Jen.Ulimwengu na Prof.Shivji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jen.Ulimwengu na Prof.Shivji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mshikachuma, Jan 29, 2011.

 1. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Jana wakati naangalia taharifa ya habari ya ITV saa mbili usiku nikakutana
  na taharifa ambayo kidogo sikuielewa au ilinichanganya kumkichwa.
  Eti Prof.shivji na Jen.ulimwengu walikuwa wanawaambia wahariri wa vyombo vya
  habari kuwa hakuna haja ya kuharakisha mchakato au madai ya katiba mpya hadi
  ilo swala liende kwa wananchi wote mijini hadi vijijini. wakimaanisha hata kama itachukua
  miaka 10 au 15 wala si mbaya. Pia wakasema kuna wanasiasa wanaharakisha katiba mpya
  ili waingie ikulu na kushika dola. Swali langu ni - kwanini watoe kauri hii sasa? ikizingatiwa
  kila mwanchi ambae yuko active anataka katiba mpya hata hivi leo! pili najiuliza,kama hawa
  ni watu walioendesha kongamano la katiba that day at UDSM inakuwaje leo waje na kauli kama hii? maana kauli kama hizi yapaswa kutolewa na watu wa CCM na si wapiganaji kama
  Ulimwengu na Shivji. Au wameshatulizwa na ccm? mbona mnatukatisha tamaa jamani? My take - katiba tunataka leo na siyo kesho.

  Kama kunasehemu nimekosea,tusameheyane wanaJF. - Nawasilisha
   
 2. M

  Mkodoleaji JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2011
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 454
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mshikachuma,
  Kweli mashaka uliyoyapata hata mimi niliyapata nilivyowasikiliza hawa magwiji jana. Lakini pia nikakumbuka jinsi Jenerali siku ya kongamano pale UDSM aliposema tuanze kujenga maadili kwanza kabla ya katiba mpya kwamba inawezekana hawa jamaa wanatumia umaarufu wao kuwapotezea wananchi focus ya katiba mpya. Kwa sababu maadili na Katiba inabidi viende pamoja na ni katika uandishi wa katiba mpya ndipo mnapoamua kuwa taifa la maadili gani. Kwa kweli hata mimi walinikatisha tamaa, yaani nilipenda niwapigie simu kuwaambia kama hamtaki katiba mpya basi afadhali mkae kimya.
   
 3. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #3
  Jan 29, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Sio akili yako...
   
 4. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #4
  Jan 29, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  washachakachuliwa hayo ni mawazo yao sisi ya kwstu ni matiba twaitaka leo
   
 5. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #5
  Jan 29, 2011
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,762
  Trophy Points: 280
  Wakuu mi nafikiri tunakosea kidogo. Mimi nakubaliana na hawa wasomi. Kwa sababu zifuatazo.

