Wakuu safari ya fungo,Gurudumu na Mindi,kwa ujumla nakubaliana na ninyi na
ahsante kwa kunielewesha baadhi ya mambo. Lakini ninaposhindana na ninyi ni
kule kukubali neno TUSIWE NA HARAKA YA KATIBA MPYA. ccm ukishawatamkia hivi
ujue umewapa mwanya wa kuikumbatia katiba hii ya sasa hata kwa miaka 40 huku tukizidi kuteseka.
Binafsi naunga mkono ndiyo tusiwe na haraka,lakini nilipenda uchaguzi ujao tuwe na katiba mpya.
Hivi miaka 2 au 3 haitoshi kutuelimisha sisi wananchi?
Alichosema Ulimwengu siku ya Kongamano UDSM ni kile kile alichosema hiyo jana. siku ile UDSM alikuwa anapingana na Mabere Marando kuhusu ajenda za vyama vya siasa katika suala la katiba mpya. nadhani ni muhimu katika jamvi kama hili la great thinkers, tukazingatia taratibu za majadiliano kwa Great thinkers. kwamba tujadili hoja. hoja ya msingi hapa ni kwamba katiba ni zaidi ya vyama vya siasa, ni zaidi ya taratibu za uchaguzi, ijapokuwa uchaguzi ni muhimu sana. tunataka katiba ambayo itawapa mamlaka wananchi kuibana serikali inayoundwa na chama chochote kile cha siasa. tukumbuke pia kwamba katika muktadha wa katiba mpya, inawezekana tukakubaliana kwamba mgombea binafsi ni halali, kwa hiyo inawezekana kabisa tukawa na rais ambaye hana chama chochote cha siasa! kwa hiyo hatuna haja ya kujifunga kabisa na chama chochote cha siasa, kiwe CCM, CHADEMA, NCCR, CUF, etc. hivi vyama vinaweza kugeuka, kama ilivyogeuka CCM, kama ilivyogeuka NCCR, na hata CUF, lakini taifa haliwezi kugeuka, maslahi ya taifa yako palepale. Ndiyo, kuna wakati CCM ilikuwa ni kweli chama cha wakulima na wafanyakazi wa Tanzania, lakini huwezi kutamka hivyo leo. Hata CHADEMA wanaweza kabisa kugeuka na kuwa chama maslahi, kama wasipopata changamoto za kutosha. tunahitaji mfumo ambao unaweza kudhibiti hata CHADEMA kama ikifanikiwa kuingia madarakani, ili watimize kile walichokuwa wanawakosoa wenzao CCM. lakini pia tunahitaji mfumo ambao hautaruhusu haya yanayotokea sasa hivi chini ya utawala wa CCM yarudiwe tena.
Ndio maana Prof. Shivji alisema siku ile kwamba medani ya mamlaka katika taifa na uhalali wa uongozi enzi za Nyerere ilijengwa katika chama na ideology yake, na umahiri wa Nyerere. akafafanua kwamba medani ya mamlaka sasa hivi lazima isiwe tena kwenye chama bali katika katiba. kwa hiyo pamoja na kuvipenda vyama vyetu, tuhakikishe kwamba tunajenga utaifa juu ya vyama hivyo, na tusiruhusu tofauti zetu za vyama ziingilie utaifa wetu. wamarekani wakiwa na national issues, u-GOP na udemocratic unawekwa kando.
lakini kuna hoja nyingine ya msingi. hatuwezi kuleta mabadiliko Tanzania kwa kuandika humu JF. ni kweli tunaweza kuelimishana, lakini ni asilimia ngapi ya watanzania wanaingia humu jf? Tunahitaji watanzania waweze kuwa na uelewa wa masuala yao ya kitaifa, kiasi cha kuweza ku-stage a formidable force against the government. kwa sasa hivi, haya yanayotokea Tunisia na Misri sio rahisi kutokea hapa Tz, kwa sababu hatujatengeneza critical mass ya kutosha ya watanzania kuweza kutamka HAPANA na kubaki na msimamo huo. hiki ndio kitu ambacho hata CCM hawakitaki kabisa. an Informed populace. wanainvest katika ujinga na ubangaizaji, na woga. hayo tunaweza kuyafikia kama tutafanya kazi ya ziada kuelimishana kwa njia mbalimbali. hapo tena sio suala la kuchelewa kupata katiba, bali ni suala la kujiandaa kwa mapambano. kama ukiingia katika mapambano na serikali, hasa za kifisadi kama hizi zetu, bila maandalizi, bila good mobilisation, utawakumbuka mababu zetu waliopigana Majimaji
lishughulikiwe haraka kama wote tnakubaliana
na katiba mpya iwe vipi....
sasa tatizo ni kuwa wengi hawajui na wengi zaidi wanahitai kuelimishwa
binafsi nakubaliana na maoni ya Generali Ulimwengu, ni bahati mbaya mleta mada hukumwelewa. Alichosema ni kwamba katiba si ya vyama vya siasa au kwa ajiri ya kukitoa chama fulani madarakani kwani hata katiba iliyopo inaweza kukitoa chama tawala madarakani kama tulivoona ktk uchaguzi uliopita. Kuhusu ushiriki wa wananchi, Prof. Shivji alisema ni muhimu kushirikisha watu wote na si kundi la watu wachache na hapo ndo alipogusia issue ya kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa katiba bora. Sasa hapo hawa maguru wamepotoka wapi? Tatizo kuna baadhi ya watu hapa JF wanafikiri tunataka katiba mpya kwa ajiri ya chama fulani kuingia madarakani! Tuache ushabiki jamani...hautotusaidia katika mambo ya msingi kama haya!
wakuu mi nafikiri tunakosea kidogo. Mimi nakubaliana na hawa wasomi. Kwa sababu zifuatazo.
1. Swala la katiba linatakiwa kuwa shirikishi na tuliendeshe sisi wenyewe watanzania.
2. Watu wengi wa vijijini hawana habari au hawajui umuhimu wa kuwa na katiba mpya. Hivyo basi kwa sababu wengi ndo wapiga kura hatuna budi kuanzisha mchakato wa kutoa elimu ya uraia (hapa ndo ngos na wengineo wafanye kazi zao). Hawa watu waeleweshwe kwamba mstakabali wa taifa letu uko mikononi mwao. Tusiwadharau kabisa kwa sababu hawana kisomo kama chetu wengi humu au wale wanaodai katiba. Kufanya hivyo (kitu ambacho ccm watapenda) itatufanya kurudi kule kule..wananchi hawaelewi kinachoendelea na ukifika uchaguzi wanatanguliza tumbo na maslahi binafsi mbele kupiga kura.
3. Haraka haraka haina baraka (wenyewe wa pwani wanasema). Tunahitaji kujipanga na kujua tunataka kitu gani kwenye hiyo katiba mpya. Tusije ishia katika mazingira ya kutafuta marekebisho ya katiba kila baada ya mda mfupi.
4. The constitution is bigger than politics and politicians. Inabidi tukae chini kama taifa tutafakari kwa kina ni jinsi gani tunaweza kupata katiba ya kutuvusha miaka mingine hamsini au mia. Mimi na wewe hatutakuwepo hapo! Hilo siyo jambo la kuamka na kuanza kulitekeleza bila utafiti wa kina.
5. Najua wengi tunaumizwa na ufisadi, lakini hili la ufisadi kama tuna nia dhabiti twaweza kulitekeleza bila matatizo, ni swala la viongozi wetu kuwajibika. Kivipi? Ndo hapo mpaka leo tunataka tuanzishe mchakato wa mazingira ambayo viongozi watawajibika kwetu wananchi na siyo kwa wahuni na majambazi akina rostam aziz na wapambe wao wachache.
6. Tuache kabisa 'name calling'. Si vyema kila tukitofautiana mawazo kusema kwamba mtu kanunuliwa na ccm. Huu mchakato lazima tujue kabisa utakuwa mrefu na mgumu na watu wengi watakuwa na mawazo na matakwa tofauti. Swala si kutukanana na kuitana majina..ni kukaa chini na kujua kipi tunataka na tunaweza kufanikisha kama jamii moja ya tanzania. Kesho wakitokea watu wanadai tuingize haki za mashoga kwenye katiba mpya..tusianze kuwatukana..bali tujenge hioja ni kwa nini hizo haki zao ziwemo au zisiwemo!
