Jengo la machinga…. Umiza kichwa

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,541
29,604
Jiji wamesema kwamba kila mfanyabiashara atapata kizimba cha meter square. Hebu mnaojua undani mtufafanulie equation hii.
Je ukubwa wa jengo I mean mita mraba za kila floor ni ngapi, halafu gawanya kwa mita moja mraba halafu weka katika kila mita mraba mtu mmoja mwenye kilo hamsini. Kisha kila kizimba at onetime kinapata five wateja watano wote wana kilo hamsini. Zidisha kwa ukubwa wa floor halafu mnaojua vipimo vya jengo lile mtuambie uwezo wa jengo wa kubeba uzito kwa muda mmoja. Je hatujisogezi kwenye maafa mengine??
Kama wakiweka utitiri wa wafanyabiashara at one place (machinga complex) mjue sisi wateja tutakuja huko and mjiandae kwa explanation endapo jengo litaporomoka kutokana na uzito wa watu hasa siku za sikukuu na mwisho wa mwaka.

Kwa nini msiwaweke wachache halafu mkajenga mengine kila manispaa ili kupunguza msongamano na gharama zisizo na lazima? Pia ninyi serikali msiwasahau watu wa mikoani wekeni complexes katika miji mikuu ili kupunguza wimbi la wanaoingia jijini kusaka mahitaji siku za sikukuu.

Umiza kichwa katika hili
 
Well thought idea....!
 
Kula tano mkuu
unajua ni kweli tunataka vitu lakini ni budi tujue hivyo vitu kwa undani tusije tukanunua umauti wetu wenyewe.
 
Duh! Kila mita moja kuwe kuna machinga! Si vurugu mechi itakuwa.
 
Hiyo wanapatiwa wale wanaojuana na wakubwa tu! Wale makabwela kama mimi hawataambulia hata robo ya hiyo nafasi!
 
Achana na siasa mwenzetu katoa pre caution ya kitaalam ambayo ni technical issue inahitaji utaalamu kuelezea madhara yatakayo tokea wakati shughuli ikiendelea kutokana na jinsi wanavyo taka kugawa,ila mi mwenyewe kama kweli wanataka kugawa hivyo sijui na viwango vya wachina!
 
Mkuu thanks kwa kufafanua
wabongo wanadhani kila kitu ni siasa tu! kuna wakati tunapaswa kuchukua kalamu na karatasi na kukuna kichwa kusaka majibu ya equation.

Natumaini wataalam watakuja na assumtions za hii kichwa umiza
 
Sijui safety factor waliyo tumia ktk kudesign hilo jengo na kawaida majengo yanayo hudumia jumuiya kama viwanja vya mpira, kumbi za starehe n.k. huwa standards zinasema safety factor iwe kubwa sasa kwa machinga complex sijui.

Kama standards zimefuatwa (over-design due to unpredictable number of occupants) basi hata watu wajae kiasi gani haliwezi kuporomoka. Tatizo huwa linakuja kama aliye design katumia viwango vya majengo ya kawaida ambayo huwa na a limited number of occupants.
 
Kwa Tanzania niijuayo mimi, utakuta aliyesimamia ujenzi wa complex ameiba sementi ya kutosha na amewajenge vimada wake wooote bangaloo za nguvu, sasa tegemea estimated materials were successfully used (kifisadi) halafu tatizo litokee.

Nilidhani kabla halijatumika wangekaa watu wa majengo na manispaa wafanye tathmini ya kujihakikishia uimara wa jengo kwa idadi wanayoitaka ya watu at a time. Pia washauriwe (manispaa) idadi ya vizimba kwa kila floor.

Je walemavu wamekumbukwa pia?? maana kama mtawapatia vizimba pekee je mmejenga vyoo vya watu wasiojiweza?? kuna maswali mengi hapa. ila ninashauri Meya na RC wa-think out of BOX ili kuweza kuepusha yanayoepukika
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom