Ccm wameongeza Kuni kwenye moto unaowaka.

Ccm wameongeza Kuni kwenye moto unaowaka.

maganjwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2012
Posts
2,810
Reaction score
2,357
Kwa jinsi hali ilivyo na upepo wa siasa unavyovuma wasingemfukuza Emanuel Nchimbi Kwa kusema hana nidhamu. Kwanza waliotakiwa kujua siasa ya nchi yetu imekuwa ngumu sana hasa Kwa ccm kuliko upinzani. Na kwenda Kwa wananchi na kueleweka inahitaji kuweka unafiki pembeni na kusema ukweli.

Hapo ndipo shida inapoanzia. Tanzania watu huamini siasa ni mchezo mchafu. Wakati katika uhalisia siasa ni maisha. Kwa nini nasema siasa ni maisha Kwa sababu inaamua maisha ya watu, na inaweza gharimu maisha ya watu. Sasa huo siyo mchezo mchafu. Unakuwa mchezo mchafu pale tunakuwa hatuna siasa safi. Kama Tuna siasa safi, siasa ni maisha.

Tujikumbushe mapinduzinya Iran ya February 1979 yakiongozwa na hayati ayatola ally khamenei. Irani ilikuwa taabani sana kiuchumi, kisiasa, kijamii na kijeshi. Lakini siasa safi ya kujali watu na kuipenda nchi na kukataa western imperial powers ikawasaidia. Kijamii wakati wa mapinduzi wasomi nchini Irani walikuwa 32% ujinga ulikuwa 68% Kwa Sasa Iran ni nchi ambayo watu wake wameenda shule sana duniani wasomi ni 93%. Kijeshi ndo superpower middle East. Huu ni mfano wa siasa safi inavyobadili maisha ya watu katika nchi.

Sisi tumekosa siasa safi yenye kuwaletea watu nafuuu ya maisha. Kinachotusaidia sisi ni masalia ya siasa ya ujamaa. Hili watu hawalijui. Kwa mfano ardhi kuwa Mali ya serikali ndo inasababisha watanzania kuwa na nafuu ya maisha na majirani zetu. Popote utakapoenda Wala hakuna anayekuuliza kama ukakuta Kuna ardhi unakaa unaanzisha maisha. Hii ndo inayotusaidia bila hiyo sera Kwa kweli kilio chetu kingeshafika mbali na watu wangekuwa makini sana na siasa. Watanzania hawako makini na siasa Kwa kuwa maisha yanaenda ingawa serikali inaingia mikataba mingi isiyo na faida Kwa wananchi.

Kwa Sasa hali ya siasa iko very tense sana Kwa maoni yangu kumfukuza Emanuel Nchimbi ni kuongeza Kuni kwenye moto unaowaka wa hali ya kisiasa hapa nchini. Watanzania hawajawahi kuwa makini na siasa kama kipindi hiki. Viongozi wa kisiasa wanafuatiliwa na raia like never before. Mijadala iko tight sana na hili tukio la makamu wa rais kuachia ngazi ni la kwanza Kwa nchi yetu.

Anyway ngoja tuone huu mpira dakika itaishaje hapo 2030.

Nawasilisha
 
IMG-20260827-WA0003.jpg
 
Back
Top Bottom