Jen.Ulimwengu na Prof.Shivji

Watu wengi wanatabia ya kukurupuka linapotokea jambo ambalo ni muhimu kwao, tabia hii sio nzuri kwa wale great thinker. Wakati mjadala wa katiba mpya ulivyoanzishwa, Pr Shivji alikua ni among prominent figure ambao walisapoti idea ya katiba mpya, sasa kwa kua maoni ya wengi yalikua hayana uhakika nini hasa wanachokitaka ktk katiba mpya waliconclude tu kua ni swala zuri.

Hakuna anaepinga uhakika kua katiba mpya ni muhimu lakin ni bora tukajua kua katiba mpya inahitaji wataalam, gharama za kifedha na maoni ya wananchi.

Kinachoonekana ktk mijadala mingi ni kua wengi wanaojadili swala la katiba mpya, basi hata hiyo ya zamani hawajui inasemaje. Kwa kulizingatia hilo, kuna uwezekano mkubwa sana kua kushiriki kwao ktk kujadili swala zima la katiba kusiwe na maana yoyote zaidi ya kuwachanganya wananchi wa kawaida.

Ni vyema nafasi hii ikatumika kwa kuwafahamisha wengi kwanini tunataka katiba mpya pamoja na kuambatisha mifano kua katiba ya zamani inasemaje na tunataka ya sasa isemeje ktk specific matter.

Kwa mfano, kama utaangalia mkulima ambae kwa mwaka mzima anakuja mjini mara moja kutembea, concerns zake kuhusu katiba mpya ni tofauti na yule aliekua bungeni anatembelea shangingi.

Sasa, Kama katiba mpya inatakiwa ifaulu ni lazima izingatie mahitaji ya wote hawa. Tukiyafahamu hayo tuaweza kujua muda unaohitajika kulifanya hilo, umuhimu wa kulifanya hilo haraka na mengineyo.
 
Tatizo la Watz hawakumbuki na wala hawajipi shida ya kujua kuwa behinda the new const. Agenda, there is a hidden agenda
 
Kenya sio mbali na sisi,ni washirika wetu kwa karibu nyanja zote,hivi walipata katiba yao mpya baada ya maka migapi wakuuu???????
 
Jana wakati naangalia taharifa ya habari ya ITV saa mbili usiku nikakutana
na taharifa ambayo kidogo sikuielewa au ilinichanganya kumkichwa.
Eti Prof.shivji na Jen.ulimwengu walikuwa wanawaambia wahariri wa vyombo vya
habari kuwa hakuna haja ya kuharakisha mchakato au madai ya katiba mpya hadi
ilo swala liende kwa wananchi wote mijini hadi vijijini. wakimaanisha hata kama itachukua
miaka 10 au 15 wala si mbaya. Pia wakasema kuna wanasiasa wanaharakisha katiba mpya
ili waingie ikulu na kushika dola. Swali langu ni - kwanini watoe kauri hii sasa? ikizingatiwa
kila mwanchi ambae yuko active anataka katiba mpya hata hivi leo! pili najiuliza,kama hawa
ni watu walioendesha kongamano la katiba that day at UDSM inakuwaje leo waje na kauli kama hii? maana kauli kama hizi yapaswa kutolewa na watu wa CCM na si wapiganaji kama
Ulimwengu na Shivji. Au wameshatulizwa na ccm? mbona mnatukatisha tamaa jamani? My take - katiba tunataka leo na siyo kesho.

Kama kunasehemu nimekosea,tusameheyane wanaJF. - Nawasilisha

Kwa taarifa yako, hawa ni kati ya watu wachache ambao mikono yao haijachafuliwa na ufisadi na mara zote wanasimamia maslahi ya watu wa kawaida.

Ukiwasikiliza kiushabiki utatamani waunge mkono upande unaotaka wewe lakini haiwezi kuwa hivyo kwani wanasiasa wetu wa kizazi cha leo ni mafisi wanaogombania mfupa kila mmoja akitaka kukaa pale afaidi zaidi. Bado tuna safari ndefu kujinasua katika makucha ya MANYANG'AU!
 
Wakuu mi nafikiri tunakosea kidogo. Mimi nakubaliana na hawa wasomi. Kwa sababu zifuatazo.
1. Swala la katiba linatakiwa kuwa shirikishi na tuliendeshe sisi wenyewe watanzania.
.
Yeah, Shivji na Ulimwengu si Watanzania!
 