  1. Swala la katiba linatakiwa kuwa shirikishi na tuliendeshe sisi wenyewe watanzania.
  2. Watu wengi wa vijijini hawana habari au hawajui umuhimu wa kuwa na katiba mpya. Hivyo basi kwa sababu wengi ndo wapiga kura hatuna budi kuanzisha mchakato wa kutoa elimu ya uraia (hapa ndo NGOs na wengineo wafanye kazi zao). Hawa watu waeleweshwe kwamba mstakabali wa taifa letu uko mikononi mwao. Tusiwadharau kabisa kwa sababu hawana kisomo kama chetu wengi humu au wale wanaodai katiba. Kufanya hivyo (kitu ambacho CCM watapenda) itatufanya kurudi kule kule..wananchi hawaelewi kinachoendelea na ukifika uchaguzi wanatanguliza tumbo na maslahi binafsi mbele kupiga kura.
  3. Haraka haraka haina baraka (wenyewe wa pwani wanasema). Tunahitaji kujipanga na kujua tunataka kitu gani kwenye hiyo katiba mpya. Tusije ishia katika mazingira ya kutafuta marekebisho ya katiba kila baada ya mda mfupi.
  4. The constitution is bigger than politics and politicians. Inabidi tukae chini kama taifa tutafakari kwa kina ni jinsi gani tunaweza kupata katiba ya kutuvusha miaka mingine hamsini au mia. Mimi na wewe hatutakuwepo hapo! Hilo siyo jambo la kuamka na kuanza kulitekeleza bila utafiti wa kina.
  5. Najua wengi tunaumizwa na ufisadi, lakini hili la ufisadi kama tuna nia dhabiti twaweza kulitekeleza bila matatizo, ni swala la viongozi wetu kuwajibika. Kivipi? ndo hapo mpaka leo tunataka tuanzishe mchakato wa mazingira ambayo viongozi watawajibika kwetu wananchi na siyo kwa wahuni na majambazi akina Rostam Aziz na wapambe wao wachache.
  6. Tuache kabisa 'name calling'. Si vyema kila tukitofautiana mawazo kusema kwamba mtu kanunuliwa na CCM. Huu mchakato lazima tujue kabisa utakuwa mrefu na mgumu na watu wengi watakuwa na mawazo na matakwa tofauti. Swala si kutukanana na kuitana majina..ni kukaa chini na kujua kipi tunataka na tunaweza kufanikisha kama jamii moja ya Tanzania. Kesho wakitokea watu wanadai tuingize haki za mashoga kwenye katiba mpya..tusianze kuwatukana..bali tujenge hioja ni kwa nini hizo haki zao ziwemo au zisiwemo!

  7. Ushauri wangu wa mwisho, TUEPUKE HELA ZA WAFADHILI KWENYE HUU MCHAKATO. KWA YEYOTE ANAYEJUA ATHARI ZA HAWA WATU ATANIELEWA. WATATUPA HELA LAKINI WATATAKA TUWEKE AGENDA ZAO. YAANI NINGEOMBA WATANZANIA TUKUBALI HUU MCHAKATIO TUUGHARIMIE WENYEWE NA TUSIWAPE NAFASI HAWA JAMAA. Tutumie wataalamu wetu wa ndani kusudi tujenge kile kinachotufaa.
   
 6. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #6
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  katiba hii ndiyo inayotutesa, inatupa umaskini na wengine ubilionea haya ndiyo matabaka yalipo wengine wanaishi ahera ya duniani wengine pepo ya duniani. Sasa wakuu mnaposema tusifanye haraka mna maana gani -tusibiri wamalize rasilimali zote kwanza? Inafanana na alishika kaa la moto, au mwenye mzigo kg 100 kumwambia subiri tunafanya mpango wa kukupokea tunajua unaumia ila tunajipanga - a BAD JOKE!
   
 7. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #7
  Jan 29, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kaka masanja, nakubaliana na maoni yako mkuu! Lakini linapo kuja swala la kuipa mda
  serikali ya ccm kuhusu mchakato wa katiba ujue tumeumia! wanaweza chukua miaka 15 hadi 20.
  Sasa Je,kwa miaka hiyo tutakuwa wapi? si itakuwa tumepigika mpaka ubongo haufanyi kazi?
  Na Je, hawa mafisadi kwa kushirikiana na serikali hii chafu watakuwa wameiba tena kasi gani?
  Na mwisho tujiulize huyu Jen.ulumwengu na Shivji wameagizwa na nani kwenda kuliongelea hili
  kwa wahariri wa vyombo vya habari? maana wao si wanasiasa na si waajiriwa wa serikari ya chama
  tawala.
   
 8. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #8
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu unapokosea ni hapa: Unakuwa na haraka sana na hiyo katiba mpya.


  Taratibu, mambo mazuri yana taratibu zake na hayataki haraka. Cha msingi ni kuhakikisha mchakato wote hautekwi nyara na Serikali wala Bunge.
   
 9. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #9
  Jan 29, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,908
  Likes Received: 12,066
  Trophy Points: 280
  Kuna watu hapa wamejipanga kismati kufikisha ujumbe yetu macho ila hatudanganyiki.
   