7. Ushauri wangu wa mwisho, tuepuke hela za wafadhili kwenye huu mchakato. Kwa yeyote anayejua athari za hawa watu atanielewa. Watatupa hela lakini watataka tuweke agenda zao. Yaani ningeomba watanzania tukubali huu mchakatio tuugharimie wenyewe na tusiwape nafasi hawa jamaa. Tutumie wataalamu wetu wa ndani kusudi tujenge kile kinachotufaa.
Jana wakati naangalia taharifa ya habari ya ITV saa mbili usiku nikakutana
na taharifa ambayo kidogo sikuielewa au ilinichanganya kumkichwa.
Eti Prof.shivji na Jen.ulimwengu walikuwa wanawaambia wahariri wa vyombo vya
habari kuwa hakuna haja ya kuharakisha mchakato au madai ya katiba mpya hadi
ilo swala liende kwa wananchi wote mijini hadi vijijini. wakimaanisha hata kama itachukua
miaka 10 au 15 wala si mbaya. Pia wakasema kuna wanasiasa wanaharakisha katiba mpya
ili waingie ikulu na kushika dola. Swali langu ni - kwanini watoe kauri hii sasa? ikizingatiwa
kila mwanchi ambae yuko active anataka katiba mpya hata hivi leo! pili najiuliza,kama hawa
ni watu walioendesha kongamano la katiba that day at UDSM inakuwaje leo waje na kauli kama hii? maana kauli kama hizi yapaswa kutolewa na watu wa CCM na si wapiganaji kama
Ulimwengu na Shivji. Au wameshatulizwa na ccm? mbona mnatukatisha tamaa jamani? My take - katiba tunataka leo na siyo kesho.
Kama kunasehemu nimekosea,tusameheyane wanaJF. - Nawasilisha
Binafsi nina vitu vingi sana ninavyopendelea viwepo kwenye katiba mpya.
Ila hapa nitataja vichache tu
1. Tume ya uchaguzi isiteuliwe na Rais
2.Mawaziri wapatikane kupitia bunge na si kuteuliwa na Rais
3.Mda wa Rais kukaa madarakani iwe ni miaka 4 tu,atakaa miaka 8 iwapo atashinda
uchaguzi unaofuatia.
4.Kiongozi yeyote wa juu serikalini akikutwa na utajiri alioupata kwa kuliibia Taifa
anyongwe hadi kufa au afungwe jela miaka 100 au zaidi.
Ni hayo kwa sasa, nawaachia wengine kuongezea hiyo list
Hata mie najiuliza Kenya walichukua mika 10 au 20? walitembelea vijiji vyote?
Jamani wananchi tunahitaji katiba mpya before next election 2015.
Pamoja na tofauti zetu katika kuchangia maada hii, inaelekea sote tunakubaliana kimsingi, ulazima wa kutungwa kwa Katiba mpya. Hata hivyo, tatizo linaloweza kutukabili baadaye; kama hatukutahadhari; ni namna ya kuwalazimisha watawala wetu kuiheshimu Katiba hiyo. Mathlani, pale inapothibitika kwamba uongozi wetu wa ksiasa hauipi katiba hiyo nguvu za kisheria kama inavyostahili, Raia atafanyaje kurekebisha hali hiyo?
Kuna watu hapa wamejipanga kismati kufikisha ujumbe yetu macho ila hatudanganyiki.
My Take, Ulimwengu na Shivji ni wananchi na raia kama mimi na wewe na kuzungumza kwao na mawaiza yao sio yana represent nchi nzima na kwenda mbele kwenye swala la Katiba wanajitoa wao wenyewe. Nashukuru tunawafahamu Nani yupo upande wa wananchi na nani anaweza kutumiwa na CCM wakati huu. This is generational thing...old generation hawajui kabisa nini vijana/new generation want and they are not listerning...it's coming realy soon.