sasa ni ofisi. tena ni ofisi kubwa tu ya shipping inayopokea
wateja wengi kwa siku. kinachotupa wasi wasi ni mtikisiko usioisha kana
kwamba kuna tetemeko la ardhi. chonde chonde wadau tusaidieni tukiwa hai
msingoje tufunikwe halafu mje kufukua vifusi

Hivi kwani msitoe taarifa kwenye vyombo husika au mpaka madhara yatokee ndio mnasema.

Hakika huu ni ujinga mara nyingi utakuwa unasikia. baada ya ajali watu ndio wanasema dereva alikuwa anakwenda speed sana lakini kabla ajali hawamwambii punguza mwendo.
 
tuliwahi kuwapigia simu hawa erb,lakini wana mlolongo mrefu sana,
hili jengo sio kama limeanza leo kutikisiska mimi naona kila siku linatikisika.
nina wasi wasi na viwango, kama kuna mwenye email yao atutajie tuwaandikie.
tupo ghorofa ya nane eti tunaambiwa hata likipita gari kubwa tu linatikisika
 
. kinachotupa wasi wasi ni mtikisiko usioisha kana
kwamba kuna tetemeko la ardhi.

Msiwe na wasiwasi hiyo ndiyo design yake, usihofu hayo ndio maendeleo ya teknolojia, siku kukiwa na upepo mkubwa utashangaa linazunguka kabisa mbele inakuwa nyuma.
 
Back
Top Bottom