 10. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #10
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Nadhani hapo ndipo tunapokosea Watanzania, kila kitu lazima kiingie kwenye siasa, hata mambo amabyo ni common sense kabisa, basi uamuzi wake utachukua miaka kwa sababu ya siasa

  Hiwezekani kwa kila mwanachi aandike katiba, kinachotakiwa kifanyike ni kuitishwa bunge la katiba na hao wanapewa jukumu la kuiandika hiyo rasimu ya katiba mpya (wakiwemo wadau kama viongozi wa dini, wasomi waliobebea km shivji, Safari nk), kisha baada ya hapo ndio inapitishwa kwa wananchi kutoa maoni yao, kama kuna marekebisho basi yanakuwa ni madogo kwa sababu waliyoandika hiyo Rasimu walikuwa ni wawkilishi wa maeneo tofauti
  Kama nchi ikiamua uchaguzi ujao ttutakuwa na Katiba Mpya kabisa
   
 11. s

  simanjiro Member

  #11
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  mi binafsi nishakusamehe, nakushauri utafute kumbukumbu za lile kongamano uzipitie upya, then hutauliza tena haya maswali!..... usichoke kujielemisha ndugu yangu!
   
 12. M

  Mindi JF-Expert Member

  #12
  Jan 29, 2011
  Joined: Apr 5, 2008
  Messages: 1,393
  Likes Received: 945
  Trophy Points: 280
  Alichosema Ulimwengu siku ya Kongamano UDSM ni kile kile alichosema hiyo jana. siku ile UDSM alikuwa anapingana na Mabere Marando kuhusu ajenda za vyama vya siasa katika suala la katiba mpya. nadhani ni muhimu katika jamvi kama hili la great thinkers, tukazingatia taratibu za majadiliano kwa Great thinkers. kwamba tujadili hoja. hoja ya msingi hapa ni kwamba katiba ni zaidi ya vyama vya siasa, ni zaidi ya taratibu za uchaguzi, ijapokuwa uchaguzi ni muhimu sana. tunataka katiba ambayo itawapa mamlaka wananchi kuibana serikali inayoundwa na chama chochote kile cha siasa. tukumbuke pia kwamba katika muktadha wa katiba mpya, inawezekana tukakubaliana kwamba mgombea binafsi ni halali, kwa hiyo inawezekana kabisa tukawa na rais ambaye hana chama chochote cha siasa! kwa hiyo hatuna haja ya kujifunga kabisa na chama chochote cha siasa, kiwe CCM, CHADEMA, NCCR, CUF, etc. hivi vyama vinaweza kugeuka, kama ilivyogeuka CCM, kama ilivyogeuka NCCR, na hata CUF, lakini taifa haliwezi kugeuka, maslahi ya taifa yako palepale. Ndiyo, kuna wakati CCM ilikuwa ni kweli chama cha wakulima na wafanyakazi wa Tanzania, lakini huwezi kutamka hivyo leo. Hata CHADEMA wanaweza kabisa kugeuka na kuwa chama maslahi, kama wasipopata changamoto za kutosha. tunahitaji mfumo ambao unaweza kudhibiti hata CHADEMA kama ikifanikiwa kuingia madarakani, ili watimize kile walichokuwa wanawakosoa wenzao CCM. lakini pia tunahitaji mfumo ambao hautaruhusu haya yanayotokea sasa hivi chini ya utawala wa CCM yarudiwe tena.

  Ndio maana Prof. Shivji alisema siku ile kwamba medani ya mamlaka katika taifa na uhalali wa uongozi enzi za Nyerere ilijengwa katika chama na ideology yake, na umahiri wa Nyerere. akafafanua kwamba medani ya mamlaka sasa hivi lazima isiwe tena kwenye chama bali katika katiba. kwa hiyo pamoja na kuvipenda vyama vyetu, tuhakikishe kwamba tunajenga utaifa juu ya vyama hivyo, na tusiruhusu tofauti zetu za vyama ziingilie utaifa wetu. wamarekani wakiwa na national issues, u-GOP na udemocratic unawekwa kando.

