Jengo la CCM Mtwara lateketezwa kwa moto

Jengo la CCM Mtwara lateketezwa kwa moto

Ni kwa nini mikoa mingine hatuwasapoti wanaMtwara? Ilitakiwa baada ya wao kukianzisha huko na sisi wengine tungewapa sapoti ya kuwachoma moto hawa magamba... Yaani unalikamata li gamba lako moja unalipiga kiberiti...
 
Ccm ndo serikali huo ndo ukweli kwani akina nape wameshindwa kumshauri baba rizi 1

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Mtela acha upumbavu. Huyo Slaa unamtaja kila siku huchoki?? Kuanzia kule fb hadi huku ni Slaa tu.Hata kwenyn mambo ambayo hayamhusu utaropol Slaa. Inavyoonekana hata Obama akiahirisha kuja Bongo utasema ni Slaa kasababisha. Hivi elimu yako inakusaidia nini Mtela Mwampamba!!!????

Mkuu hachana na "mali" ya shegela hiyo... Ukiona mtoto wa kiume anaongea kwa kubana pua huku akilegeza macho inabidi ujiulize mara 2 -2....
 
[MENTION][JFMP3][/JFMP3][/MENTION]
Heko kwa Dr Slaa kuwafundisha watanzania kudai haki zao!!

Ntonga, nakumbuka miaka kama 18 iliyopita kunakitu MTIKILA alikiongea pale JANGWANI mpaka leo huwa ninakitafakari ndiko tunakoelekea sasa na wala mda si mrefu!! alisema maneno haya, WATANZANIA NI WATU WAPOLE NA WANAOTII SHERIA SANA, ILA UTAFIKA MDA MTU ATAONA HANA CHAKUPOTEZA, akaendelea UTAFIKA MTU ATAAMUA KULIKO NIKIFA NAJIONA NA NJAA NI HERI NIENDE PALE KWA YULE ALIENACHO NIKAMNYANGANYE NIPATE KUINUSURU FAMILIA YANGU HAPO NDO SHUNGHULI YENYEWE ITAKAPOANZIA, tumwombe sana mungu atunusuru
 
umeshapata namba ya slaa umueleza ulipofikia kuchoma majengo ya ccm

Wewe ulivyo piga bomu kanisani arusha.Then ukakimbilia uganda kwa ndugu zako waasi. Tuachie nchi yetu nishakwambia.Nenda congo kwa nduguzo
 
Nachokisema hapa ni kwamba,hivi vitendo si vya kuvichekea,ipo siku tutakuja vijutia,hata BOKO HARAM kule Nijeria walianza hivi hivi na sasa serikali imetanga hali ya hatari ktk maeneo wanayoishi.
maumivu ya kichwa huanza polepole na kikawaida matukio kama haya huwa hayana macho,maana ccm hawana alama,tutakuja jutia ipo siku.

Hakuna cha BOKO HARAM wala BOKO HALALI, the issue sikilizeni sauti za wana mtwara na mheshimu mawazo yao. Thats all.
 
Wanasiada wanaiharibu hii nchi

Chukulia mfano kweni pana chemchem ya maji mazuuri,akakurupuka mtu huko akafunga likoki lake hapo nakufyonza maji yote bili maafikano mazuri,hapo utasemaje???viongozi wa hii nchi wababe wanyanyasaji na mandumila kuwili..chomeni msiache hata bomba la bendera za magambaring.

The nation that destroys its destroys itself.
 
hivi hii damu ya wana Mtwara inamwagika kwa faida ya nani?je kuna uharaka gani wa jambo hili kufanyika bila kutoa muda wa kusikiliza ni nini hasa matakwa ya wana Mtwara hata kama Serikali haipendi ili maendeleo ya kweli na yenye nia thabiti yatimizwe.....
 
