Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Polisi wa Wilaya Tandahimba linaungua moto!

Habari kutoka tandahimba zinasema kuwa watu wenye hasira wamevamia na kukichoma moto kituo cha polisi katika eneo hilo.

Source: Tbc1
 
Bora angeungua tu na huyo OCD kwani amekuwa kikwazo kikubwa kwa wananchi pindi wanapodai haki zao.

Kwa wananchi wanaomjua vizuri OCD,wanamuongelea vema,wala si mtu mbaya..

Kwa juhudi zake amewezesha ukaribu wa askari na raia kwa kufungua canteen ya vinywaji vikali na baridi..

Na ni mtu mwema tu kwa kweli.. Ila watu hawaipendi kazi yake,na askari wake.. Na mikong'oto mara nyingi inatoka kwa askari wa wilaya jirani,kama Newala na Mtwara..

Ila wiki iliyopita palikuwa fujo za raia dhidi ya askari na baadhi ya watumishi wa serikali.. Kwa kuibiwa,kuchomewa nyumba moto,kuzuia magari barabarani kwa magogo,n.k.
 
hii style ya mabomu naona imeshamiri bongo now kitu kidogo mabomu naona yako mengi sn so wanataka yaishe haraka waagize mengine,mwisho yatazoeleka na watu watatafuta jinsi ya kujikinga nayo,anyway poleni huko kwa moto mtulie ili uchunguzi ufanyike. bila kukosea itaundwa tume!
 
Yaani OCD kusaidia ufunguaji wa canteen za vinywaji vikali na baridi ndio mnamwona mwema!!!???
 
Kwa sisi ambao ni watumishi wa kawaida wa serikali kwa kweli tunaishi roho juu.. Wengi wetu wameondoka kurudi makwao,wengine wa asili ya huku wamekimbilia vijiji vya jirani!

Na mabomu usisikie.. Sijui yana uzito wa gramu ngapi! Yana vishindo vikubwa sana! Hata kama ulilala usingizi gani,utaamka tu!
 
ths is very bad. polen sana ndugu zetu wz tandahimba. but kwa wale wenye ndugu mikoa jirani ni bora kwenda hadi hali ya huko iwe shwari. na wanawake na watoto ni bora wakajiondoa maema. lakin mm najiuliza hivi rais kama alipopata taarifa za kifa kesho yake alikwenda kwanini na huko ambako amani inatoweka asiende kuongea nao?????au mimi nimewaza tofauti jamani? nafikiri mtu wa kuwasaidia ni rais mwenyewe au atoe tamko jamani. sasa tunakuwa kisiwa cha fujo badala ya amani
 
Yaani OCD kusaidia ufunguaji wa canteen za vinywaji vikali na baridi ndio mnamwona mwema!!!???

Ni mstaarabu sana,hata katika maisha ya kawaida.. Ila watu wa huku ukitaka kukorofishana nao,uwasumbue katika 'madini' yao wanayoyategemea...KOROSHO! Hapo watageuka wanyama kabisa!
 
Hivi yule aliyekuwa mgombea wa CUF Ahmed Katani yuko wapi siku hizi maana nasikia jamaa alichakachuliwa na magamba. Je hakufungua kesi ya kupinga ushindi "fake" wa mgombea wa CCM?
 
ths is very bad. polen sana ndugu zetu wz tandahimba. but kwa wale wenye ndugu mikoa jirani ni bora kwenda hadi hali ya huko iwe shwari. na wanawake na watoto ni bora wakajiondoa maema. lakin mm najiuliza hivi rais kama alipopata taarifa za kifa kesho yake alikwenda kwanini na huko ambako amani inatoweka asiende kuongea nao?????au mimi nimewaza tofauti jamani? nafikiri mtu wa kuwasaidia ni rais mwenyewe au atoe tamko jamani. sasa tunakuwa kisiwa cha fujo badala ya amani

Yaani UHALIFU NA HUJUMA hizi umefichwa kwenye MWAMVULI WA KUDAI MALIPO YA PILI YA KOROSHO ZAO...
 
Shine tazama tu utaona thread yangu.. Tangu jana usiku nilipost..

Mkuu gee cee poleni kwa misukosuko inayoendelea, ikiwa bado upo tandahimba, ndiwe pekee kwa sasa umeripoti kwa haki matukio ya tandahimba. hebu tupe updates.
 
Haonekani!! Kama vp tujuze kilichotokea na kinachoendelea!!
Binafsi nimewachoka hawa Policcm, acha wananchi wachukue uamzi sitahiki!!

ipo siku utawatafuta pamoja na mapungufu yao. uzuri taasisi hii bwana, ni utumishi wa umma, leo unaiponda kesho upo kwao wakutatulie baadhi ya shida zao. Mleta mada hajasema chochote zaidi ya kutaka maelezo kwa wadau, badala ya kumpa maelezo mnawapongeza wananchi kuchoma kituo cha polisi. kama ndo utawala bora sawa.

lakini suala la msingi ni kuwa, wananchi wa maeneo hayo wana madai na serikali kama sio mzabuni kuwa alichukua KOROSHO zao lakini hataki kuleta mafao yao.

juzi walikata hadi nguzo za tanesco, wameangusha barabara, wamekata miti na kuziba barabara na uharamia mwingi. sasa kuchoma kituo cha polisi ndo polisi itawalipa hizo pesa zao?

kwa nini wasimwendee aliyechukua mazao yao na kumwajibisha?
 
Shine tazama tu utaona thread yangu.. Tangu jana usiku nilipost..
Ni kweli, mimi pia nakumbuka thread yako ya jana. But ulisema jengo la mkuu wa polisi kwa hiyo mimi sikuelewa. Lakini kama ni kituo cha polisi ni vema tukajua usalama wa mahabusu. Maana vituo vya polisi huwa vina mahabusu wanaolala mle. Je waliokolewa au imekuwaje?
 
Hivi yule aliyekuwa mgombea wa CUF Ahmed Katani yuko wapi siku hizi maana nasikia jamaa alichakachuliwa na magamba. Je hakufungua kesi ya kupinga ushindi "fake" wa mgombea wa CCM?

Alifungua kesi ila inaenda taratibu sana... Yupo,ila huwa ni mtu wa pilika pilika.. Mara Dar,mara mikoani. Wiki iliyopita alikuwa pamoja na Mtatiro kwenye maandamano ya chama chao kuulizia mustakabali wa malipo yao yaliyobaki ya korosho..
 
Back
Top Bottom