  lakini kuna hoja nyingine ya msingi. hatuwezi kuleta mabadiliko Tanzania kwa kuandika humu JF. ni kweli tunaweza kuelimishana, lakini ni asilimia ngapi ya watanzania wanaingia humu jf? Tunahitaji watanzania waweze kuwa na uelewa wa masuala yao ya kitaifa, kiasi cha kuweza ku-stage a formidable force against the government. kwa sasa hivi, haya yanayotokea Tunisia na Misri sio rahisi kutokea hapa Tz, kwa sababu hatujatengeneza critical mass ya kutosha ya watanzania kuweza kutamka HAPANA na kubaki na msimamo huo. hiki ndio kitu ambacho hata CCM hawakitaki kabisa. an Informed populace. wanainvest katika ujinga na ubangaizaji, na woga. hayo tunaweza kuyafikia kama tutafanya kazi ya ziada kuelimishana kwa njia mbalimbali. hapo tena sio suala la kuchelewa kupata katiba, bali ni suala la kujiandaa kwa mapambano. kama ukiingia katika mapambano na serikali, hasa za kifisadi kama hizi zetu, bila maandalizi, bila good mobilisation, utawakumbuka mababu zetu waliopigana Majimaji
   
 13. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #13
  Jan 29, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  mkuu, kwa bahati nilitazama hii habari unayoinukuu hapa. Pia imekuwa bahati kuna thread nyingine hapa ina clip ya hotuba ya JU pale Nkurumah. Nimeisikiliza pia kwa sababu sikuwepo Dsm wakati wa kongamano la katiba.

  Sikumbuki kusikia JU kusema haya uliyoyaandika. Kama alisema, tafadhali uniwie radhi kama akili yangu imekuwa duwanzi kiasi hicho.

  Hasa kilichosemwa kwenye ITV jana ni kwamba, kazi ya kuandika katiba mpya siyo ya wanasiasa, na hasa siyo ya CHAMA TAWALA. Hili la chama kilichoshika dola kutojihusisha na uandikaji wa katiba ndicho nilichosikia JU akisisitiza na mimi nadhani nilielewa mantiki yake.

  Kwamba chama kilichoshika dola mara zote kitapenda katiba isiyowapa wananchi mamlaka makubwa. Kwamba katiba tuliyonayo sasa ndivyo ilivyo na chama kilicho madarakani kinafurahia jinsi ilivyo. Nadhani hili liko wazi ukikumbuka jinsi CCM wamepinga kubadili vifungu vitakavyotoa uhuru zaid kwa wananchi,mfano tume ya uchaguzi.

  Kwa ujumla alituasa kwamba tusikubali chama tawala kiwe mstari wa mbele eti kinataka kutuletea katiba mpya. This is not in their interest and given the opportunity they will prolong it as long as they wish or watuletee katiba mbovu kuliko hiyo iliyopo.

  Kama ulishawahi kushiriki katika Public Hearing ya Muswada wowote ule utakuwa umemuelewa JU mpaka nukta ya mwisho. Kwenye public hearing ya mswada, wadau huja na mawaszo mazuri sana ya kuboresha sheria husika. baada ya kutoa maoni yale, hukusanywa na katibu wa kamati. Kamati hukaa kuamua nini wakubaliane nacho na nini wasikubaliane nacho. Kisha watendaji wa wizara na Waziri pia huamua nini wakubaliane nacho na nini wasikubaliane nacho. Mwisho wa siku, inaweza kuwa mlitoa mawazo mazuri sana lakini ama yasiingizwe kwenye Muswada, au yakaingizwa kwa lugha ambayo imechakachuliwa kiasi kwamba inakuwa mbaya kuliko kama yasingeingizwa.

