Image caption Jehovahs Witness latuhumiwa kuharibu ushahidi
Aliyekuwa mzee wa kanisa la Jehovahs Witness nchini Uingereza ameelezea wasiwasi wake kuwa kanisa hilo limeharibu stakabadhi muhimu katika uchunguzi unaoendelea kuhusu dhulma za kingono kwa watoto nchini uingereza.
John Viney, ambaye mwanawe wa kike alidhulumiwa kimapenzi na muumini wa kanisa hilo ameiandikia jopo inayochunguza madai hayo, kuwa makao makuu ya kanisa hilo nchini Marekani, yaliwaagiza viongozi wa kanisa hilo nchini Uingereza kuharibu stakabadhi zote kuhusu watu binafsi na mikutano.
Kanisa hilo linasema agizo la kuharibu stakabadhi hizo ziliambatana na mahitaji ya jopo la uchunguzi huo, na kusema hawakuwa wanaficha jambo lolote.