Tutakuwa na katiba ndani ya miaka mitano (proposed), 2011-2015
itajadiliwa na wananchi miaka mitatu (1 draft document), 2015-2018

tutatengeneza final draft (2 years), 2018-2020

kupiga kura ndiyo/hapana -2020

Kuanza kutumika 2021 au 2025
 
Kama kawaida yetu watanzania, hakuna haraka! Visingizio kwamba kuna watu wanataka kuingia ikulu kwa kutumia katiba mpya vinamlio mzuri masikioni!! Vinapendeza!

Hayo matrekta yanayochomwa, magari ya wawekezaji yanayopigwa kiberiti, ujambazi unaoendelea, kufeli kwa wanafunzi, wizi wa kura, kutokuwajibika kwa viongozi, wizi wa mali za wananchi, ajira isiyopatikana vyote vinaweza kusubiri miaka 15 mpaka 20. Ahsante sana Prof Shivji na Jenerali pamoja na wote wanaokubaliana nanyi. Watanzania tutasubiri! Tutasubiri huku huku vijijini enyi wa mjini mje mtuulize shida zetu ni nini ili tushirikiane nanyi kuandaa katiba mpya taratibu bila haraka!
 
Swala la KATIBA linatakiwa lianze swala la Utawala bora (uadilifu) kwanza, maana itakuwa kazi bure bila uadilifu
 
Tatizo kutafuta sifa na umaharufu wa kisiasa ndio itakacho haribu hii-momentum ya katiba mpya. Wengine tungependa kuona vitu muhimu kwetu kama sheria dhaifu na nguvu za raisi zinapunguzwa kwanza kabla ya kelele zingine zisizo na msingi.

Haya mambo ya kujifanya mnataka katiba wapelekewe wananchi UPINZANI ni kujiwekea kitanzi wenyewe coming 2015, na kama upinzani unaendelea na kelele hizi please msilalamike tena coming 2015. Chance mnayo ya kupigania vitu muhimu kwanza lakini sifa za kujifanya katiba sijui 'lelele hooh lelele' ndio itawafanya CCM wawape mnachokitaka katiba irudi kwa wananchi tusubiri miaka kumi mingine.

Wakati haki muhimu za wananchi zipo tayari kwenye katiba hila aziheshimiwi kisheria, viongozi wabadhirifu wanapeta, raisi matumizi yake haya ulizwi, mawaziri wanatuingiza mikataba kenge hawaulizwi, wauwaji wanapeta, kuna mijitu inakopa mabenki hawalipi, stimulus policies zisizo chunguzwa, NEC ni chombo cha raisi. Haya ni mambo muhimu wala haya husiani na wananchi na core problem on our constitution.

Lakini watu mnalazimisha vitu ambavyo vipo at the bottom of the agenda, halafu kesho mkipewa mnacholilia in this case katiba irudi kwa wananchi ambayo itachukua muda kuweka, kurekebisha na kuchukua vitu muhimu a decade already; not to mention most of those right already exist its just that they're not respected.

Kiasi jamaa waseme upinzani ni mavuvuzela.
 
Hasa kilichosemwa kwenye ITV jana ni kwamba, kazi ya kuandika katiba mpya siyo ya wanasiasa, na hasa siyo ya CHAMA TAWALA. Hili la chama kilichoshika dola kutojihusisha na uandikaji wa katiba ndicho nilichosikia JU akisisitiza na mimi nadhani nilielewa mantiki yake.

Kwamba chama kilichoshika dola mara zote kitapenda katiba isiyowapa wananchi mamlaka makubwa. Kwamba katiba tuliyonayo sasa ndivyo ilivyo na chama kilicho madarakani kinafurahia jinsi ilivyo. Nadhani hili liko wazi ukikumbuka jinsi CCM wamepinga kubadili vifungu vitakavyotoa uhuru zaid kwa wananchi,mfano tume ya uchaguzi.

Facts.

1. Chama tawala wana haki kama vyama vingine kushiriki kwenye mchakato mzima wa Katiba Mpya.

2. Wanachama binafsi wa kila chama na wasio na chama wana haki ya kushiriki kwenye mchakato mzima wa Katiba Mpya.

3. Wakati muafaka wa Katiba Mpya ulikuwa 1992. Wakati muafaka wa mchakato wa Katiba mpya SASA. Katiba inatakiwa kutmika lini? Kabla ya uchaguzi ujao.

4. NDIYO Katiba Mpya inatakiwa NA KARIBU WATU WOTE, na ndiyo inatakiwa kwa maslahi ya taifa zima wakiwemo watu na rasilimali zote.

