Jenerali Ulimwengu, kumbe hata wewe ni mnafiki!

Jenerali Ulimwengu, kumbe hata wewe ni mnafiki!

wiseboy.

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2014
Posts
2,931
Reaction score
4,550
Nakubaliana na prof James Watson kuwa sisi watu weusi tuna uwezo mdogo sana wa kufikiri, ni wewe Jenerali Ulimwengu uliyewahi kutofautiana na serikali ya CCM kisa kuandika maovu yao, wakakupora uraia wako wakisema kuwa wewe si mtanzania na ukaanza kuishi ndani ya nchi yako kwa kulipia kibali, mtu uliyewahi kuwa mkuu wa Wilaya unaambiwa si raia na uishi kwa kibali, sasa hivi unaipigia kampeni CCM iendelee kutawala wewe na mwenzako Mbwambo, huu ni unafiki wa hali ya juu kupindukia, leo CCM imekuwa nzuri kwako kwa lipi hasa?

Hata kama padlocks ni best yako tambua kuwa CCM ni mfumo hata aje malaika awe rais kupitia CCM hakuna kitakachobadilika,tupo vitani kuhakikisha kuwa CCM inaanguka kwa gharama yoyote ile, unapokuwa vitani huwezi kuchagua silaha za kupigania, inapobidi unaweza kutumia silaha ya adui ili kushinda vita pindi ukifanikiwa kuiteka ndo maana tukamchukua Lowassa, Lowassa ni bomu la nyuklia ktk vita dhidi ya CCM na kwa hiyo lazima tushinde hii vita,wewe na wenzako mmetugeuka ktk battle field,hamfai kabisa.
 
Waambie hao! Ni kweli kwamba uandishi wa raia mwema na raia tanzania umebadilika kutoka kukemea maovu hadi kutetea mafisadi. Nadhani watakuwa wamenunuliwa na mafisadi (ccm).
 
Ulimwengu anaandika makala zake kwa nadharia na falsasa sana. Makala zake ni abstract sana, kiasi kwamba kama ni msomaji mgeni hutazipenda. Hii haijalishi ameandika kwa Kiswahili au Kiingereza. I can vouch for this guy-I have known him for a long time to know he is a true activist/reformist. Ni mmoja ya waandishi wachache wasiopelekeshwa na dini, ukada wala ukanda.

Yeye kama mmoja wa wamiliki wa Raiamwema ni mwandishi mkongwe wa habari na anajua sio busara na ni kinyume cha maadili ya uandishi kuwapangia wenzake cha kuandika. Na inafahamika toka enzi za Rai kuwa kuna baadhi ya waandishi wao 'akili zinahama' wakati wa uchaguzi na wamewahi kuliweka bayana. Mfano Maggid wa nyakati za uchaguzi ni tofauti na wa nyakati zingine zote. Wakati wa uchaguzi, yeye ni pro CCM.

Kwa upande wa Mbwambo, huyu nae ni mwanamageuzi asiyetetereka. Amekuwa na msimamo usioyumba kwenye kutetea mageuzi. 'Tatizo' lake, uanamageuzi wake umejikita kwenye misingi-sio pragmatist. Kiukweli, kwa wafia mageuzi na washabiki wa siasa za chadema, kumpokea Lowassa ilikuwa ngumu sana kwasababu anaenda kinyume na wengi wanachokiamini. Baada ya kuandika makala zaidi ya 20 za kuponda ufisadi na Lowassa, naweza kumuelewa akikataa kumeza matapishi yake.

Namuunga mkono Lowassa kwa sababu he is a real threat to CCM.Japo naunga mkono ukawa, nina wasiwasi (kama Mbwambo) na mstakabali wa baadae wa chadema. Rejea historia ya NCCR mageuzi. Baada ya NCCR kuzimia kisiasa, upinzani wa kweli na mhemuko wa siasa za upinzani ulipoa sana-hiki ndo wanamageuzi waliojikita kwenye misingi wanakihofia. Ukiondoa ajenda ya ufisadi, chadema itazimia kisiasa. Hata hivyo tumaini lipo kwenye idadi ya wabunge wengi wanaoweza kupata. Sina tatizo na Mbowe, ni mwanasiasa makini na mahiri, amefanya kile Mandela na ANC walikifanya-kuungana na adui (National party) kuunda serikali ili kujenga nchi na kusonga mbele. Historia itamhukumu Mbowe, kama ambavyo baadhi ya weusi wanamlaumu Mandela.