  Nadhani hata Shivji alikuwa na mtazamo kama wa JU. Mimi nawaunga mkono wote wawili
   
 14. safariwafungo

  safariwafungo Senior Member

  #14
  Jan 29, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 136
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  kimsingi suala la katiba mpya kuwepo mara baada ya kufumbua macho mimi nakubaliana na jambo hilo kwa asilimia mia kwa mia lakini yapaswa kutambua hii ni among of many variable katika equation hii ya kutafuta katiba mpya na yapaswa vile vile kukumbuka katiba mpya si ya watu wa Dar es Salaam, Mwanza na Arusha la hasha ni ya watanzania wote hadi wa kule twatwata na kintiku. Kwa maoni yangu natarajia katiba mpya iwe implementable sasa ili kuhakikisha there is implementability of our New Katiba tunahitaji consensus za watanzania wote kwa uwingi wao na makundi yao katika jamii ambayo bila shaka yanatofautiana kwa namna furani. Kwa msingi huu itahitajika mchakato tuupeleke mpaka kwenye grass root ambapo natarajia tuwe na public hearing nyingi za kutosha kiasi tufikie hatua tukubali kukubaliana na kutofautiana ili kuweza kufikia consensus ya mambo muhimu kama watanzania ambayo tunahisi ni vyema yakamulikwa na katiba mpya. Nachelea kuamini kwamba michakato inayo fanywa Dar na miji mingine kuwa ndio suluhisho la kupata mapendekezo yenye tija la hasha natarajia tufanye mchakato huu kwa ujumla wetu kama watanzania na wala si kazi ya Prof Shivji, Gen Ulimwengu, CCM, CUF, CDM ama NGO fulafulani la hasha ni letu sote waTZ sasa kama tukikubaliana katika hili ni dhari mchakato wa haraka kwa mantiki ya kufumbua macho tunaona katiba mpya utanyima haki kwa waliowengi na mwisho wa siku tutapata katiba ambayo haitekelezi since haikupatikana kwa njia ya maridhaiano ya watanzania wote kwa ujumla. Jambo la msingi hapa ni kuona utayali wa viongozi wetu kiutashi na kivitendo katika kuratibu upatikana wa katiba mpya katika msingi itakayo pelekea kuwa nakatiba iliyotokana na maridhiano ya watanzania kwa ujumla wetu. Ya paswa wale wote watakao leta mchezo katika mchakato huu tuwaadhibu kama watanzania. This is how i see this thing in multi dimension!
   
 15. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #15
  Jan 29, 2011
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Ni kama kawaida,
  Mijadala kama hii ambayo CCM hawaipendi, ikianza tu, Unajikuta kuna stoog weeengi sana.

  Shivji ni nani na Ulimwengu ni nani hata watueleze mchakato wa katiba kuchukuwa zaidi ya miaka 5? Waache walambe viatu vya CCM maana wengine wanaona Rais huyu ndo aliwaokoa na makucha ya Mkapa, lakini siamini kama kuna darasa la katiba ktk nchi hii.

  Darasa lenyewe la nchi nzima, milioni 40. Je, wasipoelewa! hakuna Katiba! Kushirikishawa ni muhimu lakini muda unaotajwa ni wa ki-zembe. Hii siyo study ya PhD.

  Kinachohitajika ni kuainisha mapungufu ya katiba iliyopo. Mapungufu yapelekwe kwa wananchi kuwaeleza kwamba tunataka katiba iwe hii kwa sababu hizi na faida hizi. Elimu kama hiyo haihitaji kutembelewa watu vijijini. Weka nusu saa ya ya vipindi kwenye TBC yao, FM radio zetu na TV zote. Yaani hata hili tuzunguke nchi nzima kama ule ujinga wa vyama vingi au kimoja!

  Baada ya hapo mambo mengine yaendelee. Au wanataka kura ya maoni?
   
 16. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #16
  Jan 29, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Wakuu safari ya fungo,Gurudumu na Mindi,kwa ujumla nakubaliana na ninyi na
  ahsante kwa kunielewesha baadhi ya mambo. Lakini ninaposhindana na ninyi ni
  kule kukubali neno TUSIWE NA HARAKA YA KATIBA MPYA. ccm ukishawatamkia hivi
  ujue umewapa mwanya wa kuikumbatia katiba hii ya sasa hata kwa miaka 40 huku tukizidi kuteseka.
  Binafsi naunga mkono ndiyo tusiwe na haraka,lakini nilipenda uchaguzi ujao tuwe na katiba mpya.
  Hivi miaka 2 au 3 haitoshi kutuelimisha sisi wananchi?
   
 17. T

  Topical JF-Expert Member

  #17
  Jan 29, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Haitakiwi ichukue more than 5 years from now!