Hao watu wa usalama kweli ni ovyo,vitu kama hivyo lazima vinakua predicted kwa jinsi hali ilivyokuwa,wangeweka pre emptive measure...jengo lichomwe mchana eti na watu wasiojulikana.upuuzi mtupu.
Kama sio wewe vile naona leo umewageuka wenzio policcm hahahaaaaaa wamechoka kutumika
 
Chukulia mfano kweni pana chemchem ya maji mazuuri,akakurupuka mtu huko akafunga likoki lake hapo nakufyonza maji yote bili maafikano mazuri,hapo utasemaje???viongozi wa hii nchi wababe wanyanyasaji na mandumila kuwili..chomeni msiache hata bomba la bendera za magambaring.

The nation that destroys its destroys itself.

Ndugu zangu

Gesi ni yetu, CCM ni yetu, CDM ni yetu, Mtwara ni yetu, rais ni wetu, nchi ni yetu.
Mustakabali mwema wa hii nchi hautapatikana kwa kumwaga damu na kuchoma mali za watu.

Tunamamlaka kamili na nilivyovitaja hapo juu.

Tukae chini, tutafakari kwa kina na kuchukua hatua sahihi, hii ni nchi yetu sote, ni ujinga uliopitiliza kuivuruga then tujidanganye tutajenga kesho. Tujifunze kutoka Syria, Libya nk.

Vurugu, vita , ubabe na kumwaga damu sio ufumbuzi.

Zipo njia mmbadala na sahihi.

Na wote tunazijua.

Sio hizi.

Respect !!!

Walishakaa chini sana kuongelea mambo yaleyale hadi makalio yameota sugu. This is time for action maana hata wakikaa hadi mwakani hakitaeleweka.
 
Hakuna cha BOKO HARAM wala BOKO HALALI, the issue sikilizeni sauti za wana mtwara na mheshimu mawazo yao. Thats all.
Nachokisema ni kwamba,hata kama watasikilizwa,lakini bado hii tabia itatuletea madhara siku za usoni,imeanzia mtwara na itaishia ktk matatizo makubwa ya kiusalama
 
hivi hii damu ya wana Mtwara inamwagika kwa faida ya nani?je kuna uharaka gani wa jambo hili kufanyika bila kutoa muda wa kusikiliza ni nini hasa matakwa ya wana Mtwara hata kama Serikali haipendi ili maendeleo ya kweli na yenye nia thabiti yatimizwe.....

Ndugu zangu

Gesi ni yetu, CCM ni yetu, CDM ni yetu, Mtwara ni yetu, rais ni wetu, nchi ni yetu.
Mustakabali mwema wa hii nchi hautapatikana kwa kumwaga damu na kuchoma mali za watu.

Tunamamlaka kamili na nilivyovitaja hapo juu.

Tukae chini, tutafakari kwa kina na kuchukua hatua sahihi, hii ni nchi yetu sote, ni ujinga uliopitiliza kuivuruga then tujidanganye tutajenga kesho. Tujifunze kutoka Syria, Libya nk.

Vurugu, vita , ubabe na kumwaga damu sio ufumbuzi.

Zipo njia mmbadala na sahihi.

Na wote tunazijua.

Sio hizi.

Respect !!!

Walishakaa chini sana kuongelea mambo yaleyale hadi makalio yameota sugu. This is time for action maana hata wakikaa hadi mwakani hakitaeleweka.
 
Kama ni kwelI basi wana. Mtwara wanastahili pongezi.good job wana mtwara choma magamba, teketwza magamba, maliza magqmbq.

Una laana ya Ukoo wewe! Yani ukoo wenu utakua ndugu na Shetani! Huwezi furahi ujinga unaofanyika Mtwara
 
Moto Unawaka Mtwara.
...ukiwatazama
kirahisi watu wake unaweza
kudhani mafala...niliposikia
nao wameanza
maandamano ya kudai haki
zao nikajua sasa shughuli
imeanza. hakuna watu
wabishi kama watu wa
Mtwara....Machalii wa
Arusha wanasubiri,
Wanyakyusa
wanasubiri.....watawala kazi
wanayo hapo..tabia ya
majibu mepesi kwa maswali
magumu usiwapelekee hao
jamaa!
 
Haya wameyataka wenyewe acha wakione cha mtema kuni,Wanamtwara gesi kwanza vyama baadaye@Mtwaranias.
 