Ulimwengu ahishimiwe, ni mwanamageuzi na mwanaharakati nguli. Ni kama Dr. Slaa. Hatuwezi kuthubutu kuusahau mchango wake (kama tunajiheshimu) ktk mageuzi eti kwasababu tu haungi mkono kuja kwa Lowassa, hata kama tunampenda sana Lowassa.
 
Mandela alishirikiana na makaburu na wapinzani wake baada ya kuingia ikulu na siyo kabla. Kwa hiyo Mbowe amekosea kumkaribisha Lowasa na kumfanya mgombea wa chadema. Watu wenye akili za kutosha hawawezi kumpa Lowasa kura. Huyu mtu hana maadili na anatumia fedha kutafuta urais na hii ni Hatari. Nina hakika baada ya kampeni wengi wanaonfuata watabadilika na hawatampa kura. Ukawa turidhike na wabunge zaidi ya nusu ili kuithibiti serikali na Sera zetu na ilani yetu zitekelezwe na serikali itakayoundwa hata kama Tingatinga akiwa rais.
 
Umeongea vyema kabisa lakini naamini kuwa hata ktk ubunge Ukawa mmepoteza sana kwani wagombea wanavyolazimika kumsafisha Lowassa ndivyo wanavyozidi kuwa associated nae.
Sasa kazi ni kubwa na wananchi watawaona wote wako sawa in fact wagombea ubunge waliokuwa wanapiga vita ufisadi wataonekana hovyo na wanafiki
Nawasikitikia sana Ukawa ..
Kuhusu Jenerali na magazeti yake wao wanaandika kipi kibaya? Raia Mwema na Raia Tanzania inaandika hali halisi na ukweli, haijakaa kishabiki.
Acheni Ukawa kulalamika .. mlichokifanya ni kufuata mkakati bomu kabisa na litawalipukia muda si mrefu. Taratibu watanzania wanazinduka na wanatambua mlichokifanya. Mnapoteza credibility!
Na mnavyoendelea na matusi na kejeli mnazidi kuzama.
 
Nakubaliana na prof James Watson kuwa sisi watu weusi tuna uwezo mdogo sana wa kufikiri,ni wewe Jenerali Ulimwengu uliyewahi kutofautiana na serikali ya ccm kisa kuandika maovu yao,wakakupora uraia wako wakisema kuwa wewe si mtanzania na ukaanza kuishi ndani ya nchi yako kwa kulipia kibali,mtu uliyewahi kuwa mkuu wa wilaya unaambiwa si raia na uishi kwa kibali,sasa hivi unaipigia kampeni ccm iendelee kutawala wewe na mwenzako Mbwambo,huu ni unafiki wa hali ya juu kupindukia,leo ccm imekuwa nzuri kwako kwa lipi hasa? Hata kama padlocks ni best yako tambua kuwa ccm ni mfumo hata aje malaika awe rais kupitia ccm hakuna kitakachobadilika,tupo vitani kuhakikisha kuwa ccm inaanguka kwa gharama yoyote ile,unapokuwa vitani huwezi kuchagua silaha za kupigania,inapobidi unaweza kutumia silaha ya adui ili kushinda vita pindi ukifanikiwa kuiteka ndo maana tukamchukua Lowassa,Lowassa ni bomu la nyuklia ktk vita dhidi ya ccm na kwa hiyo lazima tushinde hii vita,wewe na wenzako mmetugeuka ktk battle field,hamfai kabisa.

Hivi haujui siri? Malocks na Ulimwengu wana asili moja! The birds of the same feathers fly together!
 
Nadhani UKAWA tuwe tayari kupokea mawazo tofauti na yetu na tuheshimu watu Jenerali Ana mawazo mazuri tuwe makini Sana mie nataka tuwe na uhakika na Nidhamu itawale

aseme achuje makala zake kabla ya kuzirusha magazetini, ama nae amepotea anasaliti
 
Nakubaliana na prof James Watson kuwa sisi watu weusi tuna uwezo mdogo sana wa kufikiri,ni wewe Jenerali Ulimwengu uliyewahi kutofautiana na serikali ya ccm kisa kuandika maovu yao,wakakupora uraia wako wakisema kuwa wewe si mtanzania na ukaanza kuishi ndani ya nchi yako kwa kulipia kibali,mtu uliyewahi kuwa mkuu wa wilaya unaambiwa si raia na uishi kwa kibali,sasa hivi unaipigia kampeni ccm iendelee kutawala wewe na mwenzako Mbwambo,huu ni unafiki wa hali ya juu kupindukia,leo ccm imekuwa nzuri kwako kwa lipi hasa? Hata kama padlocks ni best yako tambua kuwa ccm ni mfumo hata aje malaika awe rais kupitia ccm hakuna kitakachobadilika,tupo vitani kuhakikisha kuwa ccm inaanguka kwa gharama yoyote ile,unapokuwa vitani huwezi kuchagua silaha za kupigania,inapobidi unaweza kutumia silaha ya adui ili kushinda vita pindi ukifanikiwa kuiteka ndo maana tukamchukua Lowassa,Lowassa ni bomu la nyuklia ktk vita dhidi ya ccm na kwa hiyo lazima tushinde hii vita,wewe na wenzako mmetugeuka ktk battle field,hamfai kabisa.[/QUOTE.
Ww unataka aanze kuandika usafi wa el.ndo furaha yako acha mambo yako kila mtu muovu lazma vyombo vya habar viwambie ukweli wananchi..
 
Umeongea vyema kabisa lakini naamini kuwa hata ktk ubunge Ukawa mmepoteza sana kwani wagombea wanavyolazimika kumsafisha Lowassa ndivyo wanavyozidi kuwa associated nae.
Sasa kazi ni kubwa na wananchi watawaona wote wako sawa in fact wagombea ubunge waliokuwa wanapiga vita ufisadi wataonekana hovyo na wanafiki
Nawasikitikia sana Ukawa ..
Kuhusu Jenerali na magazeti yake wao wanaandika kipi kibaya? Raia Mwema na Raia Tanzania inaandika hali halisi na ukweli, haijakaa kishabiki.
Acheni Ukawa kulalamika .. mlichokifanya ni kufuata mkakati bomu kabisa na litawalipukia muda si mrefu. Taratibu watanzania wanazinduka na wanatambua mlichokifanya. Mnapoteza credibility!
Na mnavyoendelea na matusi na kejeli mnazidi kuzama.

Ni kweli kumsafisha Lowasa hadharani ni kazi kweli kweli hasa kwa kuwa yeye mwenyewe hataki hata kutamka neno FISADI! Nadhani timu ya kampeni ya Ukawa wako humu. Wamlazimishe lowasa kuokoka na kukemea ufisadi hadharani na atoe tamko kuwa atakuwa kama Zakayo wa biblia aliyeongoka na kurudisha Mali yote ya dhuluma. Lowasa alazimishwe kutamka mali zake zote hadharani na alivyozipata ndipo wagombea wetu wa ubunge na udiwani wataweza kuendeleza agenda ya kutokomeza ufisadi kwenye kampeni. Lowasa pia aseme wazi wazi kuwa ataitekeleza sera ya chadema ya kuwapeleka mafisadi wote mahakamani endapo atakuwa rais. Kama hana ujasiri huo Ukawa kwisha.
 
dilemma

Hakuna Mtanzania mwenye akili anayekubaliana na kauli eti TUIONDOE CCM KWA GHARAMA YOYOTE ILE . Huu ni ujinga mtupu. Ina maana hata kwa gharama ya kuisambaratisha nchi kama Somalia au Libya kwenu ni sawa ili mradi eti CCM imeng'olewa madarakani. Lowassa kweli ni bomu la nyuklia ila kamwe halitalipuka, labda litamlipukia mwenyewe afe yeye peke yake labda na Chadema yake kama lile bomu la kujitoa mhanga.
 
Last edited by a moderator:
Ndg zangu tusilalamike kama Lowassa ni fisadi twende mahakamani la sivyo sisi ndo wanafiki
 
Ndg zangu tusilalamike kama Lowassa ni fisadi twende mahakamani la sivyo sisi ndo wanafiki

Kampeni meneja wa Tingatinga Tafadhali chapisha hilo faili lote la Lowasa mnalosema ni kubwa sana liloko Takukuru ili watu watulize mawazo na kuanza kufikiri. Utaisaidia nchi isichafuke kwani wafuasi wake watamkimbia wakiuona ukweli.
 
yani team lowasa tatizo lao mtu akitofautiana nao kimawazo ni msaliti,katumwa, ana upeo mdogo kwenye kufikiri.. unafikiri wenye akili na ufahamu walifurahi na kupendezwa pale mlipomtukana full bright politician profesa lipumba, mkaendeleaa kwa zitto, mkaenda mbali zaidi hata mkamtukana slaa, juzi mkaanzisha matusi kwa POLEPOLE,. PROF KITILA na leo hapa unamtukana jeneral ulimwengu huyu ambaye thamani yake ktk uandishi ni hali ya juu... unachotakiwa kujuliuliza ni kwanini wasomi maprofesa na watu wenye uelewa mkubwa ktk mambo ya siasa na jamii wanampinga lowasa??? mwaka huu mtawatukana na kuwakashifu wengi wanaopingana na lowasa
 
Mandela alishirikiana na makaburu na wapinzani wake baada ya kuingia ikulu na siyo kabla. Kwa hiyo Mbowe amekosea kumkaribisha Lowasa na kumfanya mgombea wa chadema. Watu wenye akili za kutosha hawawezi kumpa Lowasa kura. Huyu mtu hana maadili na anatumia fedha kutafuta urais na hii ni Hatari. Nina hakika baada ya kampeni wengi wanaonfuata watabadilika na hawatampa kura. Ukawa turidhike na wabunge zaidi ya nusu ili kuithibiti serikali na Sera zetu na ilani yetu zitekelezwe na serikali itakayoundwa hata kama Tingatinga akiwa rais.

Usisahau kwamba Mandela alianza kujadiliana na makaburu tokea akiwa jela. Na mpangilio wa jinsi atakavyoachiwa na serikali itakavyokuwa waliafikiana kabla.

Halafu hii kauli ya kutaka CHADEMA waweke nguvu kwenye kuongeza wabunge ni mbinu mpya ya CCM kutaka kuendelea kuidhibiti Ikulu (penye kauli ya mwisho - alfa na omega).

Japo sijaona raha Lowasa kupokelewa CHADEMA lakini naamini kwa dhati kuwa wakati umefika wa JEURI YA CHAMA KIMOJA (the impunity) kuondolewa. Hatuwezi kuendelea na mfumo ambao watu wameaminishwa kuwa ni CCM tu ndiyo inaweza kuongoza nchi hii. Ndio maana vibaka, mafia na mafisadi wa kila aina wanakanyagana kupata nafasi za uongozi huko wakiamini ndiyo kinga ya maovu iliko: rejea kauli ya Sumaye alipokuwa WM kwa wafanyabiashara wakitaka mambo yao yawanyokee.

Kama EL atafanikisha kuiweka pembeni CCM, kwangu mimi itakuwa THE END JUSTIFIES THE MEANS. Na nitawapa heshima waliocheza mkakati huo. Kwa upande mwingine, naamini kabisa hiyo itatoa nafasi ya uhakika kwa CCM kujivua MAGAMBA; kuondokana na wapayukaji na kuwa chama bora sana.
 
Waambie hao! Ni kweli kwamba uandishi wa raia mwema na raia tanzania umebadilika kutoka kukemea maovu hadi kutetea mafisadi. Nadhani watakuwa wamenunuliwa na mafisadi (ccm).
Kumbe sera zao zinafanana na CDM, mbona hawajawa UKAWA?
 
Back
Top Bottom