Changamoto

1. Nani aongoze mchakato wote? a. Madaraka yanayotolewa na katiba ya sasa au vyama vya siasa. b. Tume ya Rais c. a na b.

2. Madhumuni ya katiba ni kukidhi matakwa na maslahi ya wananchi wote. Hapa tunatofautiana sana kuhusu matakwa na maslahi tunayoyataka kwa sababu tayari tuna matabaka yenye matakwa na maslahi tofauti.

3. Resources (rasilimali) kwa ajili ya mchakato mzima. Hili ni donda ndugu kwa sababu ya kukithiri maradhi ya rushwa ambayo yanakidhi maslahi ya wachache. Kwa hiyo adui rushwa anaweza akayumbisha mchakato mzima unless mkakati usiruhusu upuuzi huo.

Mawazo ya JU na Proff wakati wote ni mazuri sana; ila ni pungufu kwa sababu hayatoi mkakati mbadala wenye resources. Ndiyo maana ukiangalia hoja zao, muda utakaotumika kuwafikia wananchi kupata maoni unalingana na resources ambazo au hazipo au zitafujwa zikipataikana. Mbaya zaidi zinaweza zikachakachuliwa (uchakachuaji ni time framing ukizubaa umeliwa)

Maoni yangu mchakato wa katiba uchukue kasi sasa na uwe tayari 2013 ili uchaguzi ujao utumie katiba mpya kwa utaratibu uliopo kwenye katiba ya sasa ambao hauna gharama mpya.
 
Swala la KATIBA linatakiwa lianze swala la Utawala bora (uadilifu) kwanza, maana itakuwa kazi bure bila uadilifu

Nani anasimamia utawala bora? Kwangu mimi simuoni. Tunahitaji kuweka misingi ya uongozi kutokana na katiba mpya.
 
Ni kweli kabisa. lakini watanzania wanahitaji nini? kumbuka 1995, watanzania walijumuika na kuiunga mkono NCCR. na climax ilikuwa uchaguzi wa ubunge Temeke, ambapo serikali iliweka nguvu kubwa sana pale lakini Mrema akashinda. watanzania wengi wakawa wanaiangalia NCCR kwa leadership, iongoze mapambano. lakini kilichofuatia ni historia. NCCR ikasambaratika, na mwaka 2000 CCM ikajiimarisha na kushinda zaidi, baada ya watanzania kukata tamaa kwamba inawezekana kuwa na mapambano, wakasema bora zimwi likujualo! 2005 ndio kabisaaa!!!

Sasa ndugu yangu old generation inao wajibu wa kutoa mafundisho ya historia kwa young generation, ambao wanabeba banner ya mapambano hivi sasa. akina Shivji wamepambana tokea enzi za chama kimoja, mpaka leo. wamefundisha wengi tu, akina Jenerali Ulimwengu, na hata akina Tundu Lissu. tuwashukuru sana kwa huduma yao kwa taifa. hakuna kitu kibaya kama kuanza kwa jazba na kushindwa, au kuanza bila plan, tunahitaji plan A, plan B, na hata plan C. na watanzania wajue hilo. unapowasikiliza watu kama Jenerali Ulimwengu, Prof. Issa Shivji, inakubidi utafakari sana wanachosema. hawahitaji kusema kila kitu, lakini wanayosema yanabeba mengi.

Nadhani huduma nzuri kabisa ya JF kwa watanzania, ni kutoa uchambuzi wa plan mbalimbali za kwenda mbele. haitoshi tu kusema HAYA NA TUANZE MARA MOJA! tuanze kwa kufanya nini? Shivji anazungumzia hatua ya kwanza ya kujenga misingi ya kisiasa, ambayo ni kujadili katiba mpya katika maeneo mbalimbali. sawa, tusema tunayotaka yawepo, lakini pia tuseme misingi ya hiyo katiba mpya. na hili la misingi ndio la muhimu zaidi katika hatua hii.

Nakubali hawa wananchi wamecontribute vizuri katika issues tofauti lakini tusikubali kwamba kila kitu wanachosema ni correct. Hizi strategies za kuelimisha wananchi mpaka sasa zimefanyika na zimefakiwa kabisa. Mpaka leo tumshukuru Dr Slaa na Chadema kwa ujumla kwani kwa kutumia platform yao kipindi only six months wakati wa kampeni za uchaguzi waliwaelimisha wananchi jinsi ya Haki zao na jinsi gani CCM inaiumiza Taifa letu. Kitu tunachotaka wengi wananchi ni jinsi ya Kuunda kwa National Conference na Kuunganishwa kwa Vyama vyote vya kisiasa ili Kuzungumzia hili swala la Katiba Mpya. Sababu kubwa ya Kuunganisha na Kukutanishwa kwa Vyama Vyote vya kisiasa ni kwamba vyama ndivyo vinawakilisha maoni ya wananchi na hii process na solution is only through Political System. Waalimu wa vyuo na Wanasiasa wengine wanaoheshimika Tanzania ni muhimu sana kwa mawazo yao na tusikose kuwakosoa endapo watakosea hata kama walikuwa kwenye siasa miaka 80. Ulimwengu na Shivji wametoa comment kwamba "ichukue hata kama miaka kumi kusiwe na tatizo lolote kuunda Katiba" hii inamaana gani? Sidhani kama that is relevant concern here. Ulimwengu na Shivji tunategemea majibu na mchangi wao jinsi gani 1.) Taratibu/Process za Kuunda Tume ya Katiba - Jinsi ya kuwausisha wananchi wote 2.) Taratibu na kazi za Tume ya Katiba 3.) Taratibu za kukusanya Maoni ya Katiba 4.) Taratibu nzima za Kukamilisha Process nzima za Katiba - Upigaji kura wa Wananchi 4.) Tarehe za Kuhitimisha Process nzima ya katiba 5.) Tarehe ya Katiba Mpya Kuanza Kutumika Tanzania

Kuna hatari ya kutegemea Ulimwengu na Shivji kama solution ya kuundwa kwa Katiba na wakaja kuhijack the whole process na tukaja kuumizwa. Vitu vipo black and white hakuna kuhide the facts na kudance with comments kila leo. Just ushahuri...

"Tuendelee Kuelimishana Juu ya Katiba na JF inasaidia sana kutimiza hili zoezi"
 
Jamani, hebu tuelewe kwanza walichokisema hao wenzetu.Mimi nilikuwapo pale kwenye hilo kongamano, na ni kweli walizungumza hilo, lakini waliendelea kusema kuwa kuna baadhi ya sheria ambazo ziko nyeti sana, hizo kwanza lazima zibadilishwe kwa haraka kabla ya uchaguzi mkuu ujao huku wakiendelea kurekebisha katiba.Mimi nakubaliana nao sana.
Kuhusu suala la katiba mpya watanzania ni waoga sana na ni sura mbili.Wakati wa vuguvugu la kutaka katiba mpya na kuleta vyama vingi, nakumbuka vizuri sanamwaka 1990 wakati wanafunzi wa mlimani (ambao ni wasomi wetu) ndiyo walioanza kuchokonoa hayo kwa ajili ya kuleta mabadiliko na kuwatetea watanzania hasa wakulima na wafanyakazi,lakini badala yake watanzania wale wale waliwageukia wasomi wetu na kuwapiga mawe, ati kwamba wao walikuwa hawataki mabadiliko na kwamba watanzania walikuwa wake sawa.Nakumbuka vizuri sana namna watanzania wale wale walivyokuwa wanawapiga mawe wasomi wetu waliokuwa wanawatetea, wakati wakiwa kwenye vituo vya mabasi wakusubiri kupanda mabasi kuelekea vijijini kwao, baada mzee mwinyi kufunga chuo kikuu na kuwatukana wanafunzi na kuwaamuru warudi vijijini kwa, na pia baada ya kuwapa vitisho vya hali ya juu akina Prof. shivji, marehemu prof. Othman (RIP) na wengine.
Sasa hivi watanzania wanataka katiba mpya kwa HARAKA, ni hatari, lazima muone mbali ndugu zanguni, msifanye papara.
 
sijui matabularasa yatakwisha lini nchi hii!

yai na kuku lipi limetangulia?

suala la maadili ni moja, lakini katiba yenye kujenga msingi wa maadili ni jambo la muhimu kabisa.

kusema tuwe na maadili kwanza ni open ended...na isiwe kisingizio cha kutokuwa na katiba mpya.naheshimu mawazo ya JU na ni ya msingi kabisa lakini lipi litangulie na lini nadhani hapo atakuwa amekosea na hajatutendea haki wana wa nchi hii wanaoendelea kuteseka.

katiba ya marekani iliandikwa siku nyingi, na haikuandikwa na wananchi wote bali founding fathers kutoka states zote walifanya hiyo kazi wakifikiri miaka 100 mbele na si maslahi yao binafsi.

kama kweli tutakaa na kuweka fundamental principles ambazo zitaongoza hii nchi, hata pale ambapo tutakuwa na raisi mwendawazimu basi nchi hii isitetereke hata kidogo.

nchi ambapo mihimili na hata raisi anaiogopa bunge akifanya ushenzi

nchi ambapo mtumishi anajali kazi, na kazi ndio kipimo cha ujira wake

nchi ambapo mifumo ya fedha inakuwa huru na mikono ya wanasiasa

nchi ambapo serikali muda wote inafikiria ni jinsi gani ya kuwawezesha watanzania wazalishe ili nacho kiongeze uzio wa kodi

nchi ambapo serikali inakuwa na production arragement na watu wake badala ya kuwa na endless negotiation na world bank na imf

nchi ambapo serikali inawajali zaidi domestic investors badala ya huu uwendawazimu wa sasa

yako mengi...

hii ni tanzania tuitakayo

hii ndio katiba tunayoitaka

ni rejea ya yote tunapokwama

ndio itakuwa starting point ya kuwa na maadili ya taifa (foundation) na tuwe tunarejea kwenye katiba.

wananchi wanajua katiba.wanaua mapungufu.yale yote ambayo wanahisi wamenyimwa au wanakosa na hasa yale ya msingi(rejea kauli ya mnyika kwenye kongamano) bila kutaja neno katiba
 
Jamani, hebu tuelewe kwanza walichokisema hao wenzetu.Mimi nilikuwapo pale kwenye hilo kongamano, na ni kweli walizungumza hilo, lakini waliendelea kusema kuwa kuna baadhi ya sheria ambazo ziko nyeti sana, hizo kwanza lazima zibadilishwe kwa haraka kabla ya uchaguzi mkuu ujao huku wakiendelea kurekebisha katiba.Mimi nakubaliana nao sana.
Kuhusu suala la katiba mpya watanzania ni waoga sana na ni sura mbili.Wakati wa vuguvugu la kutaka katiba mpya na kuleta vyama vingi, nakumbuka vizuri sanamwaka 1990 wakati wanafunzi wa mlimani (ambao ni wasomi wetu) ndiyo walioanza kuchokonoa hayo kwa ajili ya kuleta mabadiliko na kuwatetea watanzania hasa wakulima na wafanyakazi,lakini badala yake watanzania wale wale waliwageukia wasomi wetu na kuwapiga mawe, ati kwamba wao walikuwa hawataki mabadiliko na kwamba watanzania walikuwa wake sawa.Nakumbuka vizuri sana namna watanzania wale wale walivyokuwa wanawapiga mawe wasomi wetu waliokuwa wanawatetea, wakati wakiwa kwenye vituo vya mabasi wakusubiri kupanda mabasi kuelekea vijijini kwao, baada mzee mwinyi kufunga chuo kikuu na kuwatukana wanafunzi na kuwaamuru warudi vijijini kwa, na pia baada ya kuwapa vitisho vya hali ya juu akina Prof. shivji, marehemu prof. Othman (RIP) na wengine.
Sasa hivi watanzania wanataka katiba mpya kwa HARAKA, ni hatari, lazima muone mbali ndugu zanguni, msifanye papara.

Mimi nachukua issue na hiyo statement hapo juu. Sijui kama Watanzania tunasubiri wazee vijijini na wasiosoma waongoze haya mapambano ya Katiba. We are wrong for this. Hatuwezi kusubiri mpaka bibi yangu na babu yangu kijijini aje kwenye ufahamu wa umuhimu wa Katiba na hasa nasisitizia wale wasio na kisomo-wengi wao ndani ya CCM. Taifa lote duniani leo hii democratic process inaongozwa na wale walio na vision ya Taifa liende wapi na kama tunataka kupoteza muda na kusibiri subiri hili ni Hatari zaidi. Vijana na wananchi wengi wasichukuliwe kama wanakupuruka na hawajui tunakwenda wapi na these kind of statements zinafanana kabisa na dharau iliopo kwa new generation. Kitu gani kama system na process ikitengenezwa na kuanza kusonga mbele haitafanikiwa? Sijaona sababu zozote zile zinazo zuia mafanikio. Whats are problems to have open and honest system now? Mpaka leo hii sijasikia list of disadvantages ya kutoanza hii process. Tusianze kuleta michakachuo hapa na tukijua enermy number moja ni to get rid of CCM failed systems...
 
Back
Top Bottom