  • Huko MIKINDANI ofisi zote za serikali zavamiwa na kuchomwa na mpaka daraja la Mikindani nalo limevunjwa kwa maana hauwezi kutoka wala kuingia MTWARA
  • Kuna madai kwamba silaha zimeibiwa (Haijathibitishwa)
  • Maaskari wanafanya msako wa nyumba hadi nyumba maeneo ya Magomeni na Mangowela
  • Askari achomwa mshale. Haijulikani hali yake
  • Ni mapambano baina ya vijana na maaskari. Vijana hawaogopi tena risasi wala mabomu . Kundi limeelekea Shangani kwenye nyumba za vigogo.
  • Nyumba ya kupumzikia wageni inayoitwa Shengena Lodge imechomwa moto kwa kile kinachoelezwa kwamba iliwapokea askari Polisi.
  • Ofisi ya CCM saba saba imechomwa moto, na baadhi ya waandishi wamezingirwa maeneo ya Sokoni, sasa ni milio ya risasi na mabomu.
  • Matairi kila kona ya mji yamechomwa barabarani polisi na zimamoto wanafanya kazi ya kuzima na kufukuza wananchi. Kauli mbiu "Gesi haitoki hata kwa bomba la peni"

  • Kambi ya Upinzani yaukataa mpango wa serikali wa ujenzi wa bomba la gesi

  • Nyumba kadhaa za watumishi wa Serikali zimechomwa maeneo ya Shangani.(habari haijathibitishwa rasmi)

  • Ni magari ya FFU tu ndio yapo barabarani nayo hupata wakati mgumu kupita kwasababu ya mawe na magogo yaliyowekwa na vijana,baadhi ya watu kadhaa wamechukuliwa na askari eti kwakuwa walipita jirani na gari yao,askari wengi waliokuja si wa hapa Mtwara wengi wametoka Masasi na Lindi. Ving'ora vinalia ovyo ovyo.


  • watoto wamefungiwa mashuleni walimu wamekimbia


  • Vituo vya Redio vya Mtwara havizungumzii hali hii ya hatari. Vinapiga Muziki pengine vinakusanya matukio na habari ya majanga haya. Ili Wananchi wayapate .


  • Mabomu yanapigwa mfululizo maeneo ya Magomeni-Mtwara . Takriban mabomu 20 na ushee mpaka sasa. Na wanaendelea kupiga mabomu.

  • Sasa hali si shwari kila eneo, wakionekana watu watatu wanaongea maongezi maaskari wanapiga mabomu. Mabavu yamechukua mkondo wake. Wananchi wamejifungia majumbani mwao. Chuki dhidi ya Polisi yaimarika. Polisi wanapiga mabomu bila mwelekeo.

  • Magomeni na sokoni kimenuka, mabomu yanarushwa na wananchi wanakimbia ovyo.


  • Kituo kimoja cha habari kinachorusha habari za bunge chazuia mawimbi yake kwa Mkoa wa Mtwara hivyo hakisikiki(Redio na TV). Na kimewanyima haki wananchi wa Mtwara ya kupata taarifa.(Hatimaye wamerejesha matangazo yao)


  • Waziri wa Nishati amesoma hotuba yake kwa hisia kali na mbwembwe. Mwishoni amesema bomba la gesi linajengwa kutoka Mtwara kwenda Dar.



  • Maduka yote yamefungwa, baa zimefungwa, hakuna huduma za usafiri, ofisi za serikali zimepwaya kimsingi hakuna lolote linalofanyika

  • Boda boda zinazoonekana maeneo ya Nkanaledi na abiria zinapigwa mawe.


  • Makachero nao wanajifanya madereva wa boda boda na Bajaji, Tax wengine wanatembea na magari ya Serikali.


  • Maeneo yote yametawaliwa na ukimya.


  • Kesho inaendelea tena kwa siku ya pili.
  • Serikali isipoangalia inaweza ikasababisha "Uprising" maeneo mengine ya nchi.

Source: http://mtwarakumekucha.blogspot.com/
 
Back
Top Bottom