  Itakapofika 2015, tufanye uchaguzi chini ya katiba mpya kabisa,
   
 18. safariwafungo

  safariwafungo Senior Member

  #18
  Jan 29, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 136
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  mkuu nina omba kutofautia hapo kwenye red, observation yangu ya kwanza ni nani mwenye kuainisha mapungufu ya katiba iliyopo, kwa mujibu wa maelezo yako it seems there is a certain group of people who will analyze the weak point ya katiba iliyopo sasa. Hilo genge nani ataliteua kufanya hivyo na je is it a truly representative if tanzanian community. From that observation i beg to differ with your suggestion instead nafikiri itakuwa ni jambo la busara analysis hizo za mapungufu ya katiba na nini kiborweshe ama kiongezwe ni vyema yakafanyika kupitia public hearing na si kwa genge la jamaa furani wakajifungia kwenye kachumba furahi wakajifanya wanafanya brainstorming then watuletee yale kwayo wataona sahihi. Ni vyema tukafahamu kuwa mjini sio maana yake ndio unajua mengi la hasha, inawezekana waliopo huko madongo kuinama wakawa na hoja nzito na za msingi ambazo ni vyema zikawekwa katika katiba. Tusichukulie suala la katiba mpya kama vile suala la msongamano barabarani jijini Dar es salaam ambalo linachukuliwa kama ndo tatizo la msingi la watanzania la hasha tunaitaji kila mwenye kuweza kupaza sauti na apaze kwani katiba mpya naye itamuathiri otherwise tuwe na katiba za sehumu kama Dar na maeneo mengine yote ya mijini halafu na sisi wa kijijini mutuandalie ya kwetu. Ukweli ni kwamba tunaotofauti kubwa ya mahitaji kutokana na mazingira tuliyopo hivyo kama tunahitaji kuandaa katiba kwa ajiri ya watanzania kwa ujumla wao yatupasa tumpe kila mwenye uwezo wa kupata fursa aweze kutoa maono yake na tuyazungumze kwa ujumla wake katika selected public hearing place all over the country otherwise kama unataka haya tuyaache it means you have got a certain interest which you want to overlook other things which might be critical one.

  another observation is from; Yaani hata hili tuzunguke nchi nzima kama ule ujinga wa vyama vingi au kimoja!. Mkuu yatupasa kuwa makini katika hili, kwa kuwa mabadiliko ya katiba is inevitable bila shaka kila mtanzania yampasa kushiriki katika mchakato huu sasa wewe unafikiri kila mmoja anauwelewa mzuri kama wewe? Kimsingi katiba mpya inatakiwa iwe inatekelezeka na ili kuhakikisha inatekelezeka yatupasa kujumuisha kila mmoja kwa namna yoyote ile itakavyo wezekana. Ni hayo tu yangu maoni.
   
 19. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #19
  Jan 29, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  haraka haraka ya katiba mpya inaweza kuleta athari zaidi...
  ni bora taratibu.....
   
 20. J

  JokaKuu Platinum Member

  #20
  Jan 29, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,777
  Likes Received: 5,000
  Trophy Points: 280
  ..kilio cha Katiba mpya hakijaanza leo.

  ..kuna wanaodai kilianza miaka ya 90 wakati wa vuguvugu la kuanzishwa kwa vyama vingi. wako wengine wanadai kilio hicho kilianza kabla ya hapo.

  ..lets assume madai haya yalianza mwaka 1990. kwa hiyo mpaka leo hii ni miaka 21. sasa ina maana Shivji na Ulimwengu wanataka tuongeze miaka mingine 10 au 15?!!

  ..kwa msingi huo suala la katiba litakuwa limechukua miaka 31 mpaka 36 kupatiwa ufumbuzi, na Prof.Shivji na Ulimwengu are ok with that.

  ..sikubaliani na maoni ya Prof.Shivji na Jenerali Ulimwengu. suala hili naomba lishughulikiwe haraka na liwe limepatiwa ufumbuzi ndani ya miaka isiyozidi mitatu.
   
Loading...