Jeffery Samson Mkuki: Msomi wa Chuo Kikuu anayehangaika kijijini bila ajira

Best Sky Eclat nilikutana na wadada watatu Dar mwezi February mwaka huu ni waajiriwa wa TTCL. Wanapita nyumba kwa nyumba kujaribu kuongeza wateja wa TTCL na wanalipwa kwa commission.

Wote hao ni graduates wa UDSM na walijipinda hasa chuoni ili kupata honours kwa kujua zingewasaidia kupata ajira za maana.

Mara nyingi tu hawapati wateja wapya au mmoja hadi watatu kwa siku labda siku moja au mbili kwa wiki. Usafiri ni juu yao na bado wana gharama nyingine za kila siku za maisha.

Na marafiki zao wengi waliomaliza nao bado wanasaga lami/vumbi. Inasikitisha sana hali ya ajira nchini kusema kweli.
Ukiliongea hili unaitwa mchochezi best
 
Mpwa wangu alifaulu kwenda kidato cha V, shughuli ya kununua godoro, jembe, ndoo, sanduku ilikuwa mtihani. Aliwambia ndugu waache tu. aliamua kuwa mkulima.

Sasa hivi ana nyumba ya vyumba vitatu vya kulala ilijengwa kwa matofali ya kuchoma na kuezekwa kwa mabati, Ana mbuzi 100, shamba anapanda mahindi, mabamia yanampatia 10,000 kila siku asubuhi.
Maisha hayataki kujishika,uwe na elimu au usiwe nayo lazima upamabane bila ya kukubali kurudi nyuma,lakini all in all mtangulize Mungu katika kila jambo...
 
Ulisema waliofungua chuo boss...chuo kilifunguliwa back in 2007

Sikujua unamaanisha hata waliomaliza 2013 pia wamefungua chuo.
Mkuu chuo hakijengwi mwaka mmoja. That's why nikakwambia tena... in the context ya maisha ya chuo hata miaka 10, bado chuo ni kichanga. Najua watu waliosoma Computer Science batch ya 2009-2012, walikuwa hawana walimu. Na bahati mbaya walianza na kozi nyingi sana, bila kuwa na walimu.Bora wangekuwa hapa Dar, lecturers unaweza kukopa kiurahisi kutoka vyuo vingine sio Dodoma. Mwalimu anatoka UD kwenda Dodoma kufundisha. Kuna course jamaa walifundishwa 4 times semester nzima, ticha anakuja anafundisha 4 hrs straight, akimaliza anawapa na test mnafanya anapotea.

Watu waliosoma early years hasa hasa science walijuta
 
Taratibu Mkuu...! Ukiambiwa ulete ushahidi ...utautoa? Unajua uhovyo wa elimu kweli Mkuu?
Tafuta waliosoma miaka ya mwanzo wakuambie, mimi nawajua baadhi, story zao zinasikitisha. Ofcourse kama elimu kwako ni majengo, wanayo mazuri sana.

Haiwezekani mtu aliyesoma Telecom Engineering akalia njaa kiasi hicho, a properly trained Telecom engineer ana field nyingi sana ambazo zinahitaji watu hapa Bongo, asingekufa njaa.
 
Kuna watu tulisoma shule kama robots. Kujiongeza mpaka mtu fulani nje ya sisi atufinye kama kubonyeza remote.
Aisee unanikumbusha movie inaitwa three ideots Kuna mda jamaa ansema hiki unachosema anasema "we were studying like robots (while our friend caved his own way )"


Hapo nilipo fungia mabano ndo mzizi wa hii thread ambayo inaonyesha wakati wengine wanakazana kukariri matheory magumu magumu Kuna watu huko huko shuleni wao main concern yao haipo kwenye matheory wapo wanafocus nje ya mfumo rasmi wa elimu au tuseme wanawaza nje ya box au hata hata wapo busy na matheory hivyo ndo vitu wanapenda kwa hivyo hawawezi kukosa kujiajiri kwa sababu ndo vitu wanapenda hata Kama wakikosa ajira rasmi
 
Niliishia la saba wasomi nisaidieni maana ya hako kapicha
IMG-20190613-WA0010.jpeg
 
Mfumo mbovu wa elimu unazalisha wasomi wasiojiongeza, wanaishia kufilisika afya ya akili kwa msongo wamawazo. Huyu tayari akili yake haiko timamu, hata vibarua anavyopata anaishia kuacha na kubaki kuuza mkaa wamafungh! So sad!
 
Nahuyo yuko mbalitu na opportunities kubwa zaidi, angefika mbali mno!
Mpwa wangu alifaulu kwenda kidato cha V, shughuli ya kununua godoro, jembe, ndoo, sanduku ilikuwa mtihani. Aliwambia ndugu waache tu. aliamua kuwa mkulima.

Sasa hivi ana nyumba ya vyumba vitatu vya kulala ilijengwa kwa matofali ya kuchoma na kuezekwa kwa mabati, Ana mbuzi 100, shamba anapanda mahindi, mabamia yanampatia 10,000 kila siku asubuhi.
 
ni janga la dunia kwa hio tuwe comfortable tuache yanayoendelea kisa ni janga la dunia???embu tuweke comparison kati ya nchi na nchi?..lol....Elimu yetu haiwaandai watu kujiajiri....utajiajiri vipi wakati umekariri ma theories kwa lugha ya kigeni??? ajira ni tatizo..lakini relevant education inaweza ku offset tatizo la ajira.

Hebu anza kwa mfano dada, unadhani tufanye nini ili kuepuka na hili tatizo, halafu lawama utaleta baadae.
 
Yaani jamaa psychologically hayupo sawa.
Sawa akiwa na hao watu wa siasa ndio watazidi kumvuruga kabisa.
 
it is a puzzle indeed. But, hii sio mara ya kwanza kusikia hizi habari za wahitimu kukosa ajira,tuhangaike kutafuta ufumbuzi na sio kuignore magnitude ya hili tatizo..

Muwe mnaelewa, hajakosa ajira ila aliacha kazi ili akaishi na wadogo zake. Nazani karogwa au mlevi hajielewi huyo.
 
Maisha yetu yanachorwa na kipanya the artist ,mama zetu wametulea kwa kuuza bongo,kila kona ya mtaa kuna watu na viatu,

Watu hatuna kazi ila tunapata mahitaji matatu.

Kikubwa tabasamu na furaha tunaishi tuuu,

Sent from my E500 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom