Jenerali Ulimwengu, kumbe hata wewe ni mnafiki!

Jenerali Ulimwengu, kumbe hata wewe ni mnafiki!

Nakubaliana na prof James Watson kuwa sisi watu weusi tuna uwezo mdogo sana wa kufikiri, ni wewe Jenerali Ulimwengu uliyewahi kutofautiana na serikali ya CCM kisa kuandika maovu yao, wakakupora uraia wako wakisema kuwa wewe si mtanzania na ukaanza kuishi ndani ya nchi yako kwa kulipia kibali, mtu uliyewahi kuwa mkuu wa Wilaya unaambiwa si raia na uishi kwa kibali, sasa hivi unaipigia kampeni CCM iendelee kutawala wewe na mwenzako Mbwambo, huu ni unafiki wa hali ya juu kupindukia, leo CCM imekuwa nzuri kwako kwa lipi hasa?

Hata kama padlocks ni best yako tambua kuwa CCM ni mfumo hata aje malaika awe rais kupitia CCM hakuna kitakachobadilika,tupo vitani kuhakikisha kuwa CCM inaanguka kwa gharama yoyote ile, unapokuwa vitani huwezi kuchagua silaha za kupigania, inapobidi unaweza kutumia silaha ya adui ili kushinda vita pindi ukifanikiwa kuiteka ndo maana tukamchukua Lowassa, Lowassa ni bomu la nyuklia ktk vita dhidi ya CCM na kwa hiyo lazima tushinde hii vita,wewe na wenzako mmetugeuka ktk battle field,hamfai kabisa.

mtu akisema ukweli anakuwa mnafiki, watu wote hawawezi kuwa na mtazamo wa aina moja, ikiwa hvyo basi tutakuwa taifa la watu wapumbavu.
 
Waambie hao! Ni kweli kwamba uandishi wa raia mwema na raia tanzania umebadilika kutoka kukemea maovu hadi kutetea mafisadi. Nadhani watakuwa wamenunuliwa na mafisadi (ccm).
Huna kumbukumbu nzuri mkuu..tokea Lowassa alipokuwa akigombea kupitia CCM magazeti tajwa hayakuwa yakimuunga mkono kama ilivyokuwa kwa wafuasi wa vuguvugu la ukawa..Waandishi makini sio vinyonga kwamba wamkubali mtu yuleyule wanampinga kwa hoja wamkubali tu kisa kaingia upinzani tena ndani ya siku tatu huo utakuwa ujuha..wao wanasimamia misingi yao na sio ufuasi-malaya wa kugeuka na kufuata mkumbo bila ya kuwa na hoja msimamo..
 
Ulimwengu alikua mpiga debe mzuri tu Wa chadema kipindi cha slaa,lkn now chadema umebadilika sana guys,wengi wamejiweka nayo mbali,ijitakase,chadema ile siyo hii tunayoiona
 
Tatizo ni lowassa hata mkijaribu kulificha,RAIA mwema lilikataa kununuliwa na lowassa since akiwa ccm sio leo
 
The big picture ni kuiondoa CCM madarakani. Tukishatimiza hilo demokrasia ya kweli itakuwa imetua Tanzania (sio one party rule ya sasa hivi). We will look back then and think 'we did it'! The end justifies the means!
 
Duh, hawa ukawa ni hatari. Yaani mtu ukitofautiana nao kimawazo na kimtazamo eti wewe ni tahira!!!!!!!????? wanataka kutuaminisha kuwa eti Lowassa ni mtu safi kwa kuwa amehamia UKAWA???????????!!!!!!!!!!.
 
Ulimwengu alikua mpiga debe mzuri tu Wa chadema kipindi cha slaa,lkn now chadema umebadilika sana guys,wengi wamejiweka nayo mbali,ijitakase,chadema ile siyo hii tunayoiona

Bado wanahisi wako wamoja na wanadanganywa na wanaoingia wanasahau kwamba sahivi wasafi tunajiengua taratiibu alafu wachafu ndo wanaingia kwa makundi ..mwisho wa siku chama kinajaa walewale wachafu alafu tunaingia CCM kusafi
 
Nafikiri kuwa na mawazo tofauti ni afya katika majadiliano yoyote .Sioni sababu ya kumshambulia mtu kwa jina kisa mmetifsutiana msimamo.Hiki ni kipindi kigumu sisi kama wapiga kura tuangalie yupi atatuvusha hapa tulipo kama nchi uadilifu ni muhimu kuliko yote MH RAIS KIKWETE ALI WAHI KUSEMA AKILI ONGEZA NA ZAKO KAMA MBAYUYUWAYU NENDENI KICHWA KICHWA MEASURE KICHWA ...
 
Mandela alishirikiana na makaburu na wapinzani wake baada ya kuingia ikulu na siyo kabla. Kwa hiyo Mbowe amekosea kumkaribisha Lowasa na kumfanya mgombea wa chadema. Watu wenye akili za kutosha hawawezi kumpa Lowasa kura. Huyu mtu hana maadili na anatumia fedha kutafuta urais na hii ni Hatari. Nina hakika baada ya kampeni wengi wanaonfuata watabadilika na hawatampa kura. Ukawa turidhike na wabunge zaidi ya nusu ili kuithibiti serikali na Sera zetu na ilani yetu zitekelezwe na serikali itakayoundwa hata kama Tingatinga akiwa rais.

mkuu mandela alianza kushirikiana na makaburu kabla ya kutoka jela kwa lengo la kuokoa nchi ya afrika kusini iliyokuwa ikienda katika janga kubwa la vurugu za wenyewe kwa wenyewe,mazungumzo kati ya mandela na de klerk yalikuwa ya siri sana kiasi kwamba viongozi wakubwa wa anc hawakujua ,mandela alitumika kama mpatanishi kati ya waafrika wazawa na makaburu.
Mandela And De Klerk Hold Talks, Sources Say - philly-archives
 
Back
Top Bottom