Jengo la bunge linavuja

Jengo la bunge linavuja

Fruit

Senior Member
Joined
Jan 1, 2013
Posts
193
Reaction score
54
Katika hali ya kushangaza Mbunge mmoja aliomba taarifa kwa Mh. Job Ndugai jana jioni kuomba kutoa taarifa ya kuvuja kwa jengo la Bunge sehemu anayokaa yeye, Tundu Lisu na sehemu mbalimbali ndani ya jengo hilo, hivi kweli jengo lililojengwa kwa gharama kubwa hata miaka 20 halijafika linaanza kuvuja! kwa wale waliongalia Kikao cha Bunge jana jioni walijionea hilo, wabunge wanapata wakati mgumu hasa kikao kinapoendelea wakati mvua inanyesha.
 
Defaults zinatokea tu unless utuambie hujawahi kujenga. Tatizo la uswahili ni.maintainance na sifa za kijingajinga. Alihitaji kutoa taarifa kwa bunge zima? Manake kama ni sehemu inavuja basi.ni suala la kutaarifu hata mhudumu tu akatoe.taarifa. Next mbunge ataomba kuongelea kiti kina-squake!
 
Katika hali ya kushangaza Mbunge mmoja aliomba taarifa kwa Mh. Job Ndugai jana jioni kuomba kutoa taarifa ya kuvuja kwa jengo la Bunge sehemu anayokaa yeye, Tundu Lisu na sehemu mbalimbali ndani ya jengo hilo, hivi kweli jengo lililojengwa kwa gharama kubwa hata miaka 20 halijafika linaanza kuvuja! kwa wale waliongalia Kikao cha Bunge jana jioni walijionea hilo, wabunge wanapata wakati mgumu hasa kikao kinapoendelea wakati mvua inanyesha.

Madhara ya 10% ndio hizo, wasubirie ipo siku litakapowaangukia hilo jengo ndipo watakapotia akili
 
Bunge linavuja na halijaanza kuvuja jana, wala halivuji sehemu moja. Ila tusiogope, kwa kuwa sis ni wageni katika nchi hii.
 
Katika hali ya kushangaza Mbunge mmoja aliomba taarifa kwa Mh. Job Ndugai jana jioni kuomba kutoa taarifa ya kuvuja kwa jengo la Bunge sehemu anayokaa yeye, Tundu Lisu na sehemu mbalimbali ndani ya jengo hilo, hivi kweli jengo lililojengwa kwa gharama kubwa hata miaka 20 halijafika linaanza kuvuja! kwa wale waliongalia Kikao cha Bunge jana jioni walijionea hilo, wabunge wanapata wakati mgumu hasa kikao kinapoendelea wakati mvua inanyesha.

Chezea 10% ya William Erio Mkapa wa PPF nyie. Majengo yote ya serikari ambayo PPF iliweka mkono kipindi cha uongozi wa William Erio kama DG wa PPF ni feki (Fake from China). Huyu Mheshimwa alikuwa anaweka wajenzi bila kuifuata taratibu za manunuzi kwa kutishia kuwa Ikulu wameagiza ampe huyo amtakaye.

Nenda UDOM, majengo yaliyojengwa kwa PPF yamechakaa kama vile ni ya wakati wa Uhuru. Mabafu na vyoo wanafunzi wa UDOM ni mashahidi.

Bunge liunde tume kuchunguza na kumchunguza mtia hasara.

Nimeitaja PPF na Erio pamoja na madhambi yote haya, mod atafunga hii thread.
 
ukarabati siyo desturi yetu naungana na aliyesema huenda mnaochangia maada hii hamjawahi kujenga kumbukeni pia dodoma ni ukanda wa tetemeko la ardhi .uliyetoa maana tupigie simu tukuelimishe
 
Sioni cha ajabu apo. Kwani wao wazazi na bibi zao wanaishi kwenye nyumba ambazo hazivuji?

Mbona pale nje kwenye mabenchi huwa tunanyeshewa sisi tuliowapigia kura! Au wao wana-uspesho gani?
 
Hayo ni ya kawaida tu. Mbona sisi jengo letu la darasa ni la nyasi na tunavujiwa kama kawa!
 


KITAIFA




201822420.jpg
​




[h=1][/h]
job_ndugai.jpg
​


Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Posted Jumapili,Februari3 2013 saa 9:4 AM

KWA UFUPI


“Taarifa mheshimiwa Naibu Spika, hili jengo linavuja, kwa kweli hata hapa nilipokaa ndiyo hasa maji yanapita... sasa tuhakikishiwe usalama wetu Naibu Spika,”



BAADHI ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wanaoendelea na kikao cha 10, wameulalamikia uongozi wa Bunge kwa kutojali kufanya marekebisho ya jengo la Bunge wakidai kuwa linavuja kwa muda mrefu sasa.


Malalamiko ya wabunge hao yalifikishwa kwa Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai jana, ambapo walisema kwamba wana wasiwasi na usalama wa jengo hilo.

Ubovu huo ulibainika juzi Ijumaa baada ya mvua kuanza kunyesha usiku saa saba na kuendelea hadi mchana katika maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma.
Mbali na eneo linalokaliwa na wabunge kuvuja, maeneo mbalimbali ya jengo la bunge yalikuwa yanavuja.


“Taarifa mheshimiwa Naibu Spika, hili jengo linavuja, kwa kweli hata hapa nilipokaa ndiyo hasa maji yanapita... sasa tuhakikishiwe usalama wetu Naibu Spika,” alisema Mchungaji Peter Msigwa.

Akijibu hoja hiyo, Ndugai alisema, “Taarifa zimefika kwa sasa wataalamu wetu wa maeneo mbalimbali ya jengo wanafanya kazi kuhakikisha wanarekebisha hali hiyo.”


Jengo la Bunge mjini Dodoma lililojengwa kisasa zaidi kwa ushirikiano kati ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa gharama ya zaidi ya Sh29.8 bilioni kwa sasa lina uwezo wa kubeba wabunge 350 kwa pamoja, wageni maalumu zaidi ya 100 na wananchi wasikilizaji 200.

Ukumbi huo wa kisasa umekuwa mfano wa kuigwa ambapo wawakilishi wa mabunge kadhaa kutoka nchi mbalimbali za Afrika ambao wamekuwa wakifika mjini Dodoma wamekuwa wakiuchukulia kama mfano.

 
Back
Top Bottom