Ulimwengu anaandika makala zake kwa nadharia na falsasa sana. Makala zake ni abstract sana, kiasi kwamba kama ni msomaji mgeni hutazipenda. Hii haijalishi ameandika kwa Kiswahili au Kiingereza. I can vouch for this guy-I have known him for a long time to know he is a true activist/reformist. Ni mmoja ya waandishi wachache wasiopelekeshwa na dini, ukada wala ukanda.
Yeye kama mmoja wa wamiliki wa Raiamwema ni mwandishi mkongwe wa habari na anajua sio busara na ni kinyume cha maadili ya uandishi kuwapangia wenzake cha kuandika. Na inafahamika toka enzi za Rai kuwa kuna baadhi ya waandishi wao 'akili zinahama' wakati wa uchaguzi na wamewahi kuliweka bayana. Mfano Maggid wa nyakati za uchaguzi ni tofauti na wa nyakati zingine zote. Wakati wa uchaguzi, yeye ni pro CCM.
Kwa upande wa Mbwambo, huyu nae ni mwanamageuzi asiyetetereka. Amekuwa na msimamo usioyumba kwenye kutetea mageuzi. 'Tatizo' lake, uanamageuzi wake umejikita kwenye misingi-sio pragmatist. Kiukweli, kwa wafia mageuzi na washabiki wa siasa za chadema, kumpokea Lowassa ilikuwa ngumu sana kwasababu anaenda kinyume na wengi wanachokiamini. Baada ya kuandika makala zaidi ya 20 za kuponda ufisadi na Lowassa, naweza kumuelewa akikataa kumeza matapishi yake.
Namuunga mkono Lowassa kwa sababu he is a real threat to CCM.Japo naunga mkono ukawa, nina wasiwasi (kama Mbwambo) na mstakabali wa baadae wa chadema. Rejea historia ya NCCR mageuzi. Baada ya NCCR kuzimia kisiasa, upinzani wa kweli na mhemuko wa siasa za upinzani ulipoa sana-hiki ndo wanamageuzi waliojikita kwenye misingi wanakihofia. Ukiondoa ajenda ya ufisadi, chadema itazimia kisiasa. Hata hivyo tumaini lipo kwenye idadi ya wabunge wengi wanaoweza kupata. Sina tatizo na Mbowe, ni mwanasiasa makini na mahiri, amefanya kile Mandela na ANC walikifanya-kuungana na adui (National party) kuunda serikali ili kujenga nchi na kusonga mbele. Historia itamhukumu Mbowe, kama ambavyo baadhi ya weusi wanamlaumu Mandela.
Ulimwengu ahishimiwe, ni mwanamageuzi na mwanaharakati nguli. Ni kama Dr. Slaa. Hatuwezi kuthubutu kuusahau mchango wake (kama tunajiheshimu) ktk mageuzi eti kwasababu tu haungi mkono kuja kwa Lowassa, hata kama tunampenda sana